Hilo eneo anza hata kupanda mbogamboga uza utapata mtaji! Kaza mtoto wa kiume! Ukipewa hiyo elfu 50 hutokuwa na machungu nayo, utarudi tena kuomba hapa kwasababu unaona ni rahisi!Sina Mtaji Tyu Nawaza Nifuge Kuku
Mi kipindi naenda kufanya kibarua cha ujenzi sikua na mtaji kaka, mule hauombwi mtaji, ni wewe na ujuzi wako au nguvu, teknolojia imerahissha siku hizi ujenzi kazi sio ngumu mashine ndio zina koroga zege we hubebi zege kichwani unatumiwa kitoroli nk hamna kazi ngumu kule labda uwe mvivu tuSina Mtaji Tyu Nawaza Nifuge Kuku
Hongera huo mziki hakikisha na kuucheza unajua.Kaka kwanini usitafute hata kazi ya kubeba zege? Mi nilipo disco chuo tu nilijichanganya mji wa serikali Dodoma, kujenga majengo Yale kama kibarua asubuhi nipo pale navizia japo Kuna siku unaingia Kuna siku unakosa, unarudi geto, badae nikajiingiza kwenye ujasiriamali, huku nikifanya kazi hotelini kama mhudumu, nikahamia kwenye ulinzi wa usiku ili mchana nijiajiri, nika hustle hivohivo mdogomdogo, nikaanza kuhama mikoa mpaka sasa nataka kuingia kwenye MZIKI sijakurupuka tu kuingia kwenye MZIKI no, nimeanzia mbali mpaka kufika Leo naingia ngazi mpya mziki kwangu NAIONA kama ngazi mpya mana naenda kutumia kipaji changu nilicho pewa na MUNGU mambo mengine anajua yeye MUNGU kama tawin or lose lakini kumove on muhimu kaka hivo pambana sana 2012 ina mana umri wako si mdogo we ni mtu mzima upo kwenye thirty something kaka, ukitinga 40 bila inshu ya kueleweka dah MUNGU atusimamie, lakini mpaka Leo nataka nianze na label yangu ya mziki nikiangalia niliko Toka just a matter of thanks god
Kaka nimejipanga alafu ni kitu kimo kwenye damu since day one dunianiHongera huo mziki hakikisha na kuucheza unajua.
Unahitaji mtaji wa shilingi ngapi wadau waku pushSina Mtaji Tyu Nawaza Nifuge Kuku
Nacheka niniSeran Hata Ushauri unacheka
Kwa heshima, kwa kuanzia nahitaji TSh 50,000 tu. Ni kiasi nitakachotumia kuanzisha ufugaji wa kuku na kuanza kujenga hatua kwa hatua. Kama utaweza kunisaidia kwa kiasi hicho au sehemu yake, nitashukuru sana. Mungu awabariki. 🤲🏽Unahitaji mtaji wa shilingi ngapi wadau waku push
Mkuu hebu kua serious Toka hapo kwenye comfort zone hivi elfu 50k ni Hela ya kushindwa kupata kweli kwa kijana wa miaka 30Kwa heshima, kwa kuanzia nahitaji TSh 50,000 tu. Ni kiasi nitakachotumia kuanzisha ufugaji wa kuku na kuanza kujenga hatua kwa hatua. Kama utaweza kunisaidia kwa kiasi hicho au sehemu yake, nitashukuru sana. Mungu awabariki. 🤲🏽
Kila kitu unacho, rudisha mindset yako maana naona ndio changamoto kubwa uliyonayo.Nimekupata mkuu. Hilo la kutokuchagua kazi nimeanza kulifanyia kazi. Kwa sasa nina mpango wa kuanza ufugaji wa kuku kama njia ya kujiajiri.
Nimesomea mifugo na nina uelewa mzuri wa ufugaji, hivyo changamoto yangu kubwa kwa sasa si maarifa, bali ni kupata mtaji wa kuanzia. Sihitaji kuanza na mradi mkubwa; hata mtaji mdogo utanipa nafasi ya kuanza, kuzalisha na kukuza mradi hatua kwa hatua.
Kama kuna mtu mwenye uwezo wa kunisaidia kwa mtaji wa kuanzia, kuku wa mwanzo, au kunielekeza kwenye fursa ya kuanzia, nitashukuru sana. Niko tayari kufanya kazi; ninachohitaji ni nafasi ya kuanza.
Kila la heri mkuuNimekupata mkuu. Hilo la kutokuchagua kazi nimeanza kulifanyia kazi. Kwa sasa nina wazo la kuanza ufugaji wa kuku, hata kwa mtaji mdogo kabisa. Sitafuti maisha ya mkato; nataka nipate mwanzo ambao utanipa nafasi ya kujisimamia na kukuza hatua kwa hatua.
Kama kuna mtu mwenye uzoefu wa ufugaji au anayoweza kunielekeza kwenye namna ya kuanza kwa mtaji mdogo, nitashukuru sana. Mwanzo mdogo si tatizo, cha muhimu ni kuanza.
KaribuNafanyia kazi ushauri wako asante
Nikajua unataka kuokoa jahazi wengine tumemshauri ujinga😁Mkuu hebu kua serious Toka hapo kwenye comfort zone hivi elfu 50k ni Hela ya kushindwa kupata kweli kwa kijana wa miaka 30
Eneo ulilopo hamna hata vibarua vya 5k kwa siku tukifanya siku kumi ushajipatia mtaji
Nikajua unahitaji kiasi flan reasonable Sasa 50k real??
Hahah mkuu niliona dogo kakomaa kuomba mtaji nikasema ngoja nimtengenezee mazingira wadau wam_pushNikajua unataka kuokoa jahazi wengine tumemshauri ujinga😁
Mkuu nimekupata. Hii 50K kwangu ni mwanzo wa kujitengenezea, si ombi la starehe. Kwa heshima na unyenyekevu, kama kuna nafasi ya kunisukuma hata kwa kiasi chochote, nitashukuru sana. Nikipata mwanzo huu, niko tayari kupambana kwa juhudi zangu. Mungu akubariki sana. 🤲🏽Hahah mkuu niliona dogo kakomaa kuomba mtaji nikasema ngoja nimtengenezee mazingira wadau wam_push
Anaishia kusema 50k. Bado hajachapika vizuri
Ushauri wako nimeupokea mkuu, na ni wa maana sana. 🙏 Sitaki kuchagua kazi; niko tayari kuanza popote penye nafasi na kujifunza. Changamoto kubwa ni kupata mtu wa kunipa nafasi ya kuanzia. Lakini nitaanza kufuatilia mafundi na site za ujenzi huku nikiendelea na mipango yangu. Mungu akijalia, nitapambana mpaka nitoboe. 💪Angalia Fundi ujenzi wa Mataani Kwako Apo, Ongea nae awe anakuchukua Kwenda kibaruani hawana Noma.
Au Tembelea site Za Ujenzi Ajira Zipo Kibao Sema Mchawi HASIRA na nguvu mbona Utatoboa mzee
ngoja nile kusapoti upambanaji wakoTangu 2012 Nimekuwa Nikijaribu Kusimama Tena — Changamoto Niliyonayo Sasa
Wakuu, nimeona leo niandike kitu ambacho kwa muda nimekuwa nikikifikiria sana.
Mwaka 2012 nilifeli masomo. Tangu wakati huo nimepitia vipindi mbalimbali vya maisha—wakati mwingine nikiwa na matumaini, wakati mwingine nikihisi kama nimekwama sehemu moja.
Miaka imepita, lakini bado sijafikia maisha niliyokuwa nimeyafikiria.
Kwa sasa sina ajira wala kipato cha uhakika. Nipo nyumbani na bado natafuta namna ya kuanza upya. Kuna siku mahitaji ya kawaida yanakuwa changamoto, na wakati mwingine hata kiasi kidogo cha fedha kinakuwa na maana kubwa kwa mtu aliye kwenye hali kama hii.
Lakini sitaki huu uwe uzi wa kulalamika.
Nataka kuuliza wale ambao wamewahi kuanzia chini kabisa:
Ukiwa huna kazi, huna mtaji mkubwa, umefeli sehemu fulani ya maisha na unaonekana kama umechelewa kuanza, unaanzia wapi?
Nimekuwa nikifikiria kujiajiri na kuanza kitu kidogo ambacho kinaweza kukua taratibu. Tatizo ni kupata mwanzo na kujua ni wapi niweke nguvu zangu.
Labda kuna mtu hapa amewahi kupitia hali kama yangu na akapata njia ya kusimama tena.
Ningependa kusikia uzoefu wenu—
Ni kitu gani kilikusaidia kutoka kwenye kipindi kigumu?
Uliaanzia wapi bila mtaji mkubwa?
Na ni kosa gani ulifanya ambalo ungependa mtu anayepitia hali kama hii aliepuke?
Mimi bado naamini kwamba kufeli mwaka 2012 hakumaanishi maisha yote yamefeli.
Huenda mtu anayesoma huu uzi akawa na wazo, connection, fursa au hata maneno machache ambayo yanaweza kunipa direction mpya.
Niko tayari kusikiliza.
Safari yangu bado haijaisha.