TANGA: Mvua kubwa iliyodumu kwa siku nzima yaleta maafa

upload_2017-5-9_10-23-12.png


Tanga hali bado ni tete, kuna wingu kubwa la mvua bado liko baharini linaelekea pwani ya Tanga na Dar es Salaam kama picha ya satelite inavyo onyesha saa 3.30 asubuhi
 
Jamani watu wa Tanga poleni sana. Hapo ndio nyumbani nilipozaliwa na kukulia.

Mapango ya Amboni (Kiomoni) hayawezi kuathirika kwa sababu mto Mkulumuzi utabeba maji yote kwenda baharini.

NGUZO wewe sio mtu wa Kiomoni kweli? Nina swahiba wangu pale.
Poleni sana wakazi wa Tanga. Mkuu una uenyeji pale Mafuriko kama unaelekea Kihongwe?
 
Poleni sana wana tanga. Tupo pamoja katika maafa haya. Panapohitajika msaada tujuzane ni vipi tunaweza kusaidia. Maana katika serikali hii msitegemee msaada waserikali.
 
DUA WAKATI MVUA INANYESHA

اللّهُمَّ صَيِّـباً نافِـعاً

"ALLAHUMMA SWAYYIBA NAAFIAN"

MAANA YAKE " Ee Mwenyezi Mungu ijaalie iwe ni yenye kumimika kwa manufaa"

By the way Poleni ndugu zetu ila na huku Dar Mvua inanyesha mpaka sasa kama vile imejiunga na hatupimi bando. ila tuzidi kumuomba Mwenyezi anayeishusha aishushe kwa manufaa kwetu na si kwa madhara, rejea dua hiyo hapo juu.
 
Mvua hii na Amini itakuwa ni Adhabu kutoka kwa Muumba wenu watu wa Tanga mmezidi kuogelea ktk Madhambi maana ukipita ktk viunga vya Tanga jioni na usiku huoni zaidi ya Maovu Viunga vya Raska Zone ndo usiseme watu wanafanya matendo ya kifirauni kwaiyo hiyo mvua isiyo katika Itakuwa kana kwamba mnachuma kile ambacho kimepandwa na mikono yenu na adhabu ya Muumba wetu huwezi izuia kwa mikono bali yatakikana watu wa Tanga mbadilike ndugu zetu muache uovu uliyipita mipaka kwa mfno Uko Tanga kuna kikundi cha Ngoma kiitwacho Baikoko hawa watu wanapendwa sana Tanga karibu Harusi nyingi wanapenda kuwaalika watu hawa nadhani watu wa Tanga mnajua vitu wanavyovifanya ktk Maharusi yenu alafu nyinyi mnawashangilia na kuwatunza watu hawa wanaocheza Uc** wa Mnyama Kweli!!! Mambo haya ndo mnataka Mola wenu asiwaadhibu hapa Duniani?

Tanga punguzeni maaswi
 
Nipo muheza hapa mvua tangia Jana saaa 4 asubuhi mpaka sasa hvi ndio imenyamaza kidogo
 
Back
Top Bottom