Mimi kwenye mziki wako nakuwa nafanyaje? Au ndio mnenguaji😆Asee pole sana nakukaribisha kwenye MZIKI wangu japo sitaki watu wengi ili kuepusha migogoro mbeleni, si unajua mambo ya pesa zikichanganya na Shari kila siku
Hapana nimedhamiria kufanya mziki kuwa kazi yangu ya kwanza lakini lazima nipate watu mashuhuri mfano, koneksheni ya show, mtu anajua chap linapo tokea jambo la KIJAMII mfano mwenge, mikutano ya umma anaangalia nitapataje showz, si hivyo tu matukio ya show za clubs nk au kianda show wenyewe ikiwa tutapata hit songMimi kwenye mziki wako nakuwa nafanyaje? Au ndio mnenguaji😆
Ooh saw akila la kheri! Mdogo mdogo tu utafika!Hapana nimedhamiria kufanya mziki kuwa kazi yangu ya kwanza lakini lazima nipate watu mashuhuri mfano, koneksheni ya show, mtu anajua chap linapo tokea jambo la KIJAMII mfano mwenge, mikutano ya umma anaangalia nitapataje showz, si hivyo tu matukio ya show za clubs nk au kianda show wenyewe ikiwa tutapata hit song
Sawa mkuu, ni MUNGU tu ndio naemtegemea mana tayari Nina label yangu inani simamia mwenyewe nahitAji konekshen tu, na mtu mnyumbulifu ili tutengeneze billions of money japo si kazi nyepesOoh saw akila la kheri! Mdogo mdogo tu utafika!
Koneksheni zitakukuta mbele ya safari anza kujibrand mwenyewe, uzuri siku hizi mmerahisishiwa gen z unatumia tiktok live unafanya mambo watu watakuja wenyewe!Sawa mkuu, ni MUNGU tu ndio naemtegemea mana tayari Nina label yangu inani simamia mwenyewe nahitAji konekshen tu, na mtu mnyumbulifu ili tutengeneze billions of money japo si kazi nyepes
Shukran sana, nawe pia MUNGU akurahisishie kwenye biashara yakoKoneksheni zitakukuta mbele ya safari anza kujibrand mwenyewe, uzuri siku hizi mmerahisishiwa gen z unatumia tiktok live unafanya mambo watu watakuja wenyewe!
Ahsante sana mkuu. Umesema kweli—labda muda huu si wa kupambana zaidi, bali kubadili mbinu. Nimeupokea ushauri wako, nitaendelea kusonga mbele. Mungu akipenda, mavuno yatakuja. 🤝🏽Pole sana kwa safari ndefu na mapambano ya miaka mingi tangu 2012. Ni jambo la kawaida kabisa kuchoka na kujisikia vibaya wakati matokeo hayajalingana na nguvu unazoweka, lakini kumbuka kuwa kuendelea kupambana kwa miaka 14 ni ushahidi tosha wa ustahimilivu na ushujaa mkubwa ulio nao ndani yako.
Kama mambo bado hayajakaa sawa, hii haimaanishi kwamba wewe ni mshindwa, bali huenda ni wakati wa kubadili mbinu.
Tafuta Mtandao Mpya (Networking).
Wakati mwingine mlango wa mafanikio haufunguliwi na kile unachokijua, bali na nani unayemjua. Badili mazingira, zungumza na watu waliofanikiwa kwenye eneo unalolipambania, na uombe ushauri au ushirikiano (mentorship).
Tunza Afya ya Akili na Nafsi.
Mapambano ya muda mrefu yanaumiza kisaikolojia. Usijihukumu wala kujilinganisha na wengine waliochelewa kuanza lakini wapo mbali. Kila mtu ana majira yake ya kuvuna, mradi tu halali shambani.
Kwa kweli sina maneno ya kutosha ya kueleza jinsi ujumbe wako ulivyonigusa. Nimeusoma mara kadhaa, na kila nilipousoma nilijikuta nikitokwa na machozi. Leo nimekuwa nikilia siku nzima, si kwa sababu ya kukata tamaa tu, bali kwa sababu maneno yako yamenikumbusha kwamba bado kuna watu wanaoelewa na kuthamini mapambano ambayo mtu hupitia kimya kimya.Pole sana kwa safari ndefu na mapambano ya miaka mingi tangu 2012. Ni jambo la kawaida kabisa kuchoka na kujisikia vibaya wakati matokeo hayajalingana na nguvu unazoweka, lakini kumbuka kuwa kuendelea kupambana kwa miaka 14 ni ushahidi tosha wa ustahimilivu na ushujaa mkubwa ulio nao ndani yako.
Kama mambo bado hayajakaa sawa, hii haimaanishi kwamba wewe ni mshindwa, bali huenda ni wakati wa kubadili mbinu.
Tafuta Mtandao Mpya (Networking).
Wakati mwingine mlango wa mafanikio haufunguliwi na kile unachokijua, bali na nani unayemjua. Badili mazingira, zungumza na watu waliofanikiwa kwenye eneo unalolipambania, na uombe ushauri au ushirikiano (mentorship).
Tunza Afya ya Akili na Nafsi.
Mapambano ya muda mrefu yanaumiza kisaikolojia. Usijihukumu wala kujilinganisha na wengine waliochelewa kuanza lakini wapo mbali. Kila mtu ana majira yake ya kuvuna, mradi tu halali shambani.
Umesema kweli kabisa. Yaliyopita ni somo, si sehemu ya kuishi. Cha msingi ni kuitumia leo vizuri, hata kwa hatua ndogo. Maisha hubadilika pale tunapoacha kujilaumu na kuanza kufanya kazi na kile tulicho nacho sasa. Hapo ndipo mwanzo wa mabadiliko ulipo.Kwanza usifikirie ulipo kosea wala usi fikirie nyakati za nyuma hizo zilisha pita haziwezi rudi zaidi zita kuumiza tu na kwa nini uumie kwa sababu ya wakati ulio pita ? Jibu ni uta poteza mda zaidi .
Anza kufikiria na kufanyia kazi wakati uliopo ishi maisha yako kwenda mbele na sio kurudi nyuma leo usiku kabla ujalala fikiria kwa eneo uliopo jambo gani uki focus nalo unaweza toka .
Note
Usi imagine vitu visivyo kuepo wala usi waze kwa kuangalia watu wata kuonaje au wana kuonaje
Realize deeply that the present moment is all you have .Make the now the primary focus of your life .
TARUDI KESHO KUMALIZIAView attachment 3671975
Mkuu, niko bush sana na kwa kweli napitia changamoto kubwa sana kwa sasa. Ndio maana hiyo 50K kwangu ni mtaji wa kuanzia, si kwamba nimepanga kubaki na kuku wachache. Nikifanikiwa kuanza na kujenga msingi, lengo langu ni kujitoa nilipo na kwenda maeneo kama Geita/Katoro kutafuta fursa na kujipambanua zaidi.Nenda sehemu zenye migodi midogo midogo kama pande za katoro, lwamugasa, nyarugusu, mgusu, huko mkoani geita au kakola, nyakagwe mkoani shinyanga.
Huko kote mimi nimepita, nimepiga kazi za kutwa kwa elfu8 hadi kumi ila siku hizi migodi mingi ukiingia asubuhi saa moja unatoka kesho yake asubuhi saa moja unalipwa kati ya 20k hadi 30k.
Kazi kubwa ni kupakia mawe saizi ya kawaida saana na sio mchaka mchaka kivile kupumzika a.k.a KULA TANO kupo sana tu.
Misosi ipo mala mbili hadi tatu kutegemeana na mda wako wa kazi.
Kama huwezi kuingia duarani bado kuna kazi za juu kifupi kazi ni nyingi hadi kwenye plants za kuozesha marudio. Yaani madogo huku, kina mama kina baba wapo plants wanapiga kaz hawakosi 450k had 600k kwa mwezi.
Bei ya dhahabu inapanda na migodi inaongezeka so ajira pia zinaongezeka.
Hiyo 50k ya kufuga kuku!!!!???? Kuku mmoja jogoo ni 50k au we uko kijijini sana? Halafu kuanza na kuku wawili utatoka lini br??
Hatare sana mzee.... Vijana siku hz utasikia nikipata mtu akanipa pesa,, nadhani ukipewa kazi ni rahisi kuliko pesa.... Kazi itakupa uzoefu... Utakutana na watu..... Utakutana na mawazo tofauti tofauti na hapo utajikuta una kua kiakili zaidi na kukufanya uzione fursa kivingneHilo eneo anza hata kupanda mbogamboga uza utapata mtaji! Kaza mtoto wa kiume! Ukipewa hiyo elfu 50 hutokuwa na machungu nayo, utarudi tena kuomba hapa kwasababu unaona ni rahisi!
Piga hata vibarua viwili vitatu huwezi kosa! Kuna mwenzako naye jana kaanzisha uzi ila ukimpa kazi hataki yeye anataka ela..
Kila la kheri..
Ushauri mzuri mkuu, nimeuchukua. Kazi na fursa zote zina nafasi yake, muhimu ni kusonga mbele.Hatare sana mzee.... Vijana siku hz utasikia nikipata mtu akanipa pesa,, nadhani ukipewa kazi ni rahisi kuliko pesa.... Kazi itakupa uzoefu... Utakutana na watu..... Utakutana na mawazo tofauti tofauti na hapo utajikuta una kua kiakili zaidi na kukufanya uzione fursa kivingne
Nimechoka kutype
Mwenzio kila comment anakazia apewe hiyo elfu 50 we unamjazia maushauri hapa..🙄Hatare sana mzee.... Vijana siku hz utasikia nikipata mtu akanipa pesa,, nadhani ukipewa kazi ni rahisi kuliko pesa.... Kazi itakupa uzoefu... Utakutana na watu..... Utakutana na mawazo tofauti tofauti na hapo utajikuta una kua kiakili zaidi na kukufanya uzione fursa kivingne
Nimechoka kutype
Toka 2012 had leo umekosa elfu 50 ya pamoja?Kwa heshima, kwa kuanzia nahitaji TSh 50,000 tu. Ni kiasi nitakachotumia kuanzisha ufugaji wa kuku na kuanza kujenga hatua kwa hatua. Kama utaweza kunisaidia kwa kiasi hicho au sehemu yake, nitashukuru sana. Mungu awabariki. 🤲🏽