Nesto E Monduli
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 247
- 155
Duh, unanifumbua zaidi..Aliyesema hayo ya DIT baadaye alihamia Arusha na ndiye aliyesema hayo ya chopa kwa njia ya ujanjaujanja. Huyu jamaa ni tatizo la Taifa, anapenda sana kucheza na akili za wanasiasa na anachukua taaluma kama jambo la kisiasa-siasa tu.
Mtu huyu hathamini taaluma lakini leo anaiambia Tanzania na Dunia kwamba atatumia taaluma kufanya mambo makubwa kama kutengeneza/kuunda chopa! Mtu huyu anatumia njia za mkato kutengeneza mitaala ya chuo lakini tafakari kwamba mtu huyo huyo anasema atatumia taaluma wakati hafuati matakwa/misingi ya kitaaluma!
Kwa upande mwingine, Serikali imekuwa ikitenga pesa kwa ajili ya wanataaluma wa chuo kwenda viwandani kukagua maendeleo ya wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuona na kubadilishana mawazo na wataalamu wa viwanda kwa muda wa siku 15. Lakini mtu huyu alivyo wa ajabu amekuwa akifikiri wanataaluma wakisafiri kwenda viwandani ni anasa.
Nia ya Serikali kupeleka wanataaluma viwandani kukagua wanafunzi pamoja na mambo mengine ni kuona viwanda vina nini kipya au vijana wetu wanapwaya au wako vizuri katika maeneo gani ili kuweza kuboresha zaidi taaluma inayotolewa na chuo.
Tofauti yake Mtu huyu huyu anayeongopea Taifa na Dunia kwamba atatengeneza chopa anafikiri kwamba wanataaluma watapata pesa au maarifa kama akiwapa per diem ya siku 15. Ndani yake mtu huyu hataki wanataaluma wa chuo wapate pesa wala maarifa na hivyo anawalipa wanataaluma wa chuo siku tano tu, hapo watajifunza kitu gani cha maana kwa muda huo? Je unadhani mtu wa aina hiyo anaweza kufanya watu kutengeneza chopa?
Kwa ufupi, hicho kinachosemwa kwamba kuna jambo la utengenezaji wa chopa chuoni hakipo. Ili kushuhudia kwamba jambo hili halipo, watu wafike na kufanya uchunguzi wa kina kama kuna jambo hilo. Hakuna kitu hicho, huo ni uongo kabisa.
Kumbe ni yuleyule !