both
wapo wanaowajibika na wapo wasiowajibika
Well,
Hadi wakati huu, bado tunahangaika na utata wa upatikanaji wa hao viongozi, achilia mbali kuhusu uwajibikaji.
Mambo ya tume ya uchaguzi, katiba, haki za binadam, utawala bora, ufisadi, uchawa....orodha ni ndefu.
Lakini eneo moja ambalo tunafanya vizuri, ufisadi, hapo tuko mbele.
Imagine mkuu wa nchi anaongelea uchafu wa jiji, tena kongwe lenye watu wanaojiita viongozi kwenye kila nafasi iliyopo.
Hapo hatujagusa ubovu wa huduma za kijamii kwenye maeneo mengine.
Bado mkuu anasema huo uozo wa wasaidizi wake anaowaita wanajeshi wake, dawa ni kuwahamisha vituo ili kuwaokoa.
Kumbuka hatuna rasirimali za kujaribu na zisizoisha, na muda haupo, tukiendelea na huu mchezo wa kutokua na uelekeo sahihi, hatutafika popote.
Back to your question,
Viongozi kwa maana ya kujaza nafasi kwa muktadha wa muundo wetu wapo. Na wanapatiwa stahiki zao kadri ya taratibu zilizopo.
Kwenye huu uzi unaona taa zinatengenezwa, zinajaribiwa, barabara inaanza kutumika, bado hizo kasoro zipo na hao viongozi wamejaza nafasi na kupokea stahiki zao.
Hapo ndio msingi wa kauli yangu kwamba, bora waje wenye weledi wa mambo ya uongozi na usimamizi wa mambo. Sie tuendelee kufuga, kulima na kuchunga.