Tanzania kukombolewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kukombolewa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Aug 21, 2011.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wimbi la kufichua wabadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka itaiwezesha kuokoa rasilimali za nchi na hivyo kuiokoa Tanzania?WanaJF tulio na nafasi kubwa serikalini tushirikiane kufichua maovu ili kuokoa kuvujwa kwa rasilimali za nchi yetu.Ebu tujadiliane juu ya hili kwani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nathani ni wazo mbadala, vita hii ni ya kwetu wote! Haya mlioko jikoni, pigeni photo copy ya ma document hayo ya kifisadi yamwageni hapa watu waumbuke.
   
 3. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Mi hoja yangu ni kwamba tuweke mfumo wa serikali tatu,tanganyika ijitoe ndani ya tanzania ili kuwe na serikali ambayo itasimamia rasilimali za tanganyika zote,na serikali ya muungano tuwe na wakilishi wachache ambao watatoka sehemu mbili za muungano tanganyika na zanzibar wakiwa idadi sawa kabisa ,kazi yao ni kuangalia hawa abao huhujumu uchumi wa nchi pamoja na rasilimali.

  Mbona hizi hujuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zanzibar hakuna ? Ni nyema viongozi wakachukua mfano zanzibar katika kukabiliana na hujuma hizi.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kufichua tu maovu sio dawa pekee... maana mpaka hapa maovu yalofichuliwa yanatosha kabisa kwa Serkali yoyote zalendo na yenye utambuzi kua ipo kwa ajili ya wananchi kuweza kabisa kujiuzulu toka ngazi ya juu hadi chini... yaani wahusika woote wakawa flushed... Lakini ni contrary mambo yanazikdi wekwa hadharani... wananchi hasira za zidi ongezeka lakini hamna la maana linalofanywa....
   
 5. NEW TANZANIA

  NEW TANZANIA Senior Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wataelewa tu hii nayoni dawa, tuwalimue waovu
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tujadiliane nini? wakati kila siku Hosea na Mwema wanasema fichueni maovu na tunasikia habari kila siku wakisifiwa raia waliotoa habari za ubadhirifu, wizi na mengineyo.

  JF ipo wazi masaa 24, kama huwezi peleka maovu PCCB au Polisi, yaanike humu. Hatua zitachukuliwa.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi naahidi kwa nafasi niliyonayo sitayafumbia macho maovu,wabadhirifu wote ninaowajua nitamwa ushahidi humu.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Umenena.
  Sisi watanzania ni watu wa ajabu sana...."Tunasubiri ushahidi kamili".
  Ubadhirifu na ufisadi ambao ushafichuliwa bado tunaamini wakati haujafika wa kuwashughulikia hawa watu badhirifus na fisadis na viongozi lege lege?

  Tanzania itakombolewa kutoka kwa nani? Mkapa aliimaliza kwa kuweka "tundu wazi" aka utanda wizi, aliyemfuatia anakamilisha miradi ya musee wa ukapa tu. Hii vita ya kuikomboa Tanzania ya leo ni nzito kuliko ile ya kupigania uhuru. Ndugu zetu wamekuwa maadui zetu na hatuna ujasiri wa kuua "nyani".
   
Loading...