MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Celebrity au supastar kwako ni mtu wa aina gani? Maana halisi ya neno celebrity ukiangalia kwa wenzetu walioendelea ni mtu maarufu, mwenye pesa za kutosha ambae ana ushawishi katika jamii e.g Oprah Winfrey, Tom Cruise, Angelina & Brad Pitt et. Hawa wote ni watu wenye umaarufu na pesa na pia wana ushawishi mkubwa katika jamii kuanzia mavazi mpaka kupata support ya watu kwenye mambo mbali mbali wanayo amini, Je Tanzania tunao watu wa namna hii?
Ukiangalia bongo yetu "celebrities" wetu ni umaarufu tu lakina hamna mwenye pesa au ushawishi mkubwa. Kwa pesa nakubali ni kutokana na hali ya kiuchumi nyumbani na wasanii wetu kutokuwa na mvuto wa kimataifa. Ikija kwenye ushawishi sioni msanii yoyote ambaye yupo passionate about anything na akashawishi jamii iliangalie hilo swala kwa umakini zaidi. Kila siku wanamziki wetu au waigizaji wetu utakuta wana jifanye matawi kuliko hali yao ya kweli. Leo tunasikia mtu akiji sifia ana hela kesho tunasikia ni omba omba. Japo wapo wasanii walio jitosheleza ni wachache sana.
Don't get me wrong, I am not taking anything away kutoka kwa hawa wasanii lakini ni muda wakaacha kujipa sifa zisizo zao. Kuna tulio wasikia wakijiita J-lo wa Tz leo hii hawana be wala che. Kuna waliojiita wakina p diddy lakini hakuna lolote. Wana jilinganisha na hawa wasanii wakubwa wakati hawalingani chochote kuanzia soko, mashabiki wala maisha. Msanii anaenda nje kufanya show anarudi akisema ametoka kwenye tour ya kimataifa. Tour gani ya kimataifa na wakati idadi kubwa ya wanaoenda kwenye show zenu za nje ni wa East Africa waishio majuu? Ila wakirudi watajifanya kama vile show zao zilitangazwa kwenye vyombo vya habari za huko nje na kupokelewa kama wafalme.
Macelebrity wa nje wana magari ya kifahari na madereva wao, wasanii wa bongo wana panda dala dala na sisi au kuazima magari lakini sifa sasa. Sikatai kuna wenye magari yao lakini majority ni wenzetu na sisi. Inabidi waache kujipa ujiko wasizo stahili. Usupastaa una faida gani kama kesho ukifa kisanii hauna chochote? Kuna faida gani ya umaarufu wa bure? Ila ni kawaida ya watz sisi kujifanya tuna maisha bora kuliko tuliyo nayo.
Naamini kabisa usanii Tz unaweza ukawa deal kama mazingira yaliyopo yaka badilika. Leo hii msanii hana njia yoyote ya kujua kwa uhakika kauza copy ngapi. Leo hii msanii hana kipato cha uhakika bali anategemea awe juu kwa wakati huo apewe mialiko mbali mbali. Yes na sisi tunaweza kuwa na macelebrity lakini siyo hawa waliopo sasa. Waache kiburi na zarau wakati baada ya kutamba miaka michache wanasota mitaani na watu huwasahau. Nilishangaa kweli kusikia TID anaomba hela wakati yeye ndiyo mmoja wa wasanii wanaosadikika kuwa juu tena kwa muda mrefu. Mr. Nice aliye kuwa akisemekana kuwa mwana bongo flava tajiri kuliko wote sijui kaishia wapi.
Tatizo mimi naona ni sifa zina ponza. Hela wana tengeneza ila mtu aki tengeneza vijisenti tu anataka kujionyesha na kuanza kumwaga mihela mpaka zinaisha. Nina uhakika wanaweza kutengeneza pesa za kutosha kwa kiwango cha kwetu sema maarifa zero. Jamani umaarufu usiyo na mafao ya nini?
Tunaishi katika mazingira tofauti na hawa macelebrity wa njee kwa hiyo mambo ya kutaka kushindana nao au kuji linganisha nao tuta jiponza bure. We are not there yet. Kwa sasa tuna watu maarufu lakini siyo macelebrity. Nje ya kazi zao sioni wakifanya kitu. Maybe ni mazingira ya usanii Tz ndiyo yana sababisha mtu akipata umaarufu kidogo ajione kaula bingo lakini that is far from the truth. Wasanii kazeni buti, tengenezeni maisha ili muda mlioutumia kuwa wasanii usiwe wa bure mnapo staafu. Umaarufu utaisha ila ukiji jengea maisha mazuri matunda yatajionyesha kwa muda mrefu. Anyways haya maoni yangu tu.