Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima

yaani mpaka kwenye hii karne si bado tuna imani zetu za chini ya miti.....eti umeme mpaka mvua inyeshe......hii kuishi kwa bahati na sibu itaendelea mpaka lini?
 
Tatizo la umeme ni hadi mitango ya Dowans inunuliwe. Kwani huoni tatizo limeaza baada tu ya Mh. Kikwetu kuapishwa? Mlivo bisha sana wakaongeza makali? Mkiendelea kubisha wataukata moja kwa moja ...
 
Nimesikia kwamba sasa 10 MW project ndogo ndogo (SPP) zimeruhusiwa, see www.ewura.go.tz/.../Guidelines%20for%20Grid%20Interconnection%20- %20Part%20C.pdf. Let us have genuine investment in this sector. Tunachohitaji ni kuharakisha hizi projects. Hawa Tanesco wameshashindwa, hata wakiweza pesa zao zitagawanywa na kuliwa, watafilisika.
 
Tumepokea taarifa ya hali ya bajeti yetu. Tumekumbwa na matatizo mawili ambayo 'hatukuyategemea'. Umeme na Upungufu wa Chakula. Hatukutegemea mvua zitakuwa haba. (Kufeli kwa wanafunzi tulitegemea ndio maana hatujaomba kusaidiwa).

Tumeomba msaada kwa wahisani. Tunasubiri majibu.

WanaJf, wakati tunasubiri wahisani watusaidie tufanyeje? Hakuna umeme, njaa inatunyemelea! Lets talk constructively about this.

Wenzetu wanafanyaje? Wametatuaje haya matatizo?

In the meantime, MwanaJf, change ur working times kama unaweza. Was happy to see mafundi welding na vinyozi working at night!

the government is seting itself on fire man. kwenye kampeni JK alikuwa anaongea as if tukimpa yeye urais wazungu watamwaga pesa na matatizo yetu yote yatakwisha. It is the same mindset inayomfanya asishutuke na kuweka mikakati ya kutatua matatizo ya wananchi kwa sababu yeye anasubiri tu tatizo liwe kubwa awaambie wafadhili wasaidie! This time round, sijui!
 
Mie si mwanasheria natoa ushauri huku nikiomba ufafanuzi. Hivi karibuni tumepata habari ambazo si rasmi toka magazetini kuwa mitambo ya dowans ni "ya rostam". Hivi serikali haiwezi kumaliza mvutano uliopo kwa kukaa na "rostam" na kumueleza kama yeye ni mzalendo haswa wayamalize nje ya mahakama kwa arrangement ya win-win na serikali imuhakikishie mitambo ya dowans inawaka leo au kesho kwa malipo stahiki. Kwa vyovyote kwa upeo wetu tutahitaji mitambo ya aina hiyo iwe ya "dowans bin rostam" au ya kipenengule au mr green!!!!!
 
MGAO wa umeme umerudi tena kwa kasi mpya na hali hiyo kuwafanya wakazi wa jiji kushidwa kuendesha shughuli zao ipasavyo.
Mgao huo uliotangazwa mwanzoni mwa wiki hii ni mkali kuliko ule ulioisha awali na kutangaza kuwa utakuwa unakatika kwa siku tatu hadi kwa wiki.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania [Tanesco] Felchesmi Mramba alsiema mgao huo unatokana na kupungua kwa Megawat 230 za grade ya Taifa.

Pia na kushuka kwa kina cha maji katika bwawa la Mtera, mgawo huo utaendelea hadi mvua sitakapoanza kunyesha.
 
Ari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi....mpaka tunyooke kudadadeeki.Poleni sana ndugu zangu,huku kwetu no mgawo...ukikatika only 5minutes!
 
umeme ni kitu muhimu......sijaona hao wanaojiita wanasiasa wakijaribu kuchukua hatua kunusuru tatizo lililopo...wao ni kuponda tu.....ni heri MZEE WA NJI HII ALIWAHI KUJARIBU KUTAKA KUTUSAIDIA WATANZANIA......NA KUSAIDIA SI LAZIMA UWEPO MADARAKANI
 
Back
Top Bottom