Tanzania ina macelebrity wa kweli?

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Celebrity au supastar kwako ni mtu wa aina gani? Maana halisi ya neno celebrity ukiangalia kwa wenzetu walioendelea ni mtu maarufu, mwenye pesa za kutosha ambae ana ushawishi katika jamii e.g Oprah Winfrey, Tom Cruise, Angelina & Brad Pitt et. Hawa wote ni watu wenye umaarufu na pesa na pia wana ushawishi mkubwa katika jamii kuanzia mavazi mpaka kupata support ya watu kwenye mambo mbali mbali wanayo amini, Je Tanzania tunao watu wa namna hii?

Ukiangalia bongo yetu "celebrities" wetu ni umaarufu tu lakina hamna mwenye pesa au ushawishi mkubwa. Kwa pesa nakubali ni kutokana na hali ya kiuchumi nyumbani na wasanii wetu kutokuwa na mvuto wa kimataifa. Ikija kwenye ushawishi sioni msanii yoyote ambaye yupo passionate about anything na akashawishi jamii iliangalie hilo swala kwa umakini zaidi. Kila siku wanamziki wetu au waigizaji wetu utakuta wana jifanye matawi kuliko hali yao ya kweli. Leo tunasikia mtu akiji sifia ana hela kesho tunasikia ni omba omba. Japo wapo wasanii walio jitosheleza ni wachache sana.

Don't get me wrong, I am not taking anything away kutoka kwa hawa wasanii lakini ni muda wakaacha kujipa sifa zisizo zao. Kuna tulio wasikia wakijiita J-lo wa Tz leo hii hawana be wala che. Kuna waliojiita wakina p diddy lakini hakuna lolote. Wana jilinganisha na hawa wasanii wakubwa wakati hawalingani chochote kuanzia soko, mashabiki wala maisha. Msanii anaenda nje kufanya show anarudi akisema ametoka kwenye tour ya kimataifa. Tour gani ya kimataifa na wakati idadi kubwa ya wanaoenda kwenye show zenu za nje ni wa East Africa waishio majuu? Ila wakirudi watajifanya kama vile show zao zilitangazwa kwenye vyombo vya habari za huko nje na kupokelewa kama wafalme.

Macelebrity wa nje wana magari ya kifahari na madereva wao, wasanii wa bongo wana panda dala dala na sisi au kuazima magari lakini sifa sasa. Sikatai kuna wenye magari yao lakini majority ni wenzetu na sisi. Inabidi waache kujipa ujiko wasizo stahili. Usupastaa una faida gani kama kesho ukifa kisanii hauna chochote? Kuna faida gani ya umaarufu wa bure? Ila ni kawaida ya watz sisi kujifanya tuna maisha bora kuliko tuliyo nayo.

Naamini kabisa usanii Tz unaweza ukawa deal kama mazingira yaliyopo yaka badilika. Leo hii msanii hana njia yoyote ya kujua kwa uhakika kauza copy ngapi. Leo hii msanii hana kipato cha uhakika bali anategemea awe juu kwa wakati huo apewe mialiko mbali mbali. Yes na sisi tunaweza kuwa na macelebrity lakini siyo hawa waliopo sasa. Waache kiburi na zarau wakati baada ya kutamba miaka michache wanasota mitaani na watu huwasahau. Nilishangaa kweli kusikia TID anaomba hela wakati yeye ndiyo mmoja wa wasanii wanaosadikika kuwa juu tena kwa muda mrefu. Mr. Nice aliye kuwa akisemekana kuwa mwana bongo flava tajiri kuliko wote sijui kaishia wapi.

Tatizo mimi naona ni sifa zina ponza. Hela wana tengeneza ila mtu aki tengeneza vijisenti tu anataka kujionyesha na kuanza kumwaga mihela mpaka zinaisha. Nina uhakika wanaweza kutengeneza pesa za kutosha kwa kiwango cha kwetu sema maarifa zero. Jamani umaarufu usiyo na mafao ya nini?

Tunaishi katika mazingira tofauti na hawa macelebrity wa njee kwa hiyo mambo ya kutaka kushindana nao au kuji linganisha nao tuta jiponza bure. We are not there yet. Kwa sasa tuna watu maarufu lakini siyo macelebrity. Nje ya kazi zao sioni wakifanya kitu. Maybe ni mazingira ya usanii Tz ndiyo yana sababisha mtu akipata umaarufu kidogo ajione kaula bingo lakini that is far from the truth. Wasanii kazeni buti, tengenezeni maisha ili muda mlioutumia kuwa wasanii usiwe wa bure mnapo staafu. Umaarufu utaisha ila ukiji jengea maisha mazuri matunda yatajionyesha kwa muda mrefu. Anyways haya maoni yangu tu.
 
Asante manyendi kwa maneno mengi.
Sasa umetupa changamoto ya kutafuta jina la hawa wasanii wetu ..
Maana si ma supa staa kama ulivyosema wewe
 
kwa maelezo yako naona kama tanzania haina ma-celeb....ila kwani kipimo cha uceleb ni pesa peke yake?..au influence na moyo wa kusaidia jamii peke yake?..na amini u-celebrity ni vyote kwa pamoja....kwa mfano jayz alikuja tanzania kipindi flan akaenda kuzindua kisima cha maji(borehole) iliyochimbwa nadhani kwa udhamini wa vodaco kilikuwa na thamani ya 7m...SWALI kwa uceleb wa jay z.....hata mie nisingezindua kisima cha dola 6000 kama kile..na mbaya zaidi kumtwika ndoo ya maji mama wa kitanzania wakati wa uzinduzi wa hicho kisima iliniuma sana....jayz kwa mantiki hiii na mtazamo wangu wa celeb ni hafai kuitwa hivyo hata kama ana-mabilion ya dola bank..anatakiwa aitwe TAJIRI full stop...Kwa level yetu tanzania...wapo watu ambao wana moyo wa kusaidia na ni influential kwa jamii ila hawana pesa hata kama matajiri kibao kina jay wetu..hawa nao wanakosa sifa ya kuwa maceleb (NYERERE...samahani kama watz wenzangu mfano huu utakuwa umewaudhi,) nyerere alijitolea mpaka damu ya watanzania kuikomboa africa yote..pamoja na umasikini wetu watanzania....twende kwa wasanii wetu...UMAARUFU KUNUKA....aliwahi kusema huyu mchekeshaji anaitwa ZEMBWELA...masuperstaa/ma-celeb wa kibongo wote wanajitafutia UMAARUFU ambao hawana jinsi ya kuutumia na jamii iliyowazunguka hawaoni faida ya umaarufu wao zaidi ya kero na kelele zao..UMAARUFU KUNUKA...ndio haooo kila siku mizinga ila magari ya kutembelea wanayo..wengine ndio hao kila siku wanadaiwa KUOLEWA na mi-mamaa sukari tele ya mjini na nje ya nchi (sex-slaves)...in short MAARUFU TANZANIA WAPO ZAIDI YA MILLION 10, MATAJIRI ZAIDI YA MILLIONI 10 ILA MACELEB HAWAFIKI HATA 10...huyu mangi mengi naona anaelekea kwenye u-celeb, mwingine nani...bakhresa, ....naona wameisha sasa....ni maoni tuu si unajua WE DARE TO TALK OPENLY...especially our hearts and inner parts of our brains
 
Sikusema maceleb wa kwetu lazima wawe kama wa nje ila ninacho sema mimi wakwetu wanapenda kujikweza. Wanajipa sifa wasizo stahili na kama ulisoma thread yote utagundua nilisema wasanii wetu wenyewe ndiyo wanapenda kuji linganisha na wanje.
 
Kwani ni lazima wa kwetu wawe sawa na wa huko?

Kama umesoma vizuri thread utagundua nilisema specifically kuwa wkwetu hawawezi kuwa kama wa huko. Nilicho sema mimi ni tabia ya wasanii wetu kujikweza. Ntu anaenda kwenye show nje anarudi anasema as if hio shoo ilikuwa big deal huko alipoenda wakati sana sana itakuwa walienda wa east afrika tu na baadhi ya watu wachache wenyeji ambao labda wata waalika.
Au unakuta msanii ana jisifia utajiri au kutaka kuona kana matawi ya juu na si ndiyo hao tunaona baadhi yao wanakuja kuishiwa kabisa mpaka kuomba omba?
Lets call it as it is Tanzania hatuna macelebrity tuna wellknown people ukiacha wachache sana.
 
Watanzania wengi ni malimbikeni tu. Lakini sio kosa lao, wanapata umaarufu ghafla mno kiasi kwamba wanashindwa kuumudu. Nchi zilizoendelea wanaadaliwa kisaikolojia kwanza kabla. Mfano kabla ya kuingia NBA unafundishwa mambo mengi ukiwa college ikiwemo Financial Literacy and Management. Lakini pia kuna watu maarufu wa USA na wameanguka kiuchumi kama Mike Tyson. Alifika mahali akawa anapigana ili tu apate pesa za kuendelea kuishi!

Watanzania sio hao wanamuziki na waigizaji tu, pia hata wafanyabiashara uchwara ni malimbukeni balaa. Unakuta mtu ana salon mbili za kunyolea nywele, mbili za kutengeneza nywele wanawake, na gari lake Baloon la mtumba. Basi kelele tupu, atakuwa na simu tatu za gharama, kuvaa mikufu ya dhahabu, kuwapa wanamuziki pesa wamuimbe kwenye nyimbo zao...yaani kero tupu. Matokeo yake biashara zinakufa na hamumsikii tena.

Yuko wapi limbukeni Jack Pemba?

Celeb wa kweli Bongo ni Masoud Kipanya peke yake...Anajimudu kimaisha, hana papara, mjasiriamali, ana familia yake na ana ushawishi mkubwa kwenye jamii kwa kutumia katuni zake na hata vipindi anavyotangaza redioni!
 
Watanzania wengi ni malimbikeni tu. Lakini sio kosa lao, wanapata umaarufu ghafla mno kiasi kwamba wanashindwa kuumudu. Nchi zilizoendelea wanaadaliwa kisaikolojia kwanza kabla. Mfano kabla ya kuingia NBA unafundishwa mambo mengi ukiwa college ikiwemo Financial Literacy and Management. Lakini pia kuna watu maarufu wa USA na wameanguka kiuchumi kama Mike Tyson. Alifika mahali akawa anapigana ili tu apate pesa za kuendelea kuishi!

Umesema wakwetu wanapata umaarufu ghafla kwani wenzetu hakuna wanaopata umaarufu ghafla? Wapo wengi tu na huko wanaopata umaarufu ghafla.
Umesema nchi walizo endelea wanaandaliwa kisaikolojia kwanza unamaanisha maisha kiujumla au kupata umaarufu tu? Maan umetoa mfano wa chuo sijui NBA wakati si kweli kuwa kila celebrity wa marekani au ulaya wamepitia chuo na mifano ipo mingi tu tena kuna wengine hata kumaliza high school hawaku maliza.

Otherwise mkuu nakubaliana na kila kitu kingine ulicho sema. Tanzania malimbukeni wengi. Pesa kidogo tu mtu anaanza kumwaga hela kila sehemu aonekane ana uwezi kuliko hata alio nao mwishoni ni kufilisika tu. Ni wachache sana wanaoona mbele na ni wachache sana wanaokua wajasiriamali. umetoa mfano mzuri sana wa bwana Kipanya.
 
Masaki umeuliza wapi Jack Pemba,kuimbwa kwenye kila nyimbo na kumbi za burudani inahitaji gharama tena ya kila mara au hawakuimbi,halafu kuvisha pete wasichana 3-5 bila kuoa pia kunahitaji gharama kubwa.
 
kama silazima wawe sawa na wa kule Ulimwengu wa kwanza, sasa inakuwaje wanajipachika majina kama hilo macelebrite ,wakati hawana viwango hivyo.


wanajipachika majina kama yapi ambayo yanakukera mkuu??
as far as i am concerned tuna utofauti mkubwa sana na wamarekani(na dunia ya kwanza in general) kwenye kila kitu,KILA KITU..kila mahali kuna viwango vyake katika nyanja zote..kuna celebrity wa bongo na celebrity wa marekani mkuu!sivyo hata Dar halina hadhi ya kuitwa jiji basi sababu kuna NYC,London,Paris nk ambayo nayo ni majiji lakini kwa utofauti mkubwa mno na letu...najua unanielewa!
najaribu kusema kwamba,kwa viwango vyetu wao ni celebrities...
ni mtazamo tu!
 
...kuna NYC,London,Paris nk ambayo nayo ni majiji lakini kwa utofauti mkubwa mno na letu...

Sijui pia kama unakumbuka kuwa kuna megacity, metropolitan etc... Some of the mensioned majijis are actually megacities and metropols
 
Amber Rutty ni celebrity na Steve Nyeyere ni super star, kama hatutaki kaa hukohuko Marekani kwenu.
 
wanajipachika majina kama yapi ambayo yanakukera mkuu??
as far as i am concerned tuna utofauti mkubwa sana na wamarekani(na dunia ya kwanza in general) kwenye kila kitu,KILA KITU..kila mahali kuna viwango vyake katika nyanja zote..kuna celebrity wa bongo na celebrity wa marekani mkuu!sivyo hata Dar halina hadhi ya kuitwa jiji basi sababu kuna NYC,London,Paris nk ambayo nayo ni majiji lakini kwa utofauti mkubwa mno na letu...najua unanielewa!
najaribu kusema kwamba,kwa viwango vyetu wao ni celebrities...
ni mtazamo tu!
Post murua kabisa bro, kuna time huwa najiuliza huw najiuliza hivi inakuwaje kuna thread hazina logic kabisa kama hii.

Ni ujinga kulinganisha dunia ya kwanza na ya tatu katika usasa.Tunazidiwa almost kila kitu utawala,miundombinu,elimu,exposure,democracy,mpira,starehe,teknolojia yaani kila kitu.Sasa unashangaa nini kwenye hili bro?

Unashangaa kushindwa kutangazwa huko nje wanapoenda kupiga show.Bro hii ni dunia ya Samaki mkubwa kumla mdogo.Habari inayotangazwa na CNN au BBC huwezi linganisha inavyofatiliwa duniani na iliyotangazwa na TBC au KBC.

Kuhusu kujisifu ni hulka ya binadamu waliyonayo wengi tu mbali ya wasanii.Kinachowaponza wasanii ni kwamba wao ni maarufu hivyo taarifa zao kusambaa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom