Tanga kwetu raha

Tanga kwetu raha

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,423
Reaction score
8,653
Uzi maalumu kwa wana JF walio zaliwa Mkoa wa Tanga hata kama haupo Tanga ila Tanga ndio Nyumbani basi husika Hapa,Dhumuni ni kufahamiana.

Tanga ndio mji unaoendelea kwa kasi Tanzania akiachana Dar, na Arusha,Tanga ndio inafata.

Tanga tumejaaliwa kuletewa mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuja Tanga katika kijiji cha Chongoleani.

Uchumi: uchumi wa Tanga katika miaka ya 2000 ulishuka kutokana na Viwanda vingi kufa lakini ujio wa Bomba la mafuta utapelekea JIJI letu kuendelea kuku-kwa kasi.

Viwanda: Viwanda Unga wa ngano pembe Viwanda vya cement,simba ,rhino Viwanda vya mafuta sabuni na lotion Viwanda vya soda healtho na anjari Kiwanda,cha majani ya chai ya amani Kiwanda cha nondo Ambon plastic,Maji ya kunywa. Tanga fres tunazalisha maziwa ya kuuza Nchi nzima. VIWANDA vipo vingi naomba niishie hapo.

Licha ya kuwa ndio umepangika kuliko mikoa yote Tanzania,
Lakini mkoa,wa Tanga ndio mkoa uliokamilika sana kiasi kwamba wakisema kila mkoa ujitegemee nahisi utakuwa mbali sana.

Utalii Kuna pwani ya pangani Mbuga ya saadani
Shamba la vipepeo lushoto Mapango ya Amboni nk

Michezo: Uwanja,wa mkwakwani Timu,3 kubwa coastal union african,sports na mgambo jkt Coastal waliwa kuchukua ubigwa wa ligi kuu. Japo kwa sasa timu zetu hazipo kwenye ligi kuu lakini tunapambana turudi tena.

Matunda Maembe kule handeni dr idrs rashid ana heka 100 za miembe na ndio muuzaji mkubwa kwa bakhresa,Machungwa,Mananasi,apple Mafenesi nk.

Social: media: Tanga Tv, Redio mwambao, Tanga raha fm nk.

Elimu: zipo shule kubwa kama Tanga tech. Usagala nk


Mimi kama mkaazi wa Tanga, Nawatambulisha kwenu Matajiri- Mabilionea wawili tu wa Jiji la Tanga Bw Gulam ambaye ana kituo cha mafuta mkabala na kituo cha polisi cha kati hapa Tanga, huyu ni mfanyabiashara wa mafuta na Bw Kifaranga ambaye ndie mmiliki wa RATCO ( kampuni ya usafirishaji ) na mwingine ni Mzee Simba mtoto ( kampuni ya usafirishaji )pia !
Kwa Jiji la Tanga ukiwataja hao kwanza unakuwa unazungumzia Wakwasi wa mkoa wa Tanga ijapokuwa wapo wengi sana na wanazidiana tu kwa nukta chache !

Tanga tumejaaliwa kuwa na hotels za nyota tatu kama Tanga beach resort, Nyumbani hotel, Mkonge hotel,Kwetu hotel, Dolphin holel,nk.

Naomba niishie hapo: TANGA NDIO HOME
 
Hapa mashemeji zako tupo wengi,nakusikitikia dada yako hajui hata jinsi ya kuingia facebook humu j.f nasoma mimi tuu akiniuliza kitu sikijui naingia j.f ananiona noma kishenzi siku hiyo usiku ananipa stori zenu zote.
Nisalimie.
 
bundle la offa ya Tanga Tsh 2,000 1 Gb for 1 weeks Vodacom.


Tanga raha bwana HOME SWEET HOME
 
Ni kweli Aisee - Tanga kuna mambo mazuri - haswa Dada Zenu - wanaongea laini laini...........
 
Back
Top Bottom