Tangazo la Kanumba Star Times

WABONGO BANA KWAKUKOSOA NDO MANA MTAKUFA MASIKINI....KAMA HAMJUI KANUMBA AMEKULA 86,000,000 (86 MILLIONS) kwa hayo matanganzo na hizo picha...sasa endeleeni kuropoka humuuuu mpaka asubuhi,,, mtaishia kuchangia tuu mwenzenu anakula!!!

ukinichukia shauri yako...ukweli ndo huo ...wabongo wambea!!!!

i hate startimes ...i hate kanumba but i appreciate the guy on his hard work though kuna mpungufu madogo madogo keep it up...




Na Brighton Masalu
MSIMAMO aliouonesha msanii mwenye hadhi kubwa Bongo ndani ya Tasnia ya Filamu, Vincent Honorat Kigosi a.k.a Ray juu ya ushiriki wake katika matangazo ya biashara, umeonesha dhahiri ni kijembe kwa msanii mwenzake ‘hot cake’ Steven Charles Kanumba.

Katika mahojiano na gazeti moja linalotoka mara mbili kwa wiki (siyo la Global), Ray alisema hataki kushiriki kwenye matangazo ya biashara kwa vile mkataba wake ni wa kisanii na hauna manufaa yoyote zaidi ya kuuza sura.

“Siyo kama sipati matangazo ya biashara kwa ajili ya kutangaza bidhaa, fedha wanayotoa wahusika ni ndogo sana kiasi cha kukatisha tamaa, siwezi kutumika katika matangazo kwa pesa ndogo wakati nikitengeneza filamu napata zaidi ya hiyo.

“Kwa wale wanaopenda sifa za kuonekana bila faida waache tu wafanye, lakini mimi msimamo wangu upo kimaslahi zaidi,” alisema Ray katika gazeti hilo.

Kwa kauli hiyo ikichangiwa na tetesi za bifu la chini kwa chini kati ya magwiji hao, hisia zikalenga kwamba Ray alimnanga Kanumba.

Aidha, Ray aliendelea kusema kwamba jambo lingine linalomfanya akatae matangazo ni pamoja na ukomo wa tangazo kwa sababu wahusika wanaweza kulitumia milele kwa malipo yale yale.
RAY KIZIMBANI
Polisi wa Risasi Mchanganyiko alipompandia Ray hewani na kumsomea mashitaka yake, alisema ni kweli alizungumza maneno hayo na kwamba ndiyo msimamo wake, ila hajamlenga mtu yeyote.

“Ooooh! Unazungumzia ile habari, ni kweli nilisema.

Unajua nini (akitaja jina la mwandishi?) Nafanya kazi kwa ajili ya maisha yangu na mimi kama Ray, msimamo wangu siwezi kushiriki kwenye matangazo ambayo hayana faida.

“Mimi sijatamka yale kwa ajili ya mtu... sikumtaja Kanumba na wala si kwa ajili yake ila kwa manufaa ya maisha yangu. Mtu akijishuku ujue ni yeye...ila mimi bwana, siwezi kuuza sura, nataka kutengeneza pesa,” alisema Ray.

KANUMBA AJIBU MASHAMBULIZI
Kanumba alipopigiwa simu na kuelezwa juu ya madai hayo, alionekana kuwa msikilizaji zaidi hadi pale mwandishi alipohitimisha, alisema hana habari juu ya vijembe hivyo.

“Sikia mimi sijui chochote na hilo gazeti sijaliona, ila kama kweli amesema kwa ajili ya kunilenga mimi, sifa heshima na utukufu navirudisha kwa Mungu. Naishi kwa ajili yake kwa kuwa yeye ni kila kitu kwangu.”


Views: 1025
Tags: mchanyiko11
Like
1 member likes this


ShareTwitter



 
Kwa kweli Msanii Kanumba aambiwe kwa tangazo la kucheka kwa namna ile amechemsha. Kwanza halina ujumbe wa maana. Abuni jingine zuri na hilo liondolewe haraka , linakera saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana!!!!!!!!!!!!!!!
 
WABONGO BANA KWAKUKOSOA NDO MANA MTAKUFA MASIKINI....KAMA HAMJUI KANUMBA AMEKULA 86,000,000 (86 MILLIONS) kwa hayo matanganzo na hizo picha...sasa endeleeni kuropoka humuuuu mpaka asubuhi,,, mtaishia kuchangia tuu mwenzenu anakula!!!

ukinichukia shauri yako...ukweli ndo huo ...wabongo wambea!!!!

i hate startimes ...i hate kanumba but i appreciate the guy on his hard work though kuna mpungufu madogo madogo keep it up...
Jamani tusichanganye mambo. Tuongelee tangazo kama lilivyotoka. Ki ukweli pale tatizo si kanumba ni creator wa hilo tangazo. Hata mimi mwenyewe sikuwa nalielewa kabisa hadi mliposoma hii thread. Hivyo wenye tangazo wanatakiwa wachukue ujumbe kutoka kwa wadau na wajaribu kuboresha. Kanumba tukimsema ni kumuonea yeye kaombwa njoo bwana tutangaze. Akaelekezwa fanya hivi na labda na yeye akaongezea basi wenye kumlipa wakaridhika wakalitoa. Hivyo tunapojadili hili tangazo tusimjadili Kanumba kama yeye hata mimi ningepewa hizo pesa ningefanya wanavyotaka wenyewe.
 
Back
Top Bottom