Tani 128 za dengu zakamatwa zikitoroshwa - Mnayara

Tani 128 za dengu zakamatwa zikitoroshwa - Mnayara

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mamlaka ya Uthibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko Nchini (COPRA), kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, imekamata tani 128 za dengu zilizokuwa zikitoroshwa mpakani mwa Singida na Manyara.

Mazao hayo yalibainika kukosa kibali cha usafirishaji kutoka mamlaka husika na hayakupitia kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani kama inavyotakiwa kisheria.



Akizungumza baada ya kukamatwa kwa shehena hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, alisisitiza kwamba wafanyabiashara wanapaswa kuuza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani badala ya kuyauza kwa walanguzi.

Hatua hiyo inalenga kulinda bei ya mazao, kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali, na kuhakikisha wakulima wananufaika ipasavyo.

Kwa upande wake, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Chiliga, alihimiza wafanyabiashara kuzingatia mifumo rasmi iliyowekwa na serikali, hususan mfumo wa stakabadhi ghalani, kama njia salama na yenye tija kwa uuzaji wa mazao.

Chanzo: Global online tv
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom