Tanzania inafanya kile kinachofanywa na raia wa Afrika Kusini kwa Waafrika wenzao kutoka Mataifa mengine

Unamaanisha hakuna Wakenya walioruhusiwa kufanya kazi TZ? Au hakuna hao unaoita 'Wazungu' walionyimwa vibali vya kufanya kazi TZ? Inaelekea huna taarifa za kutosha kutetea hoja yako.

Kupunguza hujuma za kibiashara kuna baadhi ya nafasi za kazi ni salama zaidi kupewa raia wa mbali huko maana ni rahisi kumdhibiti kuliko Mkenya. Fuatilia historia ya kufa kiwanda cha matairi (General Tire) Arusha, na changamoto za baadhi makampuni ya vinywaji hasa bia nchini.
Umeongea points sana...kuna baadhi ya vitu watu awajui kuwa mambo mengine ni kwa ajili ya taifa
 
achana na story za ccm hapa unachafua mjadala na kuonekana una rangi gani.

roho ya kwanini kwa sababu ipi??unaweza kujibu ji kwanini mtu ana roho ya kwanini juu ya wakenya?na si waganda na wasouth au wamisri??
Nimeongelea CCM maana ndio walioongoza hii nchi toka uhuru wetu. Nchi hii haijiendei kiholela bali kwa mfumo wa siasa tunaoongozwa nao ambao ni mfumo wa kiCCM. Wanachokitaka wao na mwenyekiti wao ndio na nchi itakavyoendeshwa. Wewe sema nina rangi flani lakini ndivo ilivyo. Na wala mimi sio mshabiki wa Upinzani bali ninahitaji maendeleo ya kweli ambayo CCM wameshindwa kuleta miaka 60 baada ya uhuru kutokana na siasa zao zisizotaka kubadilika kuendana na wakati. kila siku wanatafuta mbaya wao, tunakata miongo 6 sasa. Ilikua wakoloni, ikaja wapinzani, sasa ni wakenya. Kesho itakua nani?
Pia roho ya kwanini unaiona kwa mtu wa karibu kuliko wa mbali. Mimi hutonionea kwanini sababu hunijui na hatuna ukaribu lakini ikawa tofauti na rafiki, ndugu au jirani. Na wakenya ndio watu wa karibu yetu zaidi kijadi kuliko wamisri au wasouth. Watanzania wengi walio nje watu wao wa karibu sana hua ni wakenya mara nyingi Kuliko watu wengine. Hio ni kutokana ma historia yetu ya ukaribu.
Na ni ukweli wakenya wametuacha kwa sasa kiuchumi. Chuo cha UDSM kilikua bora EAC kuliko chuo cha Nairobi lakini sahvi kimetupwa kwenye world rankings. Kenya kitakwimu kina wanafunzi raia wa kigeni wengi kuliko sisi wote EA. Inamaanisha elimu yao ina ubora na kuaminika zaidi. Miundombinu yao ni bora zaidi kwa viwango vya kimataifa na sekta ya afya pia. Wao hawaforce kuja kufanya kazi Tanzania, makampuni makubwa wanawaamini na kuwachagua kuja kusimamia biashara zao huku. Tunakasirika tunawanyima vibali. Tunachekesha kwa kweli. Sasa bora tufanye hivo halafu tuboreshe elimu yetu ikidhi viwango vinavyohitajika. Hapana, tunafuja hela ya umma, elimu inaporomoka halafu tunaanza kulia lia kenya wanatuhujumu.
 
Wewe unazungumzia 'inawezekana' Serikali inafanya maamuzi baada ya kuzingatia 'uhalisia' uliyopo siyo 'inawezekana'
Hivyo kubaliana na maamuzi ya serikali. Kuna mengi usiyoyajua
 
Nimeongelea CCM maana ndio walioongoza hii nchi toka uhuru wetu. Nchi hii haijiendei kiholela bali kwa mfumo wa siasa tunaoongozwa nao ambao ni mfumo wa kiCCM. Wanachokitaka wao na mwenyekiti wao ndio na nchi itakavyoendeshwa. Wewe sema nina rangi flani lakini ndivo ilivyo. Na wala mimi sio mshabiki wa Upinzani bali ninahitaji maendeleo ya kweli ambayo CCM wameshindwa kuleta miaka 60 baada ya uhuru kutokana na siasa zao zisizotaka kubadilika kuendana na wakati. kila siku wanatafuta mbaya wao, tunakata miongo 6 sasa. Ilikua wakoloni, ikaja wapinzani, sasa ni wakenya. Kesho itakua nani?
Pia roho ya kwanini unaiona kwa mtu wa karibu kuliko wa mbali. Mimi hutonionea kwanini sababu hunijui na hatuna ukaribu lakini ikawa tofauti na rafiki, ndugu au jirani. Na wakenya ndio watu wa karibu yetu zaidi kijadi kuliko wamisri au wasouth. Watanzania wengi walio nje watu wao wa karibu sana hua ni wakenya mara nyingi Kuliko watu wengine. Hio ni kutokana ma historia yetu ya ukaribu.
Na ni ukweli wakenya wametuacha kwa sasa kiuchumi. Chuo cha UDSM kilikua bora EAC kuliko chuo cha Nairobi lakini sahvi kimetupwa kwenye world rankings. Kenya kitakwimu kina wanafunzi raia wa kigeni wengi kuliko sisi wote EA. Inamaanisha elimu yao ina ubora na kuaminika zaidi. Miundombinu yao ni bora zaidi kwa viwango vya kimataifa na sekta ya afya pia. Wao hawaforce kuja kufanya kazi Tanzania, makampuni makubwa wanawaamini na kuwachagua kuja kusimamia biashara zao huku. Tunakasirika tunawanyima vibali. Tunachekesha kwa kweli. Sasa bora tufanye hivo halafu tuboreshe elimu yetu ikidhi viwango vinavyohitajika. Hapana, tunafuja hela ya umma, elimu inaporomoka halafu tunaanza kulia lia kenya wanatuhujumu.

kenya haina jambo hata moja linaloweza kutumika kuhalalisha ubora wa elimu waliyo nayo.

huo uchumi wenyewe mashaka matupu,na kama hata katika maisha yako unapenda kuwatumia kama benchmark usishangae ukaendelea kuona maisha yako ni ya kuilaumu ccm mpaka unaingia kaburini.

hivi inahitaji elimu bora kama ya kenya unayoisema kulima ardhi bora iliyopo tanzania??
inahitaji uchumi mkubwa kama wa kenya kujenga miundombinu kama inayojengwa tz kwa sasa??
je inahitaji chuo kuwa namba mbili duniani ili kulinda amani na umoja uliopo??
na vipi je,inahitaji wasomi kwa idadi kama kenya ili kuwa na namba kubwa zaidi ya watu wenye utajiri zaidi EA???

lengo langu hapa ni kukumbusha,hizo namba na ranks mtu anaweza weka tu maadamu kaamua yeye anaziweka kwa vigezo gani.per capita yenyewe ni namba wakenya wanaonekana wako mbali sana mbele yetu,lakini angalia inatafutwaje ndio utagundua upuuzi ulipo kwenye ranks.

sisi kama tanzania hatuwezi kupangiwa namna ya kuishi,kama ambavyo hatupangii mtu,maslahi ya tz kwanza haijalishi weww unaonaje.
 
Endeleeni kuficha vichwa kwenye mchanga, ndo jadi yenu. Kwamba mtu tu anajiamulia kupanga ranks na kujiamulia tu ubora wa elimu bila vigezo maalum. Mnavoendesha mambo Tanzania kama vichwa maji sio nchi nyingine zinavoenda na wala sio mashirika makubwa yanayopanga hizo rankings yanavoenda. Lakini viburi ndo hulka ya Tanzania hii ya sasa. Tatizo linakuja mkikwama mnatafuta lawama kwa watu akati wenyewe mnaenda tu na vichwa maji. Mkigonga mwamba ndo mnaanza kelele na roho mbaya za kunyima watu vibali.
Mimi siishi maisha ya dhiki niko vizuri tu na hata mambo yakishindikana sana option ya kwenda nchi nyingine ipo. Naongea kwasababu najua maisha yangekua bora zaidi kama mambo kadhaa yangebadilika. Kuanzisha biashara na kupata leseni Tanzania ni tatizo, kodi na tozo ni tatizo. Hayo mambo siwezi kwamba nitayakimbia ila inanilazimu niendane na huu mfumo mbovu ambao hamna mwengine yeyote anayeutengeneza zaidi ya CCM. Hata nikiwa na bidii gani ya kazi bado kuna mambo ya kimfumo yatanikwamisha au kunichelewesha. Mimi najua adui yangu ambae ni mfumo wa nchi yangu. Wewe unaedhani adui ni mkenya unapoteza mda maana wao hawatoacha kua mabosi wa hayo makampuni makubwa kisa Rais hataki. Voda alinyimwa mkenya akapata mmisri. Unilever wakaamua kuhamishia shughuli za kiuongozi Nairobi huku wakabakisha utendaji tu. Mfumo wetu wa elimu na maisha bado mbovu na kunyima vibali kenya hakutosaidia na hakujasaidia.
 
gazeri refu sana lakini nikwambie tu,simchukulii mkenya kama adui yangu anayekwamisha mipango yangu.
haya ni maneno yako,na sijui umeyatoa wapi!!!

halafu kama hali ni duni kiasi unachosema,kwanini usiende kenya na kwingine unakoona kuna afadhali!!maana kulia lia unajizeesha bure mkuu.

yess kiburi ndio hulka ya mtanzania hasa ukimuonyesha ujuaji.ila mtanzania ni kondoo sana kwa watu wenye ubinaadam,hiyo ndio hulka yake.

labda niseme wewe ndio unaumizwa zaidi na swala hili sababu umekaa nalo kwa majibu yako,kunyimwa mkenya kwa vigezo vya kibali haimaanishi mganda naye anyimwe kwa vigezo hivyo.
 
kenya haina jambo hata moja linaloweza kutumika kuhalalisha ubora wa elimu waliyo nayo.

huo uchumi wenyewe mashaka matupu,na kama hata katika maisha yako unapenda kuwatumia kama benchmark usishangae ukaendelea kuona maisha yako ni ya kuilaumu ccm mpaka unaingia kaburini.

hivi inahitaji elimu bora kama ya kenya unayoisema kulima ardhi bora iliyopo tanzania??
inahitaji uchumi mkubwa kama wa kenya kujenga miundombinu kama inayojengwa tz kwa sasa??
je inahitaji chuo kuwa namba mbili duniani ili kulinda amani na umoja uliopo??
na vipi je,inahitaji wasomi kwa idadi kama kenya ili kuwa na namba kubwa zaidi ya watu wenye utajiri zaidi EA???

lengo langu hapa ni kukumbusha,hizo namba na ranks mtu anaweza weka tu maadamu kaamua yeye anaziweka kwa vigezo gani.per capita yenyewe ni namba wakenya wanaonekana wako mbali sana mbele yetu,lakini angalia inatafutwaje ndio utagundua upuuzi ulipo kwenye ranks.

sisi kama tanzania hatuwezi kupangiwa namna ya kuishi,kama ambavyo hatupangii mtu,maslahi ya tz kwanza haijalishi weww unaonaje.
Na kwa taarifa tu wakenya wengi sana wanakodi mashamba Tanzania wanalima wanapeleka mazao Kenya. Binafsi najua mkenya mmoja ana mgodi mererani. Kwahiyo elimu yao imewafanya waweze kulima na kumiliki migodi hadi vibarazani kwenu. Ndo maana nasema Tanzania mmepigwa mbali mno wenzetu wamechangamka mda mrefu.
kuhusu miundombinu acha nicheke tu. Kudhani kwamba hapa Tanzania tuna miundombinu ya maana ni ushamba. Kuna flyover huko nchi za Afrika zinajengwa za kilometer 27, nyie hio moja ya 0,5 km ndo mnaona miundombinu. Hilo bwawa la umeme wenzenu huko washajenga wakamaliza. Muwe mnakaa kufatilia na wengine wanaendaje sio kuangalia tu TBC mnaonekana washamba mbele za watu.
 
gazeri refu sana lakini nikwambie tu,simchukulii mkenya kama adui yangu anayekwamisha mipango yangu.
haya ni maneno yako,na sijui umeyatoa wapi!!!

halafu kama hali ni duni kiasi unachosema,kwanini usiende kenya na kwingine unakoona kuna afadhali!!maana kulia lia unajizeesha bure mkuu.

yess kiburi ndio hulka ya mtanzania hasa ukimuonyesha ujuaji.ila mtanzania ni kondoo sana kwa watu wenye ubinaadam,hiyo ndio hulka yake.

labda niseme wewe ndio unaumizwa zaidi na swala hili sababu umekaa nalo kwa majibu yako,kunyimwa mkenya kwa vigezo vya kibali haimaanishi mganda naye anyimwe kwa vigezo hivyo.
Tanzania ni kwetu. Mi ntaamua kukaa au kuondoka ntakapoona hamna wa kunipangia. Humu ni jamii forum ambapo mada inaekwa na mtu anatoa maoni anavoona inafaa. Hii forum inamilikiwa na Max Mello, si wewe. akinikataza yeye ndo ntaacha. Ililetwa mada, wengine naona mkashuka na maoni yenu juu ya wakenya na mimi nimeshuka na maoni yangu juu ya serikali yangu. Silii wala kupungukiwa sana, ni mitazamo kama mingine.
 
Na kwa taarifa tu wakenya wengi sana wanakodi mashamba Tanzania wanalima wanapeleka mazao Kenya. Binafsi najua mkenya mmoja ana mgodi mererani. Kwahiyo elimu yao imewafanya waweze kulima na kumiliki migodi hadi vibarazani kwenu. Ndo maana nasema Tanzania mmepigwa mbali mno wenzetu wamechangamka mda mrefu.
kuhusu miundombinu acha nicheke tu. Kudhani kwamba hapa Tanzania tuna miundombinu ya maana ni ushamba. Kuna flyover huko nchi za Afrika zinajengwa za kilometer 27, nyie hio moja ya 0,5 km ndo mnaona miundombinu. Hilo bwawa la umeme wenzenu huko washajenga wakamaliza. Muwe mnakaa kufatilia na wengine wanaendaje sio kuangalia tu TBC mnaonekana washamba mbele za watu.

nashangaa unayajua haya halafu unalia lia tunawabagua wakenya.kwani shida yako ni nini na watanzania!!!budaa sisi kufanya yale kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu wewe unaumia!!!,utakufa kwa pressure siku si zako.

hiyo flyover ya 27 km ni yao sio yetu,wacha wajione wamefika,sisi tunakuja kweli kweli na mida si mrefu mshamba OG atajulikana tu.

so take a peel.
 
Tanzania ni kwetu. Mi ntaamua kukaa au kuondoka ntakapoona hamna wa kunipangia. Humu ni jamii forum ambapo mada inaekwa na mtu anatoa maoni anavoona inafaa. Hii forum inamilikiwa na Max Mello, si wewe. akinikataza yeye ndo ntaacha. Ililetwa mada, wengine naona mkashuka na maoni yenu juu ya wakenya na mimi nimeshuka na maoni yangu juu ya serikali yangu. Silii wala kupungukiwa sana, ni mitazamo kama mingine.

sasa kama tanzania yetu sote na hakuna wa kumpangia mwenzie namna ya kuishi wewe ni nani,wa kuhoji kwanini tunamchukulia fulani namna hii!!!

kama unadhani hujawa tayari kuondoka maana yake hujasokotwa na maisha magumu ya hapa kisawa sawa,hivyo usijaribu kuilisha akili yako usichokiamini.

endelea kuishi hapa,na mengine achia watu wafanye kazi zao,wacha kuwa msemaji sana.
 
Linchi la double standards....

Ikiongozwa na joka la double standard lenyewe......

Bure kabisa
We kweli hamnazo... Nimefanya kazi Kenya kwa miaka miwili in managerial position na kwa bahati nzuri nilifanikiwa sana kufikia malengo lakini vita niliyokuwa napigwa ilibidi niondoke tu.

Ni majirani zetu tunawapenda ila linapokuja swala la utaratibu wa kuomba permit kuna criteria nyingi za kuangalia ili kuona ni muhimu kiasi gani kuruhusu mtu kuingia nchini kwenye higher position za kampuni pia kuna maswala ya usalama, taarifa uhalifu za mtu nk.. ndio maana ya ku-submit Police clearance certificate nk. So Kama kwenye screening kukawa na shida wizara ya kazi haiwezi kutoa maelezo zaidi ya kumkatalia expert yeyote. Kama Mmisri ana ziada sioni shida nae simwafrika shida iko wapi?!!?😆
 
nashangaa unayajua haya halafu unalia lia tunawabagua wakenya.kwani shida yako ni nini na watanzania!!!budaa sisi kufanya yale kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu wewe unaumia!!!,utakufa kwa pressure siku si zako.

hiyo flyover ya 27 km ni yao sio yetu,wacha wajione wamefika,sisi tunakuja kweli kweli na mida si mrefu mshamba OG atajulikana tu.

so take a peel.
I won’t and I’ll keep talking about the tragedy of this country. I’m in my house eating fried chicken and a cold beer, come and beat me.
 
Nimesoma mahali Watanzania wanashangilia sana Raia wa Kenya aliyekuwa awe Mkurugenzi wa Cocacola Kwanza kuzuiwa na uhamiaji. Watu wanashangilia sana kana kwamba sasa maisha yao yanaenda kubadilika.

Ila kinachonishangaza ni kwamba Kwenye Makampuni mengi ya hawa wafanya biashara wenye asili ya Asia wamejaza Watu wa nje kibao.MO na watu wa Asia kibao kwenya nafasi za juu. Arusha nenda kule A to Z kuna Wa Asia kibao hata kiswahili hawajui na cha ajabu sio Expert.

Arusha ukienda pale Culture Heritage Arusha, kuna walinzi wametolewa Nepali na uhamiaji ikatoa kabisa kibali, Kampuni nyingi za kitalii Arusha zina wazungu unakuta mzungu ni Mhasibu au ndo Meneja. Kuna Wazungu wengi mno Arusha wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya ila cha ajabu hata sisi hatulalamiki bali tunalalamikia Waafrika wenzetu Wakenya au Waganda.

Sasa kwa nini Uhamiaji inadili na hawa wanaotokea Kenya tu na kuwaacha hao wa Asia na Ulaya?
logic ni ipi hapa? au ndo sheria inavyosema kwamba wadili na wakenya pekee?

Huu ni ubaguzi sawa na ule unaofanywa na Waafrika Kusini, badala wapambane na Wazungu wao wanapambana na Waafrika wenzao, kwamba maisha yao magumu yanasababishwa na Waafrika wenzao na wala sio Makaburu.

Wabongo tunashangilia sana Uhamiaji kudili na Wakenya ila wale Wa Asia na Wazungu waliojazana huku tunaona ni sawa kabisa.

Fikiria Walinzi wanatolewa sijui Nepal then tunaona ni sawa kabisa.

Chuki zitatumaliza tusome tutafute Exposure
Kenya wanaenda kununua mahindi Mexico wanaacha ya kwetu jirani tena bei chee, hapo unaona je ni sawa?
 
Miaka karibu 20 kampuni ina operate ndani ya Tanzania ata kama hatukua na watu wenye calibre za C.E.O walikuwa na muda wa kutosha kufanya succession planning kumpata mtanzania atakae ongoza baadae.

Mbona CRDB bank yenye faida kubwa na MNB wameweza, muda wa ma C.E.O ulipofika wa kustaafu walienda ‘gardening leave’ wakawaachia watanzania washike hizo nafasi katika kipindi icho interim transition walikuwa assessed kama wanatosha na mwishowe kupitishwa na body zao kama wakurugenzi wapya wa mashirika makubwa.

Same ifike wakati sasa Dangote, Vodacom na wengine waanze kuweka policies za succession planning kwa nafasi za juu kuwajengea uwezo wa Tanzania inatosha sasa kutuletea wageni.

Ila na sisi tubadilike tuachane na culture ya ushamba kujifanya tunajua sana kupiga deal kwenye kila nafasi tunazopewa na kulemaza ukuaji wa biashara. Tabia zetu nazo zinachangia kutoaminika kuliko uwezo wetu.
 
Back
Top Bottom