Tanzania: Four 'Imams' Cause Chaos in Mpanda Town

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
WANNE WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA VURUGU MSIKITINI YA KUTWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA KUONGOZA IBADA


Na Walter Mguluchuma | Mpanda

Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani mpanda mkoani Katavi kwa kufanya vurugu msikitini na kusababisha kuvunjika kwa ibada ya Ijumaa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashar amewataja watu hao kuwa ni Juma Mazomba (32) Ibrahimu Rashid (42) Mussa Hamis (27) Husein Omary (32) wote wakazi wa mtaa wa Kawajense.

Alisema watu hao walifanya vurugu hizo hapo juzi majira ya saa 7:15 mchana katika msikitii wa Kawajense Namba mbili.

Katika tukio hilo watu hao kila mmoja alikuwa akidai yeye ndiye mwenye uharali wa kuendesha (kuongoza) ibada ya Ijumaa katika msikiti huo, Kidavashari alisema mabishano hayo yaliendelea huku waumini wa dhehebu hilo wakiwa wakisubiria kuanza kwa ibada hiyo.

Kamanda Kidavashari alieleza kuwa baada ya kuona ibada imechelewa kuanza na viongozi hao wakiwa wanaendelea na mabishano waumini hao walitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea.

Ndipo ghafla viongozi hao walipoanza kurushana makonde hari ambayo iliwafanya baadhi ya waumini waliokuwa ndani ya msikiti huo wanaoishi jirani kutoka mbio na kwenda kuchukua silaha za jadi na kisha kurudi msikitini hapo.

Hata hivyo polisi walipata taarifa za tukio hilo na waliwasiri muda mfupi na kufanikiwa kutuliza ghassia hizo za pande hizo za viongozi wao wa msikiti.

Alisema kutokana na vurugu hizo zilifanya waumini kutofanya ibada ya Ijumaa katika msikiti huo.

Kidavashari alisema ugomvi huo umesababishwa na watu hao kuwa na uchu wa madaraka kwani kila upande unadai wao ni viongozi harari wa kusalisha katika msikiti huo.

Watu hao wote wanne bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kufanya vurugu ndani ya msikiti wakati wa ibada
 

diplomatics

JF-Expert Member
May 28, 2011
217
225
Si shangai sana hata huku kwetu walishawah kupigana wakigombania tende kutoka uarabun
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,168
2,000
Kule Katavi waumini wa kiisilamu ni wachache, so si ajabu kusikia jamaa wanagombea uimamu!
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,586
2,000
Haya mambo bado yapo kumbe!...kwa mtoto wa mkulima huko! Ngoja tusubiri BAKWATA watoe tamko!
 

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775
2,000
Mafunzo ya dini yanakataza uchomaji,kunajisi nyumba za ibada!hawa jamaa sijui hizi tabia wamezitoa wapi?wanaihaibisha sana dini yao,na kuifanya ionekane ni dini ya watu wenye jazba na elimu ndogo,wasiojua baya na jema!!
 

cacico

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
8,364
1,250
mapdere huwa wana zamu! wawekeane zamu, sasa wamewanyima wenzao ibada kwa ajili ya ubinafsi wao!
 

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,784
2,000
POLICE in Mpanda District, Katavi Region are holding four people who exchanged punches inside Kawajense Mosque, thus causing chaos after last Friday's prayers.

According to Katavi Regional Police Commander (RPC), Mr Dhahiri Kidavashari, the fracas started after the suspects started quarrelling among themselves over who was the right Imam to lead the prayers, a move that led them to physical confrontations.

The RPC named them as Juma Mazomba(32), Ibrahimu Rashid(42), Mussa Hamis (27) and Husein Omary (32), all residents from Kawajense Street in Mpanda town. According to RPC, the incident occurred at around 1:15 pm at Kawajense Namba Mbili mosque, when the four suspects entered the mosque and started claiming they had the right to lead the prayers.

It was further claimed that some faithful who attended the prayers went out and later returned armed with some traditional weapons including machetes and clubs.

"We were timely informed about the incident and the anti- riot-squad swiftly rushed to the scene and successfully contained the situation," explained the RPC. According to him, the four suspects are still in hands of police for interrogations and they would soon be arraigned once preliminary investigations are completed.

Source: allAfrica.com: Tanzania: Four 'Imams' Cause Chaos in Mpanda Town
 

juve2012

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
3,343
2,000
Kule Katavi waumini wa kiisilamu ni wachache, so si ajabu kusikia jamaa wanagombea uimamu!

imefika wakati viongozi wote wa dini wanaopatikana na hatia ya kugombania madaraka wapigwe chini wote na kuchaguliwe wengine kabisa kwa sababu kitendo cha kugombania madaraka ni kuonyesha kuwa watu hao wako kidunia zaidi kuliko kiimani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom