The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,458
- 17,255
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.
Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.
Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.
Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.
Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.
Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.
Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.
Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.
Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.