Asalaam Aleykum,
Nadhani wote tunafuatilia jinsi People's Power kule Misri inavyofanikiwa sasa kuangusha utawala dhalimu wa Hosni Mubarak. Hii ni fundisho kwetu Tanzania na kwingineko kuwa nguvu ya umma kweli ni sauti ya Mungu na hakuna mitutu ya bunduki au vifaru vinavyoweza kuizuia.
Naomba kutoa pendekezo kupitia tangazo hili kuwa na sisi Tanzania sasa tuanzishe "a march of a million" kama ilivyofanyika Misri ili kupinga malipo kwa DOWANS. TUCTA wameanzisha maandamano yao, CUF wameanzisha ya kwao na CHADEMA wametangaza ya kwao. Si ajabu NGOs nao wakatangaza kuandamana. Tatizo ni kuwa maandamano hayo hayana coordination. Kila mtu anapanga tarehe yake kwa hisia yake. Maandamano kama haya yatakuwa fragmented na hatutaweza kupata impact inayokusudiwa.
Watawala wamefanikiwa sana kwenye falsafa ya "divide and rule" au "divide and conquer." Hivi sasa CUF/Chadema na NCCR ni maadui wao kwa wao. Wanakataa kushirikiana na wanachukiana kwa nguvu zote. Haya ni matunda ya kazi ya watawala na wala wapinzani wenyewe hawajui wanaendeleza tu chuki against each other. Hakika, watawala wamefanikiwa kuwa divide na kuwa conquer vyama vya wapinzani. Jambo la kusikitisha ni kuwa hata wao wenyewe hawajui hili.
Lengo ni kuunganisha nguvu zote tuweke tofauti za CUF/Chadema/NCCR pembeni ili tuwe na maandamano ya pamoja makubwa kama ya Misri kupinga malipo kwa DOWANS. Tunahitaji kushirikisha Watanzania wote wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi, NGOs, wakulima, machinga, vyama vya siasa ili watu milioni 1 waingie mtaani kupinga DOWANS ili tuwape onyo watawala kuwa Watanzania sasa tunasema ufisadi BASI!
Naomba maoni/michango yenu ya jinsi ya kufanikisha suala hili haraka iwezekanavyo ili tuwe na "A March of a Million" mwezi huu wa Februari kuleta ukombozi dhidi ya ufisadi hapa nchini.