Tanzania kujitoa Jumuiya ya COMMESA yasababisha zao la Tumbaku kupoteza soko mkoani Ruvuma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
TUMBAKU-550x292.jpg

Imeelezwa tangu tanzania ilipojitoa rasmi katika jumuiya za nchi wafanyabiashara kusini mwa bara la afrika(COMMESA)imepelekea kuyumba kwa soko la zao la Tumbaku baada ya wanunuzi wa zao hilo mkoani Ruvuma kujitoa na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa mali za ushirika kunakofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika na chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku cha Songea na namtumbo(SONAMCU).

Yasini Makunguru Kaimu Meneja chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa Tumbaku cha Songea Namtumbo(SONAMCU) ametoa changamoto hizo wakati wa ufunguzi wa ununuzi wa zao hilo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018.

Katika hatua nyingine baadhi ya wakulima wa zao hilo wilayani namtumbo wameipongeza serikali kwa dhamira ya kufufua kiwanda cha usindikaji wa zao hilo kilichopo mjini songea na kuongeza kuwa mpango huo utasaidia kuongeza thamani ya zao husika na kuongeza ajira kwa vijana.

Naye mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Dokta.Binilith Saatano Mahenge amesema kuwa utatuzi wa changamoto hizo tayari serikali imeshaanza kuchukua hatua ambapo,tayari mkataba kati ya kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Premium Tanzania Limited na serikali umesainiwa unaohusu ujenzi wa kiwanda cha kusindika tumbaku mjini songea badala ya kwenda kusindikia mkoani morogoro kama ilivyo hivi sasa.

Chanzo: ITV
 
itabidi viongozi wafanye tathmini mpya juu ya
athari za kutokuwa wanachama wa commesa.
 
Tanzania haikuwahi kujiunga na Comesa pamoja na kwamba ilishiriki kikamilifu katika mchakato ulioianzisha. Ulipofika wakati wa kuridhia mkataba ule Mwalimu Nyerere alikataa..
 
Back
Top Bottom