Tanzania inafanya kile kinachofanywa na raia wa Afrika Kusini kwa Waafrika wenzao kutoka Mataifa mengine

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
2,240
2,000
Nimesoma mahali Watanzania wanashangilia sana Raia wa Kenya aliyekuwa awe Mkurugenzi wa Cocacola Kwanza kuzuiwa na uhamiaji. Watu wanashangilia sana kana kwamba sasa maisha yao yanaenda kubadilika.

Ila kinachonishangaza ni kwamba Kwenye Makampuni mengi ya hawa wafanya biashara wenye asili ya Asia wamejaza Watu wa nje kibao.MO na watu wa Asia kibao kwenya nafasi za juu. Arusha nenda kule A to Z kuna Wa Asia kibao hata kiswahili hawajui na cha ajabu sio Expert.

Arusha ukienda pale Culture Heritage Arusha, kuna walinzi wametolewa Nepali na uhamiaji ikatoa kabisa kibali, Kampuni nyingi za kitalii Arusha zina wazungu unakuta mzungu ni Mhasibu au ndo Meneja. Kuna Wazungu wengi mno Arusha wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya ila cha ajabu hata sisi hatulalamiki bali tunalalamikia Waafrika wenzetu Wakenya au Waganda.

Sasa kwa nini Uhamiaji inadili na hawa wanaotokea Kenya tu na kuwaacha hao wa Asia na Ulaya? Logic ni ipi hapa? au ndo sheria inavyosema kwamba wadili na wakenya pekee?

Huu ni ubaguzi sawa na ule unaofanywa na Waafrika Kusini, badala wapambane na Wazungu wao wanapambana na Waafrika wenzao, kwamba maisha yao magumu yanasababishwa na Waafrika wenzao na wala sio Makaburu.

Wabongo tunashangilia sana Uhamiaji kudili na Wakenya ila wale Wa Asia na Wazungu waliojazana huku tunaona ni sawa kabisa.

Fikiria Walinzi wanatolewa sijui Nepal then tunaona ni sawa kabisa.

Chuki zitatumaliza tusome tutafute Exposure
 

Satu

Senior Member
Nov 22, 2013
183
500
Unamaanisha hakuna Wakenya walioruhusiwa kufanya kazi TZ? Au hakuna hao unaoita 'Wazungu' walionyimwa vibali vya kufanya kazi TZ? Inaelekea huna taarifa za kutosha kutetea hoja yako.

Kupunguza hujuma za kibiashara kuna baadhi ya nafasi za kazi ni salama zaidi kupewa raia wa mbali huko maana ni rahisi kumdhibiti kuliko Mkenya. Fuatilia historia ya kufa kiwanda cha matairi (General Tire) Arusha, na changamoto za baadhi makampuni ya vinywaji hasa bia nchini.
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,599
2,000
Tofauti ipo hapa,Wazungu,wahindi,Waarabu wakija,wanachukua kazi zetu,wanatulipa kiduchu,sawa,lakini kampuni inaendelea kuwepo,Richa ya kutulipa wazawa kiduchu

Wakenya,wakija,ukawapa ukurugenzi,Cha Kwanza ni kuihujumu kampuni kwa ndani mpaka Ife,hata vile vimishahara vidogo havitakuwepo,Then kampuni inakufa,bidhaa zilizokuwa zinazalishwa,zinaanza kuagizwa kutoka Kenya,Wakenya wengi wanaokuja kuwa bongo ni maspy,mashushushu wa kiuchumi,wanatumwa waangamize uchumi wetu,sisi hatushindani na India,au UK,au SA kiuchumi,ila Hawa Kenya,tunavita nao,Ebu fikiria Mchina aajiriwe Microsoft,au google,General motor ,au MacDonald,kule USA Kama CEO!FBI,CIA,Homeland security,State deaprtment,secret service zote zitapinga kabisa Hilo Swala.
 

Babu la Bara

JF-Expert Member
May 24, 2017
530
1,000
Wahindi, Wazungu, Wamisri au Wanepal si washindani wetu kibiashara. Katika mataifa hayo, taifa linaloongoza hasa watu wake kutuharibia biashara ni Wakenya. Rejea Covid, Mlima Kilimanjaro, utalii, Ndege, n.k.

Wakenya wengi wanakuja kuua biashara zetu kwa kuyumbisha na kutoa siri muhimu za kiushindani wa kibiashara kwa makampuni ya kwao.

Kuna Mtanzania ni CEO wa kampuni kubwa Kenya? Ki ubinadam utawatetea ila ni watu hatari kuliko hata hao uliowataja. Hatari ya mhindi kwa Tanzania ni ndogo kuliko Mkenya. Ni wabaguzi na wana asili ya ukabila, hasa kwenye kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom