Wapo watu wako tayari kwa mabadiliko, lakini zipo sababu kadha wa kadha kwa nini upinzani haujakomaa vya kutosha Tanga.
Kwanza, wananchi wengi hasa vijijini, hawajui kusoma na kuandika. Ccm wanatumia mwanya huo kushinda kupitia wasimamizi au mawakala wasio waaminifu.
Pili, wazee wengi wa Ccm huwatisha vijana kwa ushirikina kutoviunga mkono vyama vya upinzani, kutokana na uelewa mdogo na elimu ndogo vijana huamini.
Tatu, vyama vya upinzani havijawekeza vya kutosha mkoani Tanga ikiwa ni pamoja na kupata watu wenye kuheshimika katika jamii kuongoza vyama vya upinzani. Hapa sababu za kiuchumi pia huchangia, maana vyama vya upinzani vinahitaji kujitolea kwa hali na mali. Nimekaa Tanga zaidi ya mwaka sijaona mkutano wowote wa vyama vya upinzani katika kata ninayoishi ingawa kuna viongozi wa chadema.
Pamoja na umaskini mkubwa wa wenyeji, bado wanaamini kwamba umaskini wao ni kudra za mwenyezi Mungu, na kwamba mabadiliko kisiasa siyo suluhisho la umaskini wao. Yaani umaskini umefanywa kama dini.
Zipo sehemu ambazo wageni wengi wamehamia kama Muheza, naona kuna matumaini kiasi.
Nashauri kipindi hiki cha uchaguzi, ukawa wabebe jukumu la kugharamia kampeni hasa katika majimbo ya handeni, kilindi, mkinga na korogwe pamoja na kuweka mawakala waaminifu, zipo kura za vijana zitapatikana ambazo zitaongeza kibaba, lakini pia itakuwa mwanzo wa kuutambulisha upinzani hadi ngazi ya vijiji.
Huo ndiyo uzoefu wangu angalau kwa uchache na mkoa wa Tanga.