Tanga na siasa za kujipendekeza

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
859
Kule Kigoma kuna kampeni zinaendelea katika majimbo mawili likiwemo jimbo la Buhigwe.

Ajabu ya siasa za nchi hii eti watumishi wanatoka kwenda kufanya kampeni huko Kigoma. Eti wametoka watu kazini wakapige kampeni mfano mkuu mmoja wa shule katika jiji la Tanga (jina lake na shule yake kwapani kwanza)ameenda kwenye kampeni.

Wameanza kujipendekeza kipindi hiki cha teuzi mbalimbali. Shule hiyo imekua ikiporomoka kitaaluma kwa kuchanganya siasa na kazi.

Ummy atakua anawadanganya wapambe wake hao wakafanye kampeni huko maana yupo Tamisemi. Huyo mwalimu ni miongoni mwz vibaraka wa kisiasa wa Ummy.
  • Halmashauri imezidi kuoza kwani wakuu wa idara wamejichanganya kwenya siasa,wanaibatu na kutumia ofisi vibaya.
  • Mkurugenzi anaishi na kutenda atakavyo.
  • Mkuu wa wilaya yeye watu hawamjui na hata wakaazi wa Tanga ukiwaambia Halmashauri yao haina Mkuu wa Wilaya watakubaliana na wewe. Hana kazi ya kuonekana yani hata asiwepo hapa mjini mwaka mzima ni sawatu.
  • Mkuu wa mkoa ndio anaendeshwa na Mkurugenzi maana jiji ni lake. Hakuna anayeweza kumuita Mkurugenzi na kumuwajibisha.
  • Mbunge wa Tanga ambaye ni Waziri wa Tamisemi Mungu ndio anajua. Ummy yaani Ummy basi yani maana anamuogopa Mkurugenzi sijui kwanini.
  • Mkurugenzi ukimpeleka hata Takukuru utafukuzwa au uwekwe ndani wewe.
  • Katibu Mkuu Tamisemi na yule wa Utumishi tenganisheni utumishi na siasa manake afisa elimu na wakuu wa shule Tanga mjini wao ni siasa,siasa na wao sasa watoto wetu wanafeli. Wao hawaumii kwani watoto wao hawaathiriki na siasa zao.
Mh. Rais saidia watu wa Tanga na siasa za wateule wako zisotija
 
Huo ndio ukweli. Ummy Tanga hiki nikipindi chake cha mwisho na hao chawa wake ndio wameacha kufundisha eti wameenda Kigoma.
Hii ni aibu kwa serikali.

Inamaana CCM hakuna watu wanaoweza kufanya kampeni hadi muwatoe watumishi wa umma Tanga,tena hata hawana sumu ndani ya chama muwapeleke Kigoma?

Aibu kwa Afisaelimu Tanga upande wa sekondari,aibu kwa afisa utumishi na mkurugenzi Mungu atakushuhulikia.

Ummy acha siasa za kizee simamia elimu jimboni kwako.

Hao watu wa bara wanakuvua nguo na wewe hujielewi unakimbiza mwengetu
 
Siasa za awamu ya tano ndiyo zimerudisha CCM Tanga mjini, hili ni jimbo la ACT daima.
Ummy hata awekwe na lasaba anamwagwa hawezi kujenga hoja.

Anamtegemea huyo mkurugenzi wake mwizi,mbadhirifu na bingwa wa rushwa ya hela na ile ya naniiiii.
 
Back
Top Bottom