Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima

Tatizo kwetu Mbagala!



View attachment 20534 NOT A TRADE FAIR!:It was empty containers everywhere at this Mbagala-Kizuiani (Dar es Salaam) spot yesterday - & is the case almost daily these days-as local residents queued for hours for water.The scarcity of the precious liquid is blamed largely on power shedding in the city and other parts of Tanzania. Picha kwa hisani ya IPPMedia
attachment.php

Huku kwetu mbagala, bado tunategemea maji ya visima na siku umeme hakuna basi ujue na maji itakuwa tabu.
Bahati mbaya huku ndio njia ya kuelekea kusini na wengi wetu ni wanazi wa sisiemu hivyo watawala hawana haja ya kujipendekeza.
 
Mgawo umeme sasa balaa


*Wanafunzi wa vyuo vikuu waja juu wagoma
*TRA 'Long room' shughuli za siku zakwama


Na Tumaini Makene

KATIKA hali inayotishia tatizo la mgawo wa umeme nchini kuanza kuathiri sekta nyeti nchini, baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kilichopo Chang'ombe Dar es Salaam jana waligoma kwa
saa kadhaa kuendelea na masomo wakilalamikia masuala kadhaa likiwemo tatizo la mgawo wa umeme chuoni hapo.

Hali hiyo imekuja siku moja baada ya wanafunzi wengine wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)mkoani Iringa nao kugoma, huku kati ya masuala waliyolalamikia mojawapo likiwa ni tatizo la umeme linalotokana na mgawo, usiojulikana mwisho wake, unaoendelea nchi nzima.

Wakati wanafunzi wakiathiriwa na matatizo ya mgawo wa umeme nchini unaoendelea bila mamlaka husika kueleza bayana ni lini utakoma, kitengo kingine nyeti cha serikali katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) maarufu kama 'Long room' juzi wafanyakazi na wateja waliokuwa wakiendelea na mchakato wa kukamilisha taratibu za kuchukua mizigo yao, walilazimika kukwama baada ya jenereta lililokuwa likitumika kutokana na mgawo wa umeme, kupata hitilafu.

Wakizungumzia sababu za mgomo wao wanafunzi wa DUCE ambao madai yao yanafanana na wenzao wa MUCE, yaani kucheleweshewa fedha za kujikimu, ukosefu wa umeme wa uhakika na tatizo la vitambulisho vya bima ya afya kwa ajili ya matibabu yao walisema kuwa hadi jana walikuwa hawajui watapata lini fedha za kujikimu.

Walieleza kuwa walipaswa kupata pesa hizo tangu wiki iliyopita, lakini wameshangazwa na ukimya wa mamlaka husika kushindwa kutoa fedha hizo wanazotegemea kwa matumizi na kugharamia maisha yao ya kila siku chuoni hapo.

Wakitolea mfano wa usumbufu wa tatizo la umeme chuoni hapo, baadhi ya wanafunzi waliozungumza na Majira, walisema kuwa moja ya jengo la mihadhara ya masomo ambalo limeanza kutumika hivi karibuni, limejengwa kwa vifaa vya kisasa, kiasi ambacho kama hakuna umeme wa uhakika, hawawezi kuendelea na masomo.

"Mbali ya suala hilo la fedha kuna tatizo la umeme...mambo mengi sasa hayaendi kwa sababu ya mgawo wa umeme unaotuathiri huku jenereta letu likiwa bovu tangu mwaka jana na hatujui litatengenezwa lini...lakini pia bajeti ya hilo jenereta inakwenda wapi, kama halifanyi kazi...?

"Hilo jengo unaloliona hapo, lina 'Lectrure rooms( jengo la mihadhara) halina muda mrefu tangu lianze kutumika...limejengwa kisasa sana, kiasi kwamba vitu vyake vingi vinatumia umeme.

"Kwa mfano huwezi kusoma mle bila kuwa na 'power point'(mashine ya kusaidia kukuza maandishi na vielelezo ubaoni) hiyo mara nyingi kwa sababu umeme unasumbua na hakuna jenereta, vipindi vingi vimekuwa vikishindikana kufanyika, hasa vile vyenye hadhara kubwa kama wanafunzi mia tano," alisema mmoja wa wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina moja la Mayunga.

Mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la kutopata matibabu ipasavyo kwa sababu hawana vitambulisho vya bima ya afya, pamoja na kuwa walishavilipia sh. 50,000, kwa kila mmoja, mapema wakati wa kusajiliwa kuingia chuoni, lakini mpaka leo hawajavipata.

"Kulipia vitambulisho sh. 50,000 ilikuwa ni moja ya sharti muhimu wakati wa usajili, bila hivyo mtu asingeweza kupata usajili, lakini tunashangaa tangu wakati huo hatujapata vitambulisho, hivyo hatuwezi kupata matibabu.

"Kila tunapofuatilia hatupati majibu yanayoeleweka hapa chuoni...watu wanaohusika na bima hiyo tumejaribu kuwauliza wanasema kila mara kuwa hawajapata fedha hizo kutoka chuoni hivyo hawawezi kutoa vitambulisho bila fedha hizo," alisema mwanafunzi huyo wa kiume.

Majira jana lilishuhudia takribani wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza chuoni DUCE, wakiwa nje ya madarasa wakishinikiza wapatiwe fedha hizo za kujikimu, baada ya kuwa wameishi maisha ya kubahatisha na wasiwasi tangu Januari 15, siku ambayo walipaswa kupata fedha zao za awamu ya pili, kwa muhula wa kwanza wa masomo, mwaka 2010/2011.

Wakizungumza na Majira, wanafunzi hao walisema kuwa sababu kubwa iliyowafanya kuchukua uamuzi wa kugoma kuingia madarasani, ni kucheleweshewa fedha hizo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Jitihada za Naibu Makamu Mkuu wa DUCE anayeshughulikia Utawala, Mipango na Fedha, Profesa Bavo Nyichomba, kuwatuliza wanafunzi hao walioonekana kuwa na munkari wakilalamika wamekuwa wakiishi maisha ya dhiki, ikiwemo kula kwa shida, ziligonga mwamba mwanzoni, wakisema hawakubali kurubunika kwa ahadi ya 'kesho, kesho'.

Baada ya mvutano wa zaidi ya nusu saa, huku wanafunzi hao wakisisitiza kuwa hawataweza kuingia madarasani na kusoma hadi hapo watakapopata fedha, hatimaye walikubaliana na kauli ya Prof. Nyichomba kuwa watapatiwa fedha hizo leo, Jumatano.

Akizungumza na waandishi wa habari baadae, Prof. Nyichomba alisema kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuushukuru uongozi wa DUCE kwa jitihada uliofanya kushughulikia suala hilo la upatikanaji wa fedha zao za kujikimu.

"Unajua wanataka fedha zao ambazo walipaswa wapewe tangu tarehe 15, lakini wakawa hawajapata...sasa kutokana na utaratibu mgumu wa kibenki kama zingepitia katika akaunti zao moja kwa moja kutoka bodi ya mikopo, wangechelewa kuzipata...hivyo sisi kama walezi wa vijana tukajitolea kubeba mzigo huo.

"Tukazungumza na watu wa Bodi waziweke fedha hizo katika akaunti yetu ya chuo...tangu mapema tulijua tutawapatia Jumatano (yaani leo), lakini tuliwaambia Ijumaa, maana hawa vijana ukiwaambia kuwa itakuwa Jumatano halafu ikawa vinginevyo hawawezi kukuelewa...lakini tulijua kesho watapata fedha zao.

"Tayari tumeshazungumza na benki, maana nao wanahitaji muwapatie taarifa siku moja kabla ili wajiandae, tayari tumezungumza nao, ili tuchukue fedha na kesho (leo) vijana wapate," alisema Prof. Nyichomba.

Jitihada za Majira kutaka kupata majibu sahihi ya sababu zinazokwamisha wanafunzi wa elimu ya juu kupata fedha zao za kujikimu kwa muda muafaka, lakini wanapogoma zinapatikana, hazikuweza kuzaa matunda baada ya kufika Bodi ya Mikopo na kuelezwa kuwa wafanyakazi hao hawatoi huduma wakati wa mchana, kwani ni muda wa chakula.

Kwa tukio la jana, DUCE sasa kinakuwa chuo cha nne wanafunzi wake wakigoma takribani ndani ya mwezi mmoja, baada ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, Chuo Kikuu Ardhi, kufanya hivyona kufuatiwa na MUCE juzi.

Pamoja na kuwepo madai mengine kama hayo ya matatizo ya umeme, bima za afya, ubovu wa miundombinu na huduma zingine za kijamii, uhaba wa wakufunzi na vifaa vya ufundishaji, upatikanaji wa fedha za mikopo, kwa ajili ya kulipia ada ya mafunzo chuoni, kujikimu, mafunzo kwa vitendo, limekuwa sugu, tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo, takribani miaka sita iliyopita.
 
Ukweli unabaki palepale ya kuwa bila ya kushinda vita dhidi ya ufisadi taifa hili ni kaput..............finito tu.............................
 
Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya kuifilisi Tanzania.
 
hakuna kitu kianaendelea, umeme unakwatwa kila siku asbuhi mpaka jioni, nilitegemea serikali makini ikilichukulia swala hili kama la kipaumbele, lakini hawa ndugu wako busy wanatafuta hela ya kuwalipa dowans, serikali ya CCM mnatutesa sana, mmefeli tafadhali kaeni pembeni
 
tatizo si TANESCO tatizo ni serikali ya CCM, umeme unapokua hovyo namna hii ni issue ya kitaifa, hili ni suala la miundombinu, TANESCO does not have much to do ili kubadili hali hii SERIKALI ina maswali mengi sana ya kutujibu, zile bilioni wanazotaka kuwa dowans kwa nini tusizitumie kuboresha miundo mbinu ya umeme? Serikali ya Kikwete imeshindwa kudeliver
 
Hali ni mbaya,
Joto limezidi!
Wanene wanazo standby generators na hivyo ukubwa wa tatizo haliwezi kuwafikirisha sana!
Cha muhimu ni kuwalipa dowans?
As far as I'm concerned, I prefer silent vice to ostentatious virtue.

 
hakuna kitu kianaendelea, umeme unakwatwa kila siku asbuhi mpaka jioni, nilitegemea serikali makini ikilichukulia swala hili kama la kipaumbele, lakini hawa ndugu wako busy wanatafuta hela ya kuwalipa dowans, serikali ya CCM mnatutesa sana, mmefeli tafadhali kaeni pembeni

Hawatafuti pesa ya kuwalipa ila wanafuta vijisababu vya kuwaconvince wadanganyika wakubali kilaini!!Hata hivyo tatizo la umeme hawawezi kulipa kipaumbele kwasababu binafsi haiwagusi!
 
Hawatafuti pesa ya kuwalipa ila wanafuta vijisababu vya kuwaconvince wadanganyika wakubali kilaini!!Hata hivyo tatizo la umeme hawawezi kulipa kipaumbele kwasababu binafsi haiwagusi!
Kweli kabisa sababu wao haliwagusi halina umuhimu kwao!!
 
Back
Top Bottom