NakuliliaTanzania
JF-Expert Member
- Sep 24, 2007
- 555
- 9
Sina hakika kama na wenzangyu mmeliona hili lakini kwa siku za karibuni hili gazeti linaloaminika kwa taarifa moto moto na linalojulikana kwa kupigana dhidi ya ufisadi limekuwa likichelewa kutoka mtandaoni...sijajua kiini hasa ni nini..kama ni matatizo ya IT au ni uamuzi wa makusudi
Yote kwa yote, wanapaswa waelewa kuwa wana wasomaji wengi sana online na kuchelewa kutoka mtandaoni, wataanza kutupoteza taratibu
Taarifa unazisoma almost jioni..zishakuwa kiporo tayari..na wakati huo huo magazeti mengine yanakuwa yameshaandika na yapo mtandaoni
Hivi wanaweza kutuambia ni nini hasa tatizo au hakuna tatizo?
Kila nikisema hapa kwamba Watanzania tuna matatizo wote kwa ujumla wetu... kuna watu wanasema ni CCM tu... sasa sijui hapo Tanzania Daima napo CCM ndio wanaoendesha hilo gazeti
Kila nikisema hapa kwamba Watanzania tuna matatizo wote kwa ujumla wetu... kuna watu wanasema ni CCM tu... sasa sijui hapo Tanzania Daima napo CCM ndio wanaoendesha hilo gazeti
Wakikwambia wana matatizo ya staffing utasemaje?
Maoni yangu ni kuwa service usiyoilipia na ambayo hujui inakuwa funded vipi huna haki ya kuilalamikia quality yake.Ingekuwa ni subscription service ungeweza kulalamikia punctuality.Au kama wangekuwa wanakosea katika content hapo hata bila ya kuwa subscriber ungeweza kukosoa upotoshaji.
Wakikwambia wana matatizo ya staffing utasemaje?
Maoni yangu ni kuwa service usiyoilipia na ambayo hujui inakuwa funded vipi huna haki ya kuilalamikia quality yake.Ingekuwa ni subscription service ungeweza kulalamikia punctuality.Au kama wangekuwa wanakosea katika content hapo hata bila ya kuwa subscriber ungeweza kukosoa upotoshaji.
Lakini sasa hivi wanaweza kukwambia wanachelewesha makusudi ili watu wanunue print edition kwanza nakala za kutosha halafu wataweka online, which is a fair business strategy considering they have expenses and are nopt a charity.
Badala ya kuwapigia kelele kwamba wanachelewa inatakiwa tuwashukuru kwamba angalau wapo online, magazeti mangapi ya bongo (never mind the quality) hayapo/ yapo online?
Duh..Mkuu Kasheshe..ndo maana nimeileta hapa kwa sababu hapa tunamkoma nyani giledi,, haijalishi mi siliangalii kichama zaidi naliangalia kama sehemu ya uwajibikaji...wakati wenzetu wanaupdate stories kila dakika/saa, wenzetu ndo kwanza wanatuletea viporo....ingetakiwa walau habari za kesho yake by midnight zimeshapostiwa....
Ninayo principle moja;
Ukitaka kuchezea timu ya soka ya taifa lazima utuwakilishe vyema; ukitaka kuwa miss lazima utuwakilishi vyema, ukitaka kuwa mkulima lazima uzalishe kwa kiwango cha hali ya juu, ukiwa umejiingiza kwenye habari lazima ufanye hivyo kwa makini.
Nimesikitishwa sana na wanaJF kutetea uzembe huu... kwa hakika mulaaniwe ninyi munayetetea uzembe...kisa tu ati gazeti lenu
Ninayo principle moja;
Ukitaka kuchezea timu ya soka ya taifa lazima utuwakilishe vyema; ukitaka kuwa miss Tanzania lazima utuwakilishi vyema, ukitaka kuwa mkulima lazima uzalishe kwa kiwango cha hali ya juu, ukiwa umejiingiza kwenye habari lazima ufanye hivyo kwa makini. Kama huwezi tafuta shughuli nyingine yoyote unayoiweza vizuri.
Nimesikitishwa sana na wanaJF kutetea uzembe huu... kwa hakika mulaaniwe ninyi munayetetea uzembe...kisa tu ati gazeti lenu!!!!
Siyo kutetea,
Naona baadhi yetu Wabongo tunazoea sana vitu vya dezo kiasi cha kuwa na utamaduni wa kwenda beyond kuzoea services hizi, sasa tunaanza kudemand.
Hiyo principle yako, unajuaje kama hao wanataka kukuwakilisha kama unavyofikiri? Una hakika gani kwamba hawafanyi effort zote lakini labda wanashindwa kiuchumi? Mbona hujalijibu swali langu la msingi, kwamba wewe, mtu mwenye commitment kubwa sana na excellence, unalisupport vipi hili gazeti kuhakikisha kuwa liko online on time?
Yaani watu tunakosa empathy, tunakosa kuwa considerate, tunakosa kuangalia environment, tunaishi katika utopia tu, kila siku kulaumu kulaumu bila hata kujaribu kuangalia chanzo, bila hata ku volunteer possible solutions.
Kwa taarifa tu mimi sina uhusiano wowote na magazeti Tanzania.
Kwa bahati mbaya unaonge na a mtu anayeyafahamu haya mambo ndani nje... mfano wa kuwa makini at least na kujali wateja huu hapa
Na wewe unajihesabu mteja? Unajua maana ya mteja?
Pundit.. tatizo la sisi tunaokaa nje au ambao tumekuwa exposed na affluence ya magharibi we have started to create this "instant mentality" where by one pushes a button na kitu hicho! unabonyeza namba mbili tatu, hela inachomoka, unaingiza hela hapa pale kopo la soda linatoka.
Hivyo tumefikia mahali hata kwenye kubadilisha oil ya gari huhitaji hata kutoka unaenda drive through wanakubadilisha oil na filter wewe unapiga soga unalipa unachomoka zako.
Sasa maisha haya ya nchi zilizoendelea ambazo ziko kwenye tier one zinatufanya na sisi kwa namna fulani tuamini kuwa Tanzania iko kwenye kundi hilo kwa sababu sisi Watanzania tunaoishi nchi za magharibi tunaenjoy maisha hayo.
Sasa leo ukitaka habari unaingia drudge report unaipata kabla haijafika CNN au FoxNews; ukitaka kujua maendeleo ya habari yoyote una "click" hapa na pale na habari inatokea and sometimes you can follow the news live as it is happening. Tunadhani Tanzania nako iko hivyo.
Tumesahau kuwa sisi tuko kwenye bottomo of the bottom tier! Sasa anapokuja mtu na gazeti au chombo chake habari na kuanza kuleta habari kwa haraka basi tunatarajia iwe kama au inakaribiana na "instant lifestyle" tuliyoizoea ambayo neno subira halipo. I wan't it, and I want it now!
Hivyo basi tunajikuta tunajiandaa kwa frustrations and disappointment. Kama ulivyosema, hivi haya magazeti yanapopokea matangazo ya intaneti ni kweli yanalipa kiasi cha kufanya wategemee matangazo hayo na si mauzo? NI makampuni mangapi ambayo yanatangaza kwenye intaneti Tanzania na ambayo yanaingiza biashara? Kutangaza kwenye intaneti kunapresume kuwa watu wengi (your target market) wana access ya hiyo intaneti. Vipi kama unatangaza lakini hilo tangazo halirudishi wateja?
NI kwa sababu hiyo basi magazeti kama Tanzania Daima na Raia Mwema na MwanaHalisi ambayo yanategemea zaidi mauzo kuliko matangazo ya biashara yanajikuta yanabadili mkakati wa kupata fedha na siyo suala la uzembe.
Hakuna kitu cha dezo na mambo ya ujamaa yalipita zamani. Tunaishi katika nchi ya kibepari na katika mfumo huu wa kibepari kinachopendwa na maximization of profit and individual success. Kama kuwahisha gazeti online kunapunguza mauzo ya magazeti mitaani what do you do? The answer is very clear.
Ndipo hapo tunaingia sisi wengine ambao tunajaribu kutengeneza mtandao wa habari kuweza kuleta habari za leo leo hii, na habari za sasa sasa. Guess what?
Do we get support? no.. watu wanataka dezo. Tunajaribu kuweka mtandao wa kutuletea habari kwa kadiri zinavyotokea lakini hao waleta habari wafanye kwa dezo kama kutoa sadaka kanisani? Linapotokea tukio mahali waende kwa nauli ya nani na watakapopata mahali pa kutumia intaneti cafe walipie kwa fedha zipi?
Hii ni changamoto kubwa kweli ya habari Tanzania na ndio maana kati ya vitu ambavyo kwa upande wangu ninajaribu kufanya ni kuunganisha nguvu za wale walioko nyumbani na sisi ambao tunaishi kwenye instant culture. Bado ni vigumu sana, so friends, cut them some slack otherwise.... anzisheni na nyie vyombo vyenu vitakavyoweza kufanya kazi kwa kujitolea kuleta habari 24 hours, no delay, no complains and see how easy it is.
M. M.
halafu msisahau na masuala kama vile ukataji umeme nkkwi kwi kwi,
Mkulu Kasheshe kumbe hujui kuwa webmaster wa Tanzania Daima ni ccm damu damu. No wonder makala motomoto huwa hazitokei haraka kwenye website......lol
Pundit;
kwi kwi kwi.
Kama mambo kama haya unayafahamu!!! then for sure sio mimi tu bali hata mtoto tutakaye pata wiki ijayo atakuwa ni potential customer wa Tanzania Daima. (hope these send 2u a strong msg about customer care)
Hivi Tanzania Daima wana sehemu ya ku-subscribe na sisi tukaacha kujiunga nao?