Tangazo la Hakielimu

Coke Zero

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
1,024
541
Wadau kuna hili tangazo la Hakielimu linarushwa na ITV ambapo linawaonesha wanafunzi wakiwa wamejazana darasani huku wengine wanaanguka na dawati wakati mwalimu anafundisha; kwakweli mwanzoni limenichekesha ila hili tangazo linasikitisha sana,kwa wale ambao mmefanikiwa kuliona mtakubaliana na mimi.
Nimeshashangaa sana kweli baada ya miaka 50 ya uhuru wanafunzi wanapata shida kiasi hiki!.

Mimi nasema kwa style hii Nchi hii itaendelea kuwa nyuma kielimu labda Yesu arudi.
 
Mkuu Haki Elimu huwa wana matangazo yaliyokwenda shule kabisa. Yaan ndio uhalisia wa maisha ya wanafunzi wetu baadhi ya maeneo hasa vijijini.

Hata lile la kugombea choo ni tangazi lenye umakini mkubwa. Sijawahi kuboreka na matangazo yao!

Kudos HAKI ELIMU.....
 
Acha kulitaja jina la Bwana Yesu bure! Mmetaka elimu bure ukiona hali ngumu piga push up!
 
Mkuu Haki Elimu huwa wana matangazo yaliyokwenda shule kabisa. Yaan ndio uhalisia wa maisha ya wanafunzi wetu baadhi ya maeneo hasa vijijini.

Hata lile la kugombea choo ni tangazi lenye umakini mkubwa. Sijawahi kuboreka na matangazo yao!

Kudos HAKI ELIMU.....
Ni kweli mkuu hawa jamaa wanajua kunyesha uhalisia wa mambo!
 
Safari ni ndefu, na bado maandalizi hayajaanza.
Ikiwa kama hatuna mtaala (Curiculum), sera ya Elimu imeshindwa kuainisha lugha ya kufundishia, mtoto anasoma miaka saba ili hali hawezi kusoma na kuandika. Katika jitihada za kuwadanganya wajinga anaongezewa miaka mingine 4 kwa kuambiwa ni ELIMU MSINGI.
Tunakoelekea hata Certificates za NACTE zitzitwa ELIMU MSINGI ili kufunika kombe.
Kuna wanafunzi, baada ya hiyo miaka 13 ya kusoma hawawezi kujieleza. Ikiwa kama huamini, pitia ripoti za NECTA kwa masomo ya Uraia, Kiswahili, na Kiingereza ujionee mwenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom