Tanzania Future

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,925
9,389
Tanzania inatakiwa kufikiria kwa kina kuhusu tatizo la mafuta kwa future ya nchi yetu. Inabidi tuanze kufikiria kutumia train za kwenda mikoani za kisasa na kufungua plan za kubadilisha engine za magari ili ziweze kutumia gas.
 
Wazo lako ni zuri lakini kama viongozi wetu watagundua kuwa katika hilo hawana maslahi binafsi katika masuala hata kama yana umuhimu wa kitaifa kamwe usitegemee lolote.
Nchi hii itapata maendeleo mara tu tutakapopata viongozi walio katili kwa chama cha mafisadi Tanzania. Si hivyo hizi zitabaki ndoto tu.
 
Wakati wanatakiwa kufikiri future wao wanafikiri ni vipi wadanganye wananchi ili waendelee kukaa madarakani na kuiba pesa za EPA na account nyingine ambazo hadi sasa hatuzijui.

Mtu wa kufikiri future atakiwi kuwa na concentration ya mawazo ya short term kama walivyo wao, wanafikiri ni jinsi gani wajikusanyie pesa zaidi ya walizokuwa nazo na kuwakamua zaidi wananchi kwa kodi na bei za umeme za kulipia RDC na mengineyo.

Hawa viongozi wetu wanashindwa hata kufikiri jinsi ya kumaliza vitu vidogo ambavyo vinakera sana jamii kama daraja la kigamboni wataweza wapi kufikiri kuwa na Treni ambayo inatumia njia nyingine ya propulsion zaidi ya mafuta, watakachofikiri zaidi ni kuongeza bei kama njia ya kumaliza tatizo kwani hawaqna uchungu na wananchi wanao waongoza.
 
Tanzania kama nchi bado tuna kazi nzito ya kuhakikisha kuwa wananchi wanafaidika na jasho la kazi zao, mapato ya rasilimali za nchi n.k. Kabla ya hayo hayajawezekana, inabidi pawepo na "atmosphere" itakayoruhusu kuweko kwa kwanza sheria za kisasa zilizokitwa kwa kina katika kila fani ya maisha(kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k.), na pili vyombo vya utekelezaji wa sheria hizo kwa uhakika wa asilimia mia moja visivyojali hali, vyeo, umemba wa chama, kabila n.k....MFANO:Siku zote huwa ninashangaa ninaposikia kuwa mkuu wa polisi kapiga marufuku wenye magari ya pick-up. Sasa je, mkuu wa polisi ni mtungaji wa sheria? Ninavyojua mimi ni kuwa sheria hutayarishwa na bunge/serikali/hata umoja wa kijamii(wananchi) na kujadiliwa na kupitishwa na bunge kabla haijakuwa sheria. Polisi, mahakama wana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa na siyo vice versa!
Tatizo ni kwamba, hadi sasa hakuna dalili yoyote kuwa kitu kama hicho kinaweza kutokea, kwani waliopo madarakani wanajipa majukumu mengine ambayo personal interests zinawekwa mbele kuliko kitu au mtu yeyote!
Ugumu unaongezeka pale ambapo baraza la mawaziri na viongozi wengine wa ngazi za juu wanapewa uongozi huo kwa kuwa wana kadi za chama. Haiingii akilini kwa mtu yeyote aliyeona ndani ya "darasa la kutosha" kuona kuwa unaweza kumpa uwaziri mfano wa afya mtu ambaye fani yake ni umekanika wa mafriji! Au uwaziri wa uchumi mtu ambaye fani yake ni kulea chekechea! Usitegemee patakuwa na changamoto ya kimamwazo na maendeleo kutoka kwa watu wa naman hiyo hata kama utawatishia kuwa utawacharaza bakora wasipoleta maendeleo!
 
Back
Top Bottom