Tanga city needs traffic light | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanga city needs traffic light

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KUNANI PALE TGA, Sep 2, 2011.

 1. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Habari zenu wakuu.
  Jiji la Tanga sasa linahitaji traffic lights ili kuepusha ajali katika barabara nyingi muhimu.
  mfano kwenye mkutano wa barabara ya kwenda tanfamano na mkwakwani,hostel ya usagara,na bank street. pia zipo nyingi na  members wengine waorodheshe hizo barabara. naomba kama kuna member wa halmashauri ya jiji la tanga humu ndani ya forum afikirie hii hoja. its very important.
  asante
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  nikitoka Ileje nakuja Tangaaaa.......
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama mnataka traffic lights labda mngalikuwa na madiwani wenye upeo wa hali ya juu na uwezo wa kohoji fedha za umma, sio madiwani wa sasa hivi mazoba tu kama ninavoyasikia. Zaidi ya hapo mnatakiwa kuwa na meya mwenye uwezo sio aina ya yule aliyekuwepo kisauni nasikia ndo alikuwa alwatani na mambo hayaendi,otherwise maskini tanga endeleeni na jembe na nyundo tu...!
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280

  Hivi halmashauri ya jiji la Tanga mpaka uwe member? au sijamuelewa huyu Mtanga jamani?

  Usijali nakutania tuu.

  Tanga kunaniiiii? kuna trafic lights jamani. Ukifanikisha hili ombi lako nijulishe nije kutembea huko, I love Tanga.
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Hapa kwenye msikiti wa Ijumaa Makorora kunahitajika traffic light pia, na msikiti wa Kwanjeka panatakiwa keep left
   
 6. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli jiji la Tanga idadi ya magari inaongezeka siku hadi siku. Isipokuwa jiji hili linaonekana kuwa na barabara nyingi kiasi ambacho sidhani kama tatizo la msongamano wa magari linaweza kutokea hapo mbeleni. Ukilinganisha na mji kama Moshi ambao kwa sasa unanyemelewa na tatizo la ''traffic jam''. Na halmashauri ya jiji letu inapaswa kuchukua hatua kuboresha baadhi ya sehemu mf. njia panda karibu na hostel ya usagara sec. Pia maeneo ya Toyota na pale njia panda ya karibu na Splendid view. Na kuna maeneo mengi tu. Pia kuna suala la matuta ya barabarani,baadhi ya matuta yaliyowekwa katika barabara za jiji hili yamekuwa sio matuta bali ni kama misingi. Mf. barabara ya Bombo karibu na hospitali.
   
 7. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  traffic lights ni moja tu. bado barabara kama ya makoko ikitokea bb ya1 mpaka 20 ni muhimu lakini ni mbovu na ina aibisha mji wetu. yaani sijui viongozi wa hili jiji hawaoni aibu kama mimi.tanga barabara zimekwisha na zinaaibisha. pia zile street lights haziwaki, yaani usiku ni giza tupu. viongozi ni vipofu hawaoni au ni wavivu kufanya kazi au pesa zimeliwa. tanga barabara ni chafu na zina vumbi haivumiliki.
   
 8. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  kaka traffic light inayosema ni moja iko wapi?
  Kuhusu barabara kweli ni tatizo,ila tatizo ni kuwa barabara nyingi zinazojengwa kwa sasa nadhani zinajengwa chini ya kiwango. Kwa mfano tazama barabara ambazo zilijengwa na konoike mnamo mwaka 1999 mpaka leo zile barabara zimedumu ila hizi nyingine hazina ubora.
   
 9. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Tanga, Kunani hukooo, mbona kila kitu huko kimekwisha. *mkoloni voice*
   
 10. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa maoni yangu jiji la tanga halijafikia hadhi ya kuwa na trafic lights kwani nature ya barabara zilizopo na idadi ya magari yaliyopo iwapo taa hizo zitawekwa zitasababisha msongamano .Upo wakati maeneo yaliyotatwa hapo juu yanakuwa tupu bila magari kwa muda mrefu au je itakuwa busara gari moja kusubiri kuruhusiwa kwa muda mrefu wakati upande mwingine hauna magari?Haya ni maoni yangu kama mdau wa barabara tanga
   
 11. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #11
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wazungu wanasema prevention is better than cure. mdau hapo juu kasema tanga bado hakuna haja ya kuwa na traffic lights. lakini barabara ambazo nimezitaja ni muhimu sana kwani asubuhi na mchana zinakuwa bize sana. kila mtu anakata au kukatisha barabara bila kujua nani asimame na nani apite. uki fanya reaserch kwenye hizo barabara utajua umuhimu wa kuwa na hizo taa.
   
 12. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kutengeneza Round abouts (keep left) ni bora zaidi kuliko kujenga traffic lights, ukizingatia pia kuwepo na tatizo la kutokuwa na umeme wa uhakika-tatizo litarudi pale pale pindi umeme ukikosekana.
   
 13. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Traffic lights bila umeme, yangu macho.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Bado una fikra za kizamaaani, tembelea Dar na Arusha ukaone Traffic Lights za solar.
   
 15. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  hivi kazi ya traffic lights ni nini? kuongoza magari?
  1. tanga hamna foleni ya magari,labda wakati kichwa cha treni kinavuka barabara pale brbr ya 1
  2. kumlika barabara? labda kwani kuna waendesha bike wengi bike zao hazi taa
  3.kupamba jj? labda japokuwa kuna taa nyingi barabarani tangu unapoingia mizani,
  kwa ujumla tanga hamna foleni kabisaaa... cjawahi hata kuona askari (traffic) wakiongoza magari hata mara 1. mtoa mada labda
  aniambie. hyo bjt ya kuweka taa wangeboresha barabara ya 15, kichefuchefu barabara maarufu kama ile kuwa vile katikati ya jj
   
 16. N

  Ngokongosha JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 709
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 180
  hata huku mwanza tunatumia traffic lights za solar
   
 17. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  barabara za Tanga ni chafu na mbovu mno zinahitaji kutengenezwa. Tanga hakuna foleni ya kutisha na nadhani keepleft ni bora zaidi kwa tanga kuliko traffic lights kwani mtu anakuwa anauwezo wa kutumia barabara nyingine kufika anakotaka. Stendi ya Tanga nayo inahitaji maboresho na nadhani nivizuri ikahamishwa pale na kupelekwa kwa minchi chumbageni au Majani mapana
   
 18. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  swali hili angefaa aulizwe nyerere ... bahati mbaya keshatangulia kwa mola wake...
   
 19. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Madiwani wenu ndo mzigo wenu,
  Utawakuta pale Tawaqal barabara ya 4 mguu juu wakunywa juice ya tende masaa mawili hajamaliza glass moja, huo muda wa kujadili maendeleo ataupata wapi?

  Yaani kwa kweli hilo jiji halina mwamko wa maendeleo kabisa, duka linafunguliwa saa 5 asubuhi, then saa 9 linafugwa unategemea nini hapo jomba, Yaani wazawa wa hapo ni wavivu ile mbaya!
   
Loading...