Tangazo la Kanumba Star Times

Tangazo la Kanumba Star Times

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
950
Japo nia ni kujaribu kuvuta wateja kununua ving'amuzi vya Star times, pengine ubunifu unahitajika katika kuandaa matangazo. Lile tangazo la Star Times linalorushwa na TBC-1 likimwonyesha Kanumba the Great na zawadi ya Kin'gamuzi kwa Kimwana wake kwa ajili ya xmas ni miongoni mwa matangazo ya Kibiashara ambayo uhariri wake ni wa hali ya chini sana..hakuna mwanaume timamu anaweza kufanya yale anayofanya Kanumba (kucheka cheka hovyo)...labda kama ile nafasi ingekuwa ya ze-comedy..

Wanangu leo wameniuliza sasa baba pale ndio nini??...hasa mbona yule kaka (Kanumba) anacheka cheka tu kila siku??..nikawaambia anatangaza ...Nimehisi tangazo lile haliwezi kushwawishi ununuzi wa King'amuzi hasa kwa watoto na watu wazima ambao kwa tafsiri yake ni kana kwamba wanaoguswa ni watu wa aina ile ya Kanumba Kanumba na kina dada wa sampuli ya yule aliye na Kanumba katika katangazo.

Hachana na lime ambalo Kanumba amevaa Jezi ya AC Milan:

startimes.jpg

[h=3]THE GREAT NDANI YA MWANZA NA STARTIMES....[/h]

Kila zawadi niliyoitoa ilinibidi nisaini


ilifika wakati wa kila shabiki wangu kupiga picha na mimi


Wakala maarufu wa startimes Mwanza nilimpa zawadi ya picha tuliyopiga pamoja Dar-Movenpink siku niliyosimikwa rasmi ubalozi.





Huyu mama toka matangazo yakitangaza kuwa Kanumba atakuepo viwanja hivyo toka asubuhi alikaa akinisubiri hata pale watu walipojaa na kumziba asinione pamoja ni mlemavu alipaza sauti akisema mwanangu kanumba naomba nikushike mkono nakuonaga katika tv,na hapo ilikuwa ni saa tisa maskini hajala ili anione tu,nami nilikatisha onesho hili na kuamuru aje mbele kufika kumbe ni mama mlemavu kaletwa na mwanae akimsukuma hakika huruma ilinijaa sana,mama aliongea akilia kuonesha upendo wake kwangu,nilimpatia zawadi toka Startimes lakini pia nilitoa pesa yangu na kumpa mama akale na mwanae,Nilimuuliza Mungu moyoni tizama mama huyu mwenye upendo wa dhati lakini ni mlemavu na asiye na uwezo mzuri kimaisha,vipi vijana wenzetu wenye afya nzuri lakini hawana upendo wala uzalendo kama huu,bali chuki,ugomvi,matusi na kupondana,Dunia hii kwa sasa inahitaji upendo na uzalendo kama huu wa huyu mama...ni maono yangu tu.


Mama akilia baada ya kupokea zawadi huku mwanae akimsukuma ktk baiskeli ya walemavu mara baada ya kuongea na mimi.


Dada huyu akipokea zawadi mara baada ya kuweza kuigiza kicheko changu na watu kumshangilia,sikujua kama mashabiki hufatilia hata jinsi mtu unavyocheka.











 
Mle kuna effect flani zimefanywa utafikiri movie la kihindi yule demu akidondosha makablasha pale!!wabongo wanaigiza hadi matangazo...!!
 
Kweli lile tangazo lipo chini ya viwango kabisa halafu kufanywa na msanii mwenye jina (nimesema jina sio uwezo) kubwa kama Kanumba??
Hatukutegemea makosa ya wazi kivile na kama wameandikiwa still walikua na uwezo wa kurekebisha?
Kwanza binti analazimisha kujua zawadi aliyoandaliwa,naamini zawadi kama haikua kwenye ahadi basi itakua ni ya kushtukiza...
Pili,mi sijaelewa kinachomchekesha kama chizi,ina maana hata anapokua kwake(sijui kwao) anaangalia tv akafurahishwa ndio anacheka vile? Na huyo binti kubwaga magazeti na bag yake ndio nini?
Msilewe sifa hadi kulipua,hao STAR TIMES hakuna anaeona kua limekaa vibaya?
Mbn yule dada (fifi kisura sijui jina lingine) kuna tangazo la godoro kalitendea haki,huku imekuaje??
 
kwanza nakereka nilionapo hilo tangazo yaani halina uhalisia wowote. Nitarudi baadae kidogo
 
That advert is lacking creativity,linabore na halina mashiko,too fake!
 
Kwani Kanumba ana elimu ya advertisement au ni njaa ya kibongo inayomsukuma kutangaza? Umesahau kuwa hata ikulu kuna muigizaji na msanii aitwaye Jaa Kaya au Njaa Kaya?
 
Pale yule dada ameigiza kama mke wa Kanumba ambae wanaishi nae ndani,

Nisichoelewa hicho
king'amuzi alikua akimpa chanini wakati wanacho nyumbani na ndio alikua akiangalia hicho??
 
Aisee Ngoshwe umeniwahi....ilikuwa nilianzishie thread hilo tangazo! Hilo tangazo linachefua sana!
 
Duh, naskia waliilowesha serewali yake wakamkalisha kwenye tuthpick, ndo maana anacheka lakini uso una taharuki
 
Nikionacho hapa ni kuwa na wewe umelipwa na hao Star times ili kuwatangaza bila ya kulipia hapa JF.
Au wewe ndiye Kanumba mwenyewe unapima upepo huku unatangaza biashara?
Kama sivyo hizo events nyingine zinafuata nini kwenye thread yako?
 
STARTIMES wapo wapo tu kama walivyo TING/ATN ... Sina uhakika kama TCRA na mamlaka husika wamefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuwapatia LESENI hawa kwa ajili ya "Analogy-to-Digital" TV broadcasting?

naona kama wanao upungufu wa kila hali
 
Pale kwenye lile Tangazo walichemka sana. Kwa urahisi wa kuangalia kama tangazo limepokelewa waangalie watoto wanalichukuliaje. Yaani pale ni mchemsho wa hali ya juu
 
WABONGO BANA KWAKUKOSOA NDO MANA MTAKUFA MASIKINI....KAMA HAMJUI KANUMBA AMEKULA 86,000,000 (86 MILLIONS) kwa hayo matanganzo na hizo picha...sasa endeleeni kuropoka humuuuu mpaka asubuhi,,, mtaishia kuchangia tuu mwenzenu anakula!!!

ukinichukia shauri yako...ukweli ndo huo ...wabongo wambea!!!!

i hate startimes ...i hate kanumba but i appreciate the guy on his hard work though kuna mpungufu madogo madogo keep it up...
 
Ndio maana Ray anakuambia yeye hawezi kuuza sura kwenye TV kama vile. Kanumba naye anapenda sana kujikweza, alienda south big brother kachemsha.
 
Pale yule dada ameigiza kama mke wa Kanumba ambae wanaishi nae ndani,

Nisichoelewa hicho
king'amuzi alikua akimpa chanini wakati wanacho nyumbani na ndio alikua akiangalia hicho??

Ya Mkuu umegusa penyewec kabisa..sijajuwa kama mume au mke anaweza kununulia mwenzie zawadi ya vitu kama TV, Makochi, Kitanda au meza ya chakula??..Kanumba kafanya "Ukanumba" zaidi..
 
Back
Top Bottom