Tani 13,100 za korosho zauzwa

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1572791421564.png


TANI 13,100 za korosho zimeuzwa katika mnada wa kwanza wa zao hilo na bei ya juu ikiwa ni Sh 2,525 na bei ya chini ni Sh 2,468. Zimeuzwa katika Chama Kikuu cha Ushirika cha Newala & Tandahimba (TANECU) kwenye uzinduzi wa msimu huu wa mwaka 2019/2020.

Katika mnada uliofanyika wilayani Newala, kampuni 34 zilijitokeza kufanya zabuni ya kununua korosho na kati ya hizo kampuni sita zimeshinda. Meneja wa TANECU, Mohamed Nassoro alisema mahitaji ya wanunuzi kwenye mnada huo, yalikuwa ni kupata tani 40,000 za korosho, wakati zilizopatikana kwenye maghala ya chama hicho kwa kuanzia ni tani 13,000.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa aliwatoa hofu wanunuzi wa zao hilo, wakati shughuli hizo za ununuzi zikiendelea, kutokana na yale yaliyotokea msimu uliopita 2018/2019.

Baadhi ya wakulima hao, Hamidu Issa na Abdul Karim, walisema “sisi tumekubali kuuza korosho kwa bei hii, ila tunaiomba serikali itusaidie suala la malipo kusiwe tena na ucheleweshwaji wa malipo ili hizi fedha zitusaidie kufanyia mambo mengine.” Waliongeza kuwa, “ mnada unapofanyika zisipite siku nyingi kufanya malipo na isije ikatokea kama msimu uliopita kwa sababu kuna wakulima wengine hadi sasa hivi hawajapata malipo yao na huu ni msimu mwingine umeanza.” Kwa msimu wa mwaka 2018/2019, mnada wa kwanza wa chama kikuu hicho bei ya juu ilikuwa Sh 2,717 na wakulima waligoma kuuza korosho, ndipo serikali ikafanya uamuzi wa kununua zao hilo.
 
Wanakusini wenzangu, mbona mwaka Jana mligomea being zaidi ya 2650, iweje Leo mnakubali mpaka 2465
 
Wakulima wamekoma kugoma, safi sana dawa imewaingia vizuri, wache markert yenyewe icontrol price
Usiwe chizi wewe aliyekuambia wakulima wamewahi kugoma nani? Uliza tukuambie
si wanagoma wanunuzi wa kangomba walionunua 2500 we unasema wakulima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom