Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

Mie sioni umuhimu wowote wa kuwepo na Bunge nchini zaidi ya kuongeza gharama kubwa kwa walipa kodi.
 
Serikali haina dini sasa dua ya nini tena?!

Hiyo ni sawa na kuchukua(kuteka) maji kwenye kisoda kisha kwenda kumwagia baharini kisha unasema na mimi nimechangia mchango wangu wa maji baharini
 
Hebu niambie huo ulazima wa kuwa na Bunge kama hili. Miaka nenda miaka rudi madudu chungu nzima. Kama wawakilishi wa Watanzania hakuna lolote la maana wanalolifanya zaidi ya kuomba waongezewe mishahara na marupurupu kwa kudai gharama za maisha zimeongezeka wakati ongezeko la gharama za maisha haliwaathiri Wabunge tu.

Madudu ya ufisadi wa kutisha EPA, Richmond/Dowans, IPTL, Kiwira Coal Mining, mabilioni ya Uswiss, Mikataba feki ya rasilimali, kuanguka kwa elimu, kushuka kwa kiwango cha kutisha katika upatikanaji wa huduma muhimu kama matibabu, umeme, maji, usafiri n.k.

Wengi wao wanadhani wako Bungeni kuitetea Serikali matokeo yake Serikali inafanya itakavyo. Imefikia mpaka wizara kupewa 25% ya bajeti kwa mwaka mzima na Wabunge hawatii neno. Nazungumzia Wabunge wa MACCM. Niambie tangu 1995 hadi leo hii Bunge limefanya mambo gani ambayo yanastahili kupongezwa. Na matatizo yote ya Bunge hili yanachangiwa na Wabunge wa MACCM.




lazima tuwe na wawakilishi mkuu,.
 
Serikali haina dini sasa dua ya nini tena?!

Hiyo ni sawa na kuchukua(kuteka) maji kwenye kisoda kisha kwenda kumwagia baharini kisha unasema na mimi nimechangia mchango wangu wa maji baharini

haina haja ya kuwa na Dua mkuu!!
 
mbona jambazi au mwizi kabla ya kuenda iba au kufanya tukio kwanza anaomba dua unalitambuaaa hilo
 
mbona jambazi au mwizi kabla ya kuenda iba au kufanya tukio kwanza anaomba dua unalitambuaaa hilo
Hao wawili uliowataja wana imani(dini) zao.

Tofauti na serikali iliyoweka mambo wazi ya kuwa serikali haina dini
 
watu wanaapa na vitabu vya dini mahakamani na bado wanasema uongo itakuwa hao wanasiasa
 
Hakuna cha maombi wala dua hapo bunge limekuwa mojawapo ya kazi za shetani!!ni ushetwaani mtupu ni majizi yenye mwavuli wa dini zao.
 
Nimeiona hii kwenye gazeti la Mwanachi la leo linalohusu 'Dua ya kuombea Bunge inayosomwa kama kasuku.

Dua hii inasema kama hivi:

Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu,Muumba wa Mbingu na Dunia,umeweka katika dunia Serikali za Wanadamu na Mabunge ya Mataifa ili haki ya itendeke.Twakuomba uibariki nchi yetu idumishe uhuru,umoja.haki na amani,umjalie rais wetu hekima,afya njema,na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri,wadumishe utawala bora.Utuongezee hekima na busara sisi wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wa jujadili kwa dhati mambo yatakayoletwa mbele yetu leo,ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na utsawi wa nchi yetu.Amina"

Kwenye sala/dua hii ni nzuri siwezi kukataa wala kupinga,lakini nina maswali kadhaa kuhusu hili:

1.Je Bunge letu linaitendea haki sala au dua hii.
2.Kwanini dua hii isisomwe na wabunge wote ili kila mmoja aweze kuifanyia tafakuri ya kina pale anapoomba au kusali dua/sala hii asubuhi wafunguapo Bunge.
3.Na kwanini sala/dua hii husomwa kwa haraka sana kama vile kuna muda unapotea,yaani kwanini dua hii sifanywe kwa tafakuri ya kina pale inaposaliwa?

Inawezekana hoja hii ilishawahi kuletwa hapa na sikuiona basi naomba mnisamehe,ila ningependa tuitafakari dua hii na kuiomba serikali yetu au Bunge letu liichulie DUA hii kwa moyo na kila mtu ndani ya Bunge awe anaisoma na kuitafakari,ninadhani itabadilisha dhana nzima ya uchangiaji usiona tija,uchangiaji wa mipasho na matusi kwa wabunge wa pande zote mbili.

Karibuni nyote tuijadili.
 
Kuna uhusiano wowote wa dua katika kuombea bunge la katiba na yale matendo ambayo yanafanywa na wajumbe wa katiba hasa ukizingatia manung'uniko mengi yamekuwa yakitolewa na wananch juu ya uwezekano wa baadh ya wajumbe kuchakachua katiba ambayo kiukweli ni maoni ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa tz.

Je kunaweza kukawa na athari kubwa kwa maana kwamba ni kumdhihaki mwenyezi Mungu?

=======

Kwa mwenye IMANI kwa Mungu kwa dini zote mbili anaweza kuungana nami nakusema kuna mahusiano kabisa.Unaposali kwa dhati au ukaomba dua kwa dhati,na ukawa na nia njema ya Taifa lako waweza kujitafakari na kuona unakosea nakujirudi.

Lakini sababu wanasiasa wetu wamekosa uwoga kwa Mungu na mungu wao kuwa pesa na madaraka zaidi hawaoni uwoga tena na kuona dua au sala hii inawapotezea muda.Na nitaungana nawe kbisa kuona Mungu wetu aliyetuumba sasa anadhihakiwa na hawa waliopewa na madaraka ya kutuongoza na sikututawala.
 
dua ni nzuri ila anaeisoma dua hiyo si mtu mwema

Je unafikiri hivyo?Siyo namna inavyoombwa as if wanapoteza muda?Maana Mungu anampa MVUA hata mwenye dhambi,habagui.Ni namna tu mtu anavyojinyenyekeza kwa aliyemuumba.
 
Back
Top Bottom