Tanga... jamani nasema Tangaaa

Kuna Mwalafyale alileta mchele wa biashara, katika kutafuta wateja na soko akutana na mambo hayo hapo juu, licha ya hivyo akitoka kwenye mihangaiko anakuta mahanjumati kwenye sahani vimefunikwa kwa kawa. Baba wa watu ameuza ule mchele akaanza kumega faida, mwisho mtaji, mwisho pesa imekwisha akatafuta kibarua. Imepita miaka mitatu nduguzake wanakuja kumtafuta, wanamkuta na balghashia anatoka na Tasbih.
 
Nimecheka mpaka nimejishtukia hapa kwa MWENDOKASI, na kupaliwa nimepaliwa!
 
..... eti wamemkuta na baraghashia na anatoka na Tasbih...
Hakuwa na Msuli kweli? Wamama wa Tanga wana dhambi sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…