Tangazo - HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,668
13,237
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
Mkurugenzi wa halmashauri anawatangazia wakazi wote wa manispaa na umma kwa ujumla kuwa:-

1).Ni kosa kuingiza gari zaidi ya tani 3.5 katikati ya jiji bila kibali
2).Ni kosa kujenga uzio bila kibali
3).Ni kosa kufanaya ujenzi bila kibali
4).Ni kosa kumwaga kokoto/mchanga na vifaa vya ujenzi kandikando ya barabara bila ya kibali
5).Ni kosa kubandika matangazo ya aina yoyote,kupitisha gari la matangazo bila kabali
6).Ni kosa kupiga musiki au kufanya sherehe/tamasha bila kibali
7).Ni kosa kutiririsha maji na kutupa takataka bila kibali
8).Ni kosa kukata/kuchimba barabara bila kibali
9).Ni kosa kuonyesha video mitaani
Adhabu kali zitatolewa kwa watakaokuka taratibu.
Imetolewana,
Mkurugenzi wa manispaa
Halmashauri ya manispaa ya Ilala.
Naona haya kama maandishi ya kawaida tu kwani kila mtu anafanya atakavyo na hakuna sheria/hatua zozote zinazo chukuliwa.
Mnasemaje wadau?
 
Mi nimeipenda hiyo yenye red. kwa hiyo wanatoa vibali vya kutiririsha maji na kutupa taka hovyo. yaani ukiwa nacho you are free to do it Lol!
 
ni kweli bora iwe hivyo maana kinondoni hatulali, pamoja na hayo hata chips za mitaani ziache ni uchafu je waliolipia hotel watafanya kazi gani
 
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
Mkurugenzi wa halmashauri anawatangazia wakazi wote wa manispaa na umma kwa ujumla kuwa:-

1).Ni kosa kuingiza gari zaidi ya tani 3.5 katikati ya jiji bila kibali
2).Ni kosa kujenga uzio bila kibali
3).Ni kosa kufanaya ujenzi bila kibali
4).Ni kosa kumwaga kokoto/mchanga na vifaa vya ujenzi kandikando ya barabara bila ya kibali
5).Ni kosa kubandika matangazo ya aina yoyote,kupitisha gari la matangazo bila kabali
6).Ni kosa kupiga musiki au kufanya sherehe/tamasha bila kibali
7).Ni kosa kutiririsha maji na kutupa takataka bila kibali
8).Ni kosa kukata/kuchimba barabara bila kibali
9).Ni kosa kuonyesha video mitaani
Adhabu kali zitatolewa kwa watakaokuka taratibu.
Imetolewana,
Mkurugenzi wa manispaa
Halmashauri ya manispaa ya Ilala.
Naona haya kama maandishi ya kawaida tu kwani kila mtu anafanya atakavyo na hakuna sheria/hatua zozote zinazo chukuliwa.
Mnasemaje wadau?
bila kibali=bila kutoa rushwa; sawa sawa dugu?
 
Ndoto za Abunuasi zinaotwa mchana.... hakuna hata moja litakalo tekelezwa hapo
 
inamaana naweza kuomba kibali nikaruhusiwa kutupa taka hovyo??? Huyu mkurugenzi na ofisi yake ni wapumbavu. Nafikiri ni rudie usemi ule ule kuwa viongozi wa CCM na wafanyakazi ktk idara za umma wameishiwa uwezo wa kufikiri.
 
Hii yote ni kutaka kuonyesha na wao wapo kazini ila hakuna hata moja lenye msingi wa maendeleo hapo, kupoteza muda na kuwafumba wananchi tu waone kuwa mambo yapo ok. Hao viongozi wa manispaa na wahusika wote watafute vitu vya maana vya kufanya na sio kufuatilia VIBALI tuuuuu coz huko kwenye vibali ndiko kuna mianya ya rushwa!!
 
porojo tu

....Nakubaliana nawe. Isingekuwa ni Porojo tu wangetuelekeza nikimkuta jirani yangu anafanya hivyo nipige simu wapi ama niwasiliane na nani. Si kila mmoja anafahamu ofisi zao zilipo!!! Ni Porojo Tu!
 
nadhani watendaji wengi serikalini hasa wa ccm wanafanya kazi bora siku iende hawako result oriented. Hawafuatilii wanachosema kama utekelezaji wake unafanyika au vipi na hawako makini katika kazi zao
Ni kosa kutiririsha maji na kutupa takataka bila kibali
hicho kibali kinapatikani wapi na ni nani huwa anakitoa?
tunahitaji mabadiliko ili tuweze kufanikiwa!
 
Kweli wamechemsha kwa sababu hawawezi kutoa kibali cha kutiririsha maji au kutupa taka barabarani.
 
hehehehe

Manispaa KWISHNEY katika lugha.

Kwa hiyo mkurugenzi na jamaa zake wamekuja na this funny TANGAZO.

nadhani pawekwe katazo lingine

NI KOSA KUFIKIRIA BILA KIBALI.

Kwani hao jamaa wanapaswa kwanza kuzisafisha nafsi zao kutoka ufisadi to utakatifu ndipo hata utendaji wao utakuwa wa haki
 
Ni tangazo zuri sana nafikiri linajaribu kuweka au kusisitiza mpango mji lakini pia kuhakikisha mji unakua bora na salama.

Suala ni je hivo vibali vinatolewa wapi? na ni taratibu zipi zifuatwe ili kupata vibali kama hivo? Je kibali kipi ni halali kwa maana je kuna mfano wa kibali halali ili endapo mtu ukipewa kibali badia uweze kutambua?

pamoja na kwamba nia ni nzuri hii itaishia na kugeuka kuwa Rushwa kwa mlolongo mzima kuwekewa urasimu wa hali ya juu ili kuweza kutoa mianya ya Rushwa.

NI maoni yangu tu...!
 
Watu wanajenga mabaa na maguest house kwenye maeneo ya watu,nani anawapa vibali hivi.Nashindwa kuelewa kwamba kwa miaka zaidi ya 40 tangu uhuru hakukuwa na sheria kama hizi.Wakurugenzi wamechoka kufuikiri wanaishi kwa mazoea.Kinachotakiwa i vitendo kwani maandishi kama haya yapo sana na tumeyazoea.
 
Mpaka ukipate hicho kibali inachukua mwaka mzima.Ukienda utaambiwa barua yako uliyoleta imepotea andika tena,mhusika leo yupo kwenye kikao.Ni karaha tupu.Nadhani inawapasa wabadilike wao kwanza watendaji,na wananchi tutafuatia.
 
bila kibali=bila kutoa rushwa; sawa sawa dugu?

Inasikitisha kuona Wakurugenzi wa Halmashauri wanakuwa miungu watu katika kuwadhibiti watu wa kawaida na kushindwa kusimamiwa mambo ya maana hususani katika kuongeza vitanda katika hospitali ya Amana, kusafisha masoko, kuzoa taka na hata kutuwekea Television kubwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wetu ili tuweze kuona mipira, kupata taarifa mbalimbali za kijamii, maendeleo na uchumi na pia kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imechangiwa na watendaji wa serikali za mitaa. Wananchi tunalipa kodi kwa mujibu wa taratibu na mifumo ya kodi ya Tanzania (Value Added Tax-VAT) ambapo kabla ya kutumia bidhaa yeyote tunayonunua lazima tulipe kodi. Hao vibopa ambao hawalipi kodi na kuneemeka tu na kodi zetu ndiyo wachafua mazingira, wanaojenga uzio ili kuficha maovu yao, kubandika matangazo njiani na kutiririsha maji machafu. Tumechoka kukemewa kama yatima katika nchi yetu. Tenda haki kwa kuacha kutumia gari hilo la shilingi milioni 250 ambalo linaweza kununua vitanda vipya na magodoro mapya katika hospitali yote ya amana na pia kuboresha huduma za kiafya. Pili ndipo uanze kutuma matangazo yako kwenye ubao huu (Jamii forum Platform) ambao hata halmashauri yako haijalipia kodi. Ungekuwa unatenda haki kama jamaa hawa wa jamii forum tungekuwa mbalii. Rudisha kodi zetu kwa kutupa huduma bora nilizotaja hapo juu na siyo kutukemea kama yatima katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom