Maendeleo101
Member
- Nov 5, 2010
- 5
- 0
Midaharo yote iliyoendeshwa karibia kipindi chote cha kampeni imeleta changamoto kubwa sana.Hata hivyo mdahalo kuhusu kambi ya upinzani ndani ya bunge umekuwa wa aina yake hasa katika kuonyesha ni jinsi gani wanasiasa walio wengi bado hawajakomaa au basi hawajui kanuni na taratibu za midahalo kama hiyo.
Nimesikitishwa sana kuona watu walivyo na jaziba katika mambo madogo sana ya kutofautiana kwa hoja.Wale wenye uchanga wa namna hii wa kuhamaki kwa hoja aliyotoa mtu bila kugusa nafsi ya mtu fulani wachukue muda wao wajifunze kutoka wa midahalo ya wenzetu,hasa Wamarekani na Waingereza.
Tunapokuwa kwenye midahalo kama hiyo nguvu ya hoja ndo inayotawala sio kutoa mafumbo ya matusi ambayo watu walio makini watayatasri.Toa hoja nzito utasikilizwa.
Wale wanaojiita wanaharakati nao,hawana budi kujifunza kuongea bila ya kuwa na jaziba.Ni vizuri sana kupunguza hisia (emotions) katika midahalo kama hii na hasa itikadi iliyokidhiri(extremism) inayoweza pengine kusababisha kelele na mabishana na hatimaye kuzua ugomvi. Nenda youtube tafuta midahalo kati ya Obama na Hilary au Obama na McCain au Camerun and Goldon Brown,kama una nia ya kujifunza utapata mengi ya kujifunza kwenye midahalo kama hiyo.