Tanzania Bara ina Mawakili 1,188 Tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Bara ina Mawakili 1,188 Tu!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, May 14, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wapendwa WanaJF,
  Tanzania Bara ina Mawakili wa kujitegemea 1,188 tu kwa takwimu za hadi Desemba 15, 2009 (Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi). Kwa kuwa Mawakili wengi sana wanapenda kuishi Dar es Salaam (angalia uk 120 na 121 wa The Legal Profession in Tanzania: The Law and Practice by Dr Fauz Twaib, Published by LawAfrica Publishing (T) Ltd, 2008) kuliko mikoa mingine, si rahisi wa watu wengi, especially wenye vipato duni na wanaoishi vijijini kupata huduma za kisheria kwa kuwa idadi ya mawakili hawaishi nao na ni wachache.
  Kwa kuwa CCM Katika Ilani yake ya Uchaguzi, 2005 Ibara ya 108 (i) na (j) inasema kwamba CCM ingeanzisha mfumo wa kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo kupata msaada wa kisheria na vilevile ingeanzisha mfumo utakaotumia wanasheria wa awali (para-legals) katika Mahakama za Mwanzo, mifumo hiyo ianzishwe mapema ili haki wa raia wa nchi hii zilindwe! CCM ikija kuomba kura tena mwishoni mwa mwaka huu 2010 tuwaulize juu ya utekelezaji wa ahadi hii, japokuwa ahadi kibao hazijatekelezwa!
  Tujadili zaidi!
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nipo katika mchakato wa kuwa mwansheria na badaye wakili ili kuziba mapengoo hayoo. Ni career ambayoo bado ina fursa nyingii zaidii.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Jitahidi ndugu, maana kuingia kwenye Roll of Advocates nako ni issue, ndio maana wako wachache!
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,746
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280


  mwezi june wataongezeka.kwani wanafunzi wa zao la kwanza la shule ya sheria(law school) wataapishwa.
   
 5. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Tena katika hao 1188 toa wale ambao wameshatangulia mbele ya haki na wengine ambao they are no longer active in practice utabakiwa labda na mawakili 700 tu ambayo ndio "idadi kamili"
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mi nilidhani wapo wengi ndo maana inatuchukua miaka kuitwa kwenye bar exam!!!!
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Moja kati ya ahadi nyingi walizoahidi na hazipo, wakija tena tuwaambieje?????? Kama mtu ulipata ridhaa ya watu kwa kuahidi kitu halafu hutendi hicho kitu iluchoahidi sisi tiliokupa ridhaa tuna haki gani juu ya ahadi zako????
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  May 22, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Lawful means ni kutowapa kura tena wakija kuomba au kuwakumbushia tena ahadi zao maana inawezekana wana maelezo. Pia kufanya maandamano halali ili kushinikiza. Unlawful means ni kupindua serikali, kumpiga Rais mawe anapokuja ziarani, kuzomea, nk! All in all, haki huwa haziombwi, zinapiganiwa!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  May 22, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Good News!
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kenya ina mawakili zaidi ya 6000 na Uganda ina mawakili zaidi ya 3000
  Hii jumuia ya EA tutaweza kweli kushindana na hao jamaa?
  Cha kusikitisha zaidi Mawakili wengi toka Kenya na Uganda wamekuja kusoma TZ hapo Mlimani.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  May 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180

  Tutafika tu ndugu, hii EAC itatufungua macho!
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Actually tunachekesha sana. Halafu chimbuko la sheria East Africa ni Unidar ajabu sisi ndio tunasuasua. kutokana la saturation ya mawakili kwa majirani ndo maana nchi zingine issue yao kubwa ni cross border practice.

  Take that with the fact that Kenya ni nucleus ya multinationals katika Est and Central Africa mawakili wa tanzania wataambulia kushika kesi za matusi na kesi za talaka.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo la legal profession ni ubinafsi umetawala! Walioko juu wanaona wakifungua milango soko litavamiwa na status ya uwakili itashuka! Hivi tuseme kwa upande wa Kenya na Uganda kwa kuwa mawakili ni wengi kwa hiyo hawana status? It is so sad, Kitivo cha Sheria cha UDSM ni cha kwanza kwa Afrika Mashariki kuanzishwa, lakini sasa hivi tuko wa mwisho kuwa na mawakili! In fact, it is ridiculous!
   
Loading...