CHADEMA Watofautishe “Utawala wa Sheria” na “Utawala wa Hisia”

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
CHADEMA Watofautishe “Utawala wa Sheria” na “Utawala wa Hisia”

Na Mwamba wa Kaskazini, Ngarenaro

*LEO kama kawaida yangu ya pilikapilika za hapa na pale nikiwa hapa kitaani kwangu nimesikiliza mijadala michache sana miongoni mwa wanaKaskazini kuhusu hukumu ya Mwenyekiti wa Chadema na wenzake ambayo imewaweka jela viongozi wanane.*

Viongozi hao wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenda jela au kulipa faini na mpaka leo walikuwa hawajaweza kulipa faini hiyo ingawa Chama na wapenzi wa Chama hicho wanakwenda mbio kukusanya michango kuwalipia faini viongozi hao watoke jela.

Kumeibuka malalamiko kuhusu hukumu hii. Nimejaribu kusikiliza hoja za mashabiki wa Chadema hapa Arusha sikupata msingi wa hoja kwa wale wachache wanaolalamika au kudhani kuwa viongozi hao wameonewa.

Nimesema wachache nikimaanisha hasa neno hilo kwa sababu nidhahiri shahiri kuwa hapa Arusha vijana wengi waliokuwa “busy” na masuala ya siasa huwaoni kwa sasa wakiendekeza hayo, labda wako busy na shughuli za kutafuta kipato.

*CHADEMA WanalalamikiaNini Hasa*

Katika kushangazwa na wafuasi wenzangu na viongozi wa Chadema nimehangaika kutafuta hoja imekuwa ngumu. Nimemsikia Lazaro Nyalandu mmoja wa viongozi wa Chadema anasema anaamini waliofungwa hawana makosa.

Lakini katika mkutano huo huo na wanahabari, viongozi wa Chadema wanaonekana kukosa hoja hasa na wanagongana kimtazamo, baada ya Benson Kigaila, kiongozi mwingine wa Kitaifa kusema makosa waliyofungwa nayo viongozi akina Mbowe ni ya kisiasa yakilenga kukidhoofisha Chama hicho.

Hapa nimetatizika, hizi kelele zinazosikika za kudai Mahakama haikutenda haki au akina Mbowe wameonewa, sababu ya kuamini hivyo ni zipi hasa? Ndio hizi kiongozi mmoja anasema hakuna makosa kabisa? Mwingine anasema yapo lakini ya kisiasa? Huku ndio kuleta siasa kwenye masuala ya kitaalamu.

Andiko langu leo sio la blah blah, nimeandika kuwashauri viongozi wetu wa Chadema moja kwa moja kuwa waachane na siasa za blah blah; waenzi na kuheshimu utawala wa sheria kwani Utawala wa sheria hauangalii Chama wala kabila wala dini au hali ya mtu.

Kama kweli wao ni watu wanaoenzi utawala wa sheria, kama wanavyoimba kila mara, walipaswa kushangilia hukumu hii , waishukuru Mahakama na wakamilishe tu vifungo vyao jela, walipe faini au wafuate mkondo wa kukata rufaa Mahakamani.


Utawala wa sheria unatuelekeza kila mtu kutii sheria na uamuzi wa vyombo vya kisheria, awe kiongozi awe mwananchi wa kawaida. Kwa mujibu wa hukumu, umekusanywa ushahidi wa mashahidi zaidi ya 30 na Mahakama imeona umejitosheleza kuwa Mbowe na wenzake walitemnda makosa ya jinai yapatayo 12 katika 13.

Nashauri badala ya kulalama viongozi wetu wakuu hawa wa Chadema wajifunze kuheshimu sheria za nchi, na kamwe wasitumie kesi hii kuitusi Mahakama au Serikali, hakutasaidia.

Kwangu ni kosa kubwa la kisiasa kwa Chama kinachotarajia kushika dola kubeza uhuru wa Mahakama ile ile ambayo imepata kuwapa wao wenyewe haki dhidi ya wengine na hata kama ni siasa Mahakama hiyo hiyo imepata kuwahukumu wanasiasa wa vyama vingine na hata wasio na vyama lakini hawakuporomosha makashfa kama haya.

*_Ni Kutaka Kuleta Utawala wa Hisia!_*

Utawala wa sheria ni msingi muhimu wa utawala bora ambao Mbowe na wenzake walipaswa kuuenzi. Hata hivyo, na kwa bahati mbaya sana, tunachokiona ni mwendelezo wa Chadema kuenzi dhana mpya na ya kijinga ya “Utawala wa Hisia.”

Ni aibu kwa kiongozi wa Kitaifa wa ngazi ya Benson Kigaila kuwaaminisha wana Chadema na hata watu walioko nje ya nchi kwamba akishtakiwa mtu wa Chadema au kuhukumiwa mtu wa Chadema ni siasa, wakikamatwa na kuhukumiwa wengine ni sawa.

Viongozi wetu wa Chadema wabebe msalaba wao kwa makosa yao katika hili kama ambavyo hata wanaCCM, chama tawala, nao wamepata kubeba mzigo wao kwa makosa yao. Labda niwakumbushe wanaharakati wenzangu:

Mosi, Mwaka 2015 wanachama wa Chama Tawala na pia mawaziri waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja walihukumiwa kwenda jela miaka mitatu.

WanaCCM Yona na Mramba walihukumiwa kifungo jela na kuanza kukitumikia hadi mwaka juzi walipotolewa ili kutumikia kifungo cha nje lakini Mgonja akaachiwa huru. Makosa ya jinai hayana Chama na hayaongozwi na hisia bali sheria. Chadema wajue hili.

Labda niwakumbushe tena miaka miwili au mitatu iliyopita aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa jana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Khamis naye alipandishwa kizimbani mjini Dodoma kwa makosa ya rushwa ingawa baadaye Mahakama iliifuta kesi hiyo.

Mahakama na makosa ya jinai yanaongozwa na sheria si hisia. Turejee hapa kuhusu kesi ya Sadifa: *_Redirect Notice

Katika awamu hii tena wabunge watatu wa CCM Kangi Lugora, Victor Mwambalaswa na Sadiq Murrad waliwahi kupandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam kwa tuhuma za rushwa: Kama Chadema wamesahau waangalie hapa *_http://mwanahalisionline.com/wabunge-wa-ccm-wapandishwa-kizimbani-kwa-rushwa/_*


Wengi bado mnakumbuka kisa cha kada wa CCM aliyekuwa pia Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Rajab Maranda, ambaye alishtakiwa na hata kufungwa kwa kosa la kushiriki wizi wa EPA. Lakini si Kigoma tu, kada mwingine wa CCM Kilimanjaro alishafungwa miaka 60. Soma hapa: *_https://www.jamiiforums.com/threads/kada-wa-ccm-lupango-kwa-kubak.6813/_*

Lakini pia Chadema na wanaharakati wenzangu tuwakumbushe kwamba wasibeze uhuru wa Mahakama kwa sababu leo wanasiasa hao wa upinzani wamekutwa na hatia. Tuwakumbushe tu mara kadhaa ni katika Mahakama hizi hizi wapinzani hao hao waliwahi kupata haki yao walipoonekana kutokuwa na hatia.

Kwa mfano Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Ndugu Mbowe, aliwahi kushinda rufaa dhidi ya kesi yake ya kudaiwa kumshambulia afisa wa uchaguzi wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Rejea hapa: *_Redirect Notice

Naye Mbunge wa Chadema (Mbozi), Paschal Haonga naye alipata kushinda kesi kwenye Mahakama hizi hizi wanazozitukana Chadema leo baada ya kushitakiwa kufanya fujo kwenye chumba cha ofisi ya uchaguzi. Angalia: *_https://www.tanzaniaweb.com/Tanzani...aswali-matatu-kesi-ya-Haonga-wenzake-433538_*

Wapinzani wanashtakiwa Tanzania tu? Majuu Je?

Ukiwasikiliza Chadema na baadhi ya mawakala wao wa nje, pia utabaini wanatafsiri ya kijinga ya wanapotenda makosa na kuchukuliwa hatua; kwamba wanashtakiwa kwa sababu ni wapinzani (wapo mbona wabunge kibao wa upinzani hawajawahi kushtakiwa?).

Lakini ukiitazama akili ya wanachadema pia utaona wanaona kushtakiwa wapinzani ni kama vile ni “Tatizo la Kiafrika.” Ngoja niwape mifano miwili tu ya kutoka huko kwa mabeberu mnakojikomba kijinga.

Nchini Uingereza mwaka jana tu mbunge wa Chama cha upinzani cha Labour kwa jimbo la Peterborough , Bibi Fiona Onasanya alifungwa jela miezi mitatu kwa udanganyifu. Soma hapa: *_https://www.theguardian.com/uk-news...a-onasanya-jailed-for-lying-speeding-ticket_*

Aidha, Katika historia ya Marekani, ambako eti akaunti ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Marekani nayo inaungana na ujinga huu kwa kushangaa hukumu hii, historia inaonesha katika zama zote za uongozi iwe Republican au Democrats wakiwa madarakani, wanasiasa wa vyama tawala na upinzani wamefunguliwa kesi na kufungwa mara kadhaa bila kujali itikadi zao bali makosa yao.

Soma hapa: *_Wikipedia, the free encyclopedia
List_of_American_federal_politicians_convicted_of_crimes. Ukisoma andiko hili utashangaa kuona wakati wa Rais Obama wa Democrats kuna wanasiasa wanaofikia nane (8) wa upinzani (Republicans) waliopata kufikishwa kortini na hata kufungwa kwa makosa mbalimbali.

Kwa kifupi ujumbe wangu kwa wanachedema na wanaharakati wenzangu leo ni mfupi tu: Chadema wajue kuna sheria na hisia na hata kama nami, kibinadamu, nimeguswa na ni miongoni mwa waliotuma mchango ili kina Mboiwe walipe faini watoke jela, huu ndio ukweli unaouma, lakini ukweli tunaopaswa kuukubali na kuuishi.

Niite Mwamba (sema mara tatu) wa Kaskazini.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tofautisha kutii Sheria Na kubambikwa ni vitu viwili tofauti. Utawala hauwezi kamilika kama wasababishi Wa tukio mkuregenzi Na polisi Wao wamelindwa hii ni dabo standard
Pamoja Na kulindwa still hatia ya mauaji ya bint haiwezi futika
 
Angehukumiwa baba yake au dada yake angezungumza huu urojo
Hajalazimishwa mtu kuchanga
Atoe upupu wake hapa
Wikipedia sekipedia mokapedia my foot!
 
Back
Top Bottom