Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maamuma, Dec 12, 2011.

 1. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Dua ya kuiombea nchi yetu na kuliombea Bunge - husomwa hivi:

  (Msisitizo ni wangu)

  Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sana dua ya kuliombea Bunge inaposomwa na Spika au Naibu wake. Siku zote nimekuwa na mashaka kama kweli kinachoombwa ndicho hasa kinachohitajika na Wabunge wetu. Pamoja na upungufu uliomo kwenye dua hii nadhani hili la kuomba kuongezewa hekima na busara kwa wabunge haliombwi ipasavyo.

  Nijuavyo ni kwamba mtu huongezewa kitu ambacho anacho tayari ila anahitaji nyongeza. Sidhani kama baadhi ya wabunge wetu wana hekima na busara kiasi cha kuhitaji nyongeza. Matokeo yake aliye na hekima huongezewa (kama inavyoombwa) na asiye nayo hapewi (maana hakuna cha kuongeza). Kwa maana hiyo wale wabunge wachache ambao huongezewa hekima na busara huwa wanapishana kwa mbali sana na wale ambao hawana, na hii huleta mgongano na mabishano makubwa yasiyo na tija.

  Nimelazimika kusema haya kutokana na hoja ya hivi karibuni ya wabunge kutaka kuongezewa posho. Hivi kweli wabunge wetu, hayo ndio maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu?

  Waheshimiwa wabunge, ombeni mjaliwe hekima na busara kama vile anavyoombewa Rais wetu. Ili yule asiye navyo apewe angalau kidogo.

  Wakatabahu,

  Maamuma.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Serikali haina dini, bunge lina dini gani? Hiyo dua huwa wanamuomba mungu aitwaye nani?

  Kama tambueni kuwa mungu wamuombaye anaonekana kuwa ni mkuu wa itikadi ya taaluma ya maji marefu mbunge wa korogwe.
   
 3. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2013
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  "ee Mwenyezi Mungu tusaidie tufanye maamuzi kwa manufaa ya watu wote"

  Je maamuzi ya Bunge huwa kwa manufaa ya wote??
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2013
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  "Umjalie Rais wetu hekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri, wadumishe utawala bora"

  Hii dua ni ya KULIOMBEA BUNGE (read Bunge), Huyu RAIS na washauri wake wanaingiaje tena kwenye dua ambayo ni SPECIFIC kwa BUNGE na WABUNGE?!
   
 5. z

  zuberi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2013
  Joined: Jun 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkuu kuna mjumbe mmmoja Bukoba aliwahi mapema kupeleka maoni yake katika tume ya katiba na kusema WIMBO WA TAIFA UFUTWE KWA MAANA WIMBO HUU HUWA OMBEA VIONGOZI LAKINI CHA AJABU VIONGOZI HAO NDIO MAFISADI WAKUBWA TENA WALA HAWA WAHURUMII WAWAOMBEAO kwa mantiki hiyo basi naungana na wewe juu ya dua la kuliombea bunge
   
 6. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2013
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Siku hizi sala au Swala linachukuliwa ni sheria na wala sio imani na unyenyekevu kwa Mungu wetu, kitu muhimu kama bunge alafu muombeaji ni kiongozi wa bunge ambaye ni mtu wa kawaida (kuombea bunge), kwanini wasitoe ajira kwa viongozi wa dini? Nahisi ndo maana vurugu na matusi hayaaishi, nahisi serikali iliangalie hili
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2013
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Jana Msigwa ameingia bungeni na Biblia, mapepo yamepagawa hadi yakaanza kutaja taja neno 'nguruwe'
   
 8. k

  kinauche JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2013
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 7,682
  Likes Received: 838
  Trophy Points: 280
  Nasikia kuna profesa mmoja aliseama neno 'Mungu' liondolewe kwenye sala ya bunge kwa kuwa linawabagua wapagani. ├Ťnaweza kuona? Wakati wenzao Kenya rais anapiga magoti huku tunasema tusitaje Mungu. Mijitu mingine ├«melaaniwa kwa laana. Sasa hii nchi itaendeleaje kama tunamkataa Mungu?

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Apr 16, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280

  Duh mkuu naona una kahoja. Hii kitu inabidi iangaliwe upya lakini sasa kwa kuwa tuna imani nyingi hapa nchini itabidi waajiriwe viongozi wa Budha, Katoliki, Sabato, Islamu, Bahai, nk. Kwa jinsi hiyo huenda suala la sala/swala likachukua nusu saa nzima manake kuna wenzetu wakianza kuomba inabidi wekemee hasa wakiingiwa na roho na kuzanza kunena!
   
 10. m

  mob JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2013
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  MUNGU mwenye rehema tunakuomba utujalie amani na tuishi kwa amani na kila mtu bila ubaguzi
   
 11. kelao

  kelao JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2013
  Joined: Sep 24, 2012
  Messages: 4,836
  Likes Received: 1,229
  Trophy Points: 280
  Pale bungeni ni unafiki mtupu na ndo maana Mungu amewalaani sasa bunge linaonekana kituko!
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2013
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Sasa wabunge wanataka kuwe na vyuo vya kutongozea, na kuhalalisha Bangi mmmhhh mwisho watakuja kuthibitisha ndoa za jinsia Moja
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Waajiri wa dini gani?
  Na watatumia muda gani wote kuomba?
  Na wapagani je? Wakatambike?
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2013
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kwa tanzania hii ambayo leo hii udini umeota mizizi sijui kama sala hizo zitafanya kazi!! Hiki ndicho kitakachotokea:
  • Wakati Sheikh anasoma dua, wabunge Wakristo watakuwa wanakemea kimya kimya Sheikh ashindwe kwa jina la YESU!
  • Wakati Mchungaji anasoma dua, Waislamu watakuwa wanasema kimya kimya "astaghfurall! astaghfurall!!"
  Sasa unazani dua hizo zitapokelewa kweli?
  Waacheni hivyo hivyo, wachanane kavu kavu na ikibidi ifike siku hat watiane mikono hadi waheshimiane!
   
 15. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2013
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  :Wasomi wa kiislamu wanasema ni sala ya kikristo....!
   
 16. john tongo

  john tongo JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2013
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  chunga sana kitu kinachoitwa kiapo,wabunge wetu wakiapishwa wanashika biblia au quran kama comitment,lakini wanayoyafanya ni kinyume kabisa,unategemea nini hapo kama si "kudata"
   
 17. i

  iseesa JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  HOJA: SPIKA wa BUNGE lijalo ni lazima awe MUISLAMU kama hoja iliyopita ya kuwa MWANAMKE
   
 18. kamtu33

  kamtu33 JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2013
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 971
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 60
  Tatizo siyo DUA, tatizo liko kwa hao wanaoombewa hiyo DUA maana hata kwenye viapo vyao wanaapa vizuri ila wakisha apa wanasahau kama walisha apa
   
 19. K

  Kikwajuni One JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2013
  Joined: Mar 18, 2013
  Messages: 8,168
  Likes Received: 1,545
  Trophy Points: 280
  Hawa wapagani hawajajiandikisha serekalini,wangejisajili,wakajulikana,ingekwa wepesi kujulikana ni kina nani na wako wapi na wanafanya nini
   
 20. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  "Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu na Dunia, Umeweka katika Dunia Serikali za Wanadamu na Mabunge ya Mataifa ili haki yako itendeke.

  Twakuomba, uibariki nchi yetu idumishe uhuru, umoja, haki na amani, Umjalie Rais wetu hekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri, wadumishe utawala bora.

  Utuongezee hekima na busara, sisi Wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wa kujadili kwa dhati, mambo yatakayoletwa mbele yetu leo, ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu. Amina."

  Kwa tabia wanazofanya Wabunge wetu Dua hizi hupokelewa na Mungu kweli??!!!
   
Loading...