Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Baba_Enock, Dec 12, 2010.

 1. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Takribani wiki moja imepita tangu TANESCO walipotangaza kusitishwa zoezi la mgao wa umeme - Cha ajabu ni kwamba - baada ya kauli hiyo - ukanda huu wa Tegeta tumekuwa tukikatiwa umeme kila siku na wakati mwingine masaa 12! - Ninapoandika ujumbe huu umeme umekatika tangia saa moja ya asubuhi na kila mara unapouliza "Tanesco" unaambiwa kuna "itilafu" na mafundi wanarekebisha umeme utarudi muda sio mrefu - hizi "itilafu" ni nini?

  Au mgao bado unaendelea kimya kimya?

  Nadhani imefika wakati wa "kutembea na revolver" na ukipewa majibu ya "kihuni" you simply "shoot point-blank" - Far East hii ilitokea sana esp Thailand na huduma kwa wateja ilibadilka "dramatically" - copy that?

  ======================
  UPDATE: Wametangaza mgawo nchi nzima!

  Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima

  Thursday, 23 December 2010
  Exuper Kachenje
  Mwananchi

  SHIRIKA la Umeme (Tanesco) jana lilitangaza mgawo mpya na mkubwa wa nishati hiyo ambao utavifanya viwanda, maduka, ofisi na makazi kukosa umeme kwa kati ya masaa sita hadi 12 kwa muda wa mwezi mzima.

  Tangazo hilo la mgawo ambalo limekuja katika kipindi ambacho mjadala wa jenereta za kampuni ya Dowans ukiwa umeibuka tena, linatarajiwa kuongeza gharama za maisha kutokana na ukweli kuwa viwanda vingi vitalazimika kutumia jenereta katika uzalishaji licha ya Tanesco kutangaza kuwa vitapewa umeme nyakati za mchana.

  Wananchi ambao kipato chao kinategemea biashara ya samaki, saluni, na vinywaji pia wataguswa na makali hayo moja kwa moja wakati mabenki, vituo vya mafuta, mahoteli na makampuni mengine ya kutoa huduma yatajikuta yakiingia gharama kubwa katika utendaji wao.

  Tangazo la Tanesco limetolewa wakati kukiwa na ahadi kemkem za kumaliza kabisa tatizo la mgawo wa umeme, huku Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikiwa imeliruhusu shirika hilo la umma kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 18.5.

  "Mgawo huu wa umeme umeshaanza kwenye mikoa yote na utadumu kwa majuma manne hadi katikati ya mwezi Januari mwakani," alisema meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alipoongea na waandishi jana.

  "Mgawo utahusisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa isipokuwa mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara."

  Kwa mujibu wa Masoud, mgawo wa sasa umetokana na upungufu wa umeme uliojitokeza baada ya moja ya visima vinavyozalisha gesi vya kampuni ya Pan African Energy, kuzimwa.

  Alisema kisima hicho kinachotoa gesi kimezimwa kwa ajili ya kukifanyia matengenezo ya kawaida, hivyo kusababisha upungufu wa megawati 40 za umeme zinazokwenda katika gridi ya taifa.

  Pan African Energy ni kampuni ambayo inachimba gesi hiyo eneo la Songo Songo, Kilwa na baadaye husafishwa na kusafirishwa na kampuni ya Songas ambayo huzalisha umeme wa megawati 180 eneo la Ubungo na kuiuzia Tanesco.

  Kwa mujibu wa makubaliano, Songas hutakiwa kuzalisha umeme kwa kiwango kilicho kwenye mkataba na ni jukumu la Tanesco kuutumia umeme huo wa gesi kulingana na mahitaji yake au kutoutumia. Tanesco huilipa Songas hata pale inapokuwa haitumii umeme wa kampuni hiyo.

  Badra alisema kuwa kiwango hicho cha upungufu wa umeme kinaweza kuongezeka hadi kufikia megawati 120 jambo alilosema likitokea, shirikma hilo litazidisha mgawo.

  “Wakati mwingine kunapokuwa na peak (matumizi yanakuwa makubwa), upungufu unaweza kufikia megawati 120. Ikitokea hivyo, kwa kuwa sasa tunategemea uzalishaji umeme kwa njia ya maji, itabidi nasi tuongeze mgawo,” alisema Badra.

  Alieleza kuwa mgawo huo utaanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika baadhi ya maeneo huku maeneo yaliyopata umeme katika muda huo yakiukosa kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku mara tatu kwa wiki.

  Kwa mujibu wa Badra, ratiba ya mgawo huo zitatangazwa katika magazeti na vyombo vingine vya habari.

  Hata hivyo, alisema baadhi ya maeneo hayatakumbwa na mgawo huo akitaja baadhi kuwa ni hospitali, pampu za maji, migodi na viwandani ambako alisema vitakosa umeme usiku ili mchana viendelee kuzalisha.

  Alisema kuwa maeneo yanayopata umeme kutoka transoma ya Kipawa hawatakumbwa na mgawo huo, kutokana na kukamilika kwa matengenezo yake.

  “Transfoma ya Kipawa imeshatengemaa na hivyo kuanzia Desemba 23 (jana) haki ya kupata umeme katika maeneo yaliyoathirika kutokana na kuharibika kwa transfoma hiyo, itarejea kama kawaida na wateja wa maeneo hayo hawatakumbwa na mgawo huu tulioutangaza,” alisema Badra.

  Baadhi ya maeneo yanayopata umeme kutoka transfoma hilo ni pamoja na Yombo Dovya, Tandika, Temeke, Chang’ombe, Chamazi, Tazara, Maji Matitu, Charambe, Keko na Uwanja wa Taifa.

  Akizungumzia siku kuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, Badra alisema Tanesco itajitahidi kuhakikisha wananchi wanasherehekea siku hizo bila kukosa umeme huku akiwaomba radhi kwa mgawo huo.

  Mgawo wa umeme, ambao ulizalisha kashfa kubwa ya Richmond ulipoibuka mwaka 2006, umeshaanza kuzoeleka kwa wananchi na ahadi za shirika hilo na wizara kugeuza tatizo hilo kuwa historia, sasa zinaonekana za kawaida.

  Machi 16 mwaka huu Tanesco ilitangaza mgawo wa umeme katika mikoa yote ya Tanzania Bara uliokuwa wa saa tano kila siku. Wakati mgawo huo ukiisha, Tanesco ilitangaza kuwa tatizo la umeme sasa litakuwa historia.

  Watanzania, ambao ni asilimia 12 tu wanaotumia huduma hiyo majumbani, pia walipata machungu ya mgawo wa umeme Oktoba mwaka uliopita ambapo walikosa huduma hiyo kwa saa 12 kwa siku.

  Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo Stephen Mabada, alitangaza mgawo huo akieleza kwamba Tanesco ililazimika kuanza mgawo huo kutokana na upungufu mkubwa wa uzalishaji umeme, uliosababishwa na kuharibika kwa mitambo minne kwenye vituo vya uzalishaji wa nishati hiyo.

  Mitambo iliyoharibika ilikuwa ni ya Kidatu, mkoani Morogoro, Kihansi (Iringa) na Pangani (Tanga) wakati jijini Dar es Salaam mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia wa Songas pia uliripotiwa kuharibika.

  Wakati huo, serikali iliamuru kuwashwa kwa mitambo inayozalisha umeme kwa kutumia mafuta ya IPTL licha ya kampuni hiyo na Tanesco kuwa kwenye mgogoro mkubwa ambao unashughulikiwa mahakamani.

  Matatizo makubwa ya umeme yaliibuka mwaka 2006 wakati nchi ilipokumbwa na janga kubwa la ukame na ikabidi serikali ichukue hatua za dharura kumaliza tatizo hilo.

  Lakini hatua hizo za dharura zikaishia kwenye kashfa kubwa ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme kwa kampuni ya Richmond Development LLC, ambayo ilidhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake kwenye mkataba.

  Baadaye mkataba huo ulirithishwa kwa kampuni ya Dowans Tanzania ambayo, licha ya kuchelewa, ilileta nchini mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 120.

  Lakini mwaka 2008 Tanesco ilikatisha mkataba huo mwaka mmoja kabla ya kumalizika, ikidai kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ilikiukwa wakati wa kuingia mkataba huo, lakini ikaahidi kuwa ina uwezo wa kuzalisha umeme bila ya kutegemea jenereta hizo.

  Uamuzi huo uliifanya Dowans kufungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), ikidai kuwa taratibu hazikufuatwa wakati wa kuvunja mkataba huo.

  Mwaka mmoja baadaye Tanesco ikaibuka na hoja ya kutaka kuinunua mitambo hiyo ya Dowans, ikidai kuwa nchi ilikuwa hatarini kuingia kwenye tatizo kubwa la umeme na kwamba isingekuwa rahisi kununua mitambo mingine kabla ya tatizo hilo kuanza.

  Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na Kamati ya Madini na Nishati ambayo ilieleza kuwa kununua mitambo hiyo mitumba ni kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma, kitu kilichomfanya mkurugenzi wa Tanesco wa wakati huo, Dk Idris Rashid kutoa tamko kuwa iwapo nchi itaingia gizani, asilaumiwe.

  Mapema mwezi huu, ICC) ilitoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Dowans na kuiamuru Tanesco kuilipa kampuni hiyo binafsi fidia ya Sh185 bilioni.
   
 2. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2010
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,789
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280

  Hapa nilipo kuna giza totoro joto ni kali, ikanilazimu kuwapigia watu wa TANESCO kuwauliza kuna nini kimetokea tena baada ya kutanzaziwa kuwa mgao wa umeme umekwisha.
  majibu niliyopata ni kuwa TANESCO hawajatangaza kusitisha kwa mgao wa umeme, sasa wana JF hizi taarifa tunazozipata vyombo vya habari wanazitoa wapi?

  Mtoa taarifa anapatikana No0784768586

  nawasilisha
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ujazo wa maji uliongezeka maradufu baada ya mvua kunyesha kwa hiyo mitambo inakwama kwama. Vuta subira, hili la mgao soon litakuwa ni historia tu.
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  TANESCo wanadaiwa kuwalipa mafisadi mapesa tele ilivyoamuriwa na mahakama fulani huko majuu - unategemea mgao uishe kweli?
   
 5. Wikiliki

  Wikiliki JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana Jf huku kwetu ninapokaa kila ikifika kumi na mbili jioni umeme unakatika unarudi saa sita usiku. Huu si mgao? Lile tangazo la Tanesco kuwa wamesitisha mgao ilikuwa ni uongo, kuendelea kutudanganya sisi wadanganyika.
   
 6. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  :target: tULIAMBIWA KUWA MGAO WA UMEME SASA KWISHA MBONA HAWAJI KUTOLEA MAELEZO KULIKONI...????
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi punde nimetoka kuongea na muhusika wa Tanesco na amenithibitishia kuwa mgao upo ila "wakubwa" wao bado hawajatangaza. Na naamini kuwa kuna mgao ila sielewi kwanini Watanzania wamekuwa makondoo kiasi hiki kwani ukipita mjini mchana ni makelele ya majenereta na sehemu kubwa ya mji mida ya usiku ipo gizani. Nadhani kuna haja ya vyama vya upinzani kulivalia njuga suala hili hasa ukizingatia Tanesco wamepandisha bei ya umeme wapinzani waulize umeme upi? Maana ni giza na makelel ya majenereta ndio yanayo sikika masikioni mwa wakaazi wa jiji.
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  habari kaka..... hapa ni JF store post hii ingeenda jukwaa la siasa au habari mchanganyiko naona ingepata response zaidi
   
 9. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Uko sawa kabisa.
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mgao wa Umeme mpaka SISI M iondoke madarakani!
   
 11. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,404
  Trophy Points: 280
  hapo umesema, usisahau kuopiga kura oct 31 2015
   
 12. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  [​IMG]
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Mbona nchi inaendeshwa kama na wale pwagu na pwaguzi? Juzi tu Ngeleja katangaza hakutakuwa tena na mgao wa umeme, hata wiki mbili hazijapita wanatangaza kwamba kuna mgao wa umeme!!!! Nini kinachojiri ndani ya Serikali iliyopo madarakani? Aaaaaaarrrrrrggggggghhhhhh!

  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~

  Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima

  Thursday, 23 December 2010
  Exuper Kachenje
  Mwananchi

  SHIRIKA la Umeme (Tanesco) jana lilitangaza mgawo mpya na mkubwa wa nishati hiyo ambao utavifanya viwanda, maduka, ofisi na makazi kukosa umeme kwa kati ya masaa sita hadi 12 kwa muda wa mwezi mzima.

  Tangazo hilo la mgawo ambalo limekuja katika kipindi ambacho mjadala wa jenereta za kampuni ya Dowans ukiwa umeibuka tena, linatarajiwa kuongeza gharama za maisha kutokana na ukweli kuwa viwanda vingi vitalazimika kutumia jenereta katika uzalishaji licha ya Tanesco kutangaza kuwa vitapewa umeme nyakati za mchana.

  Wananchi ambao kipato chao kinategemea biashara ya samaki, saluni, na vinywaji pia wataguswa na makali hayo moja kwa moja wakati mabenki, vituo vya mafuta, mahoteli na makampuni mengine ya kutoa huduma yatajikuta yakiingia gharama kubwa katika utendaji wao.

  Tangazo la Tanesco limetolewa wakati kukiwa na ahadi kemkem za kumaliza kabisa tatizo la mgawo wa umeme, huku Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikiwa imeliruhusu shirika hilo la umma kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 18.5.

  "Mgawo huu wa umeme umeshaanza kwenye mikoa yote na utadumu kwa majuma manne hadi katikati ya mwezi Januari mwakani," alisema meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alipoongea na waandishi jana.

  "Mgawo utahusisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa isipokuwa mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara."

  Kwa mujibu wa Masoud, mgawo wa sasa umetokana na upungufu wa umeme uliojitokeza baada ya moja ya visima vinavyozalisha gesi vya kampuni ya Pan African Energy, kuzimwa.

  Alisema kisima hicho kinachotoa gesi kimezimwa kwa ajili ya kukifanyia matengenezo ya kawaida, hivyo kusababisha upungufu wa megawati 40 za umeme zinazokwenda katika gridi ya taifa.

  Pan African Energy ni kampuni ambayo inachimba gesi hiyo eneo la Songo Songo, Kilwa na baadaye husafishwa na kusafirishwa na kampuni ya Songas ambayo huzalisha umeme wa megawati 180 eneo la Ubungo na kuiuzia Tanesco.

  Kwa mujibu wa makubaliano, Songas hutakiwa kuzalisha umeme kwa kiwango kilicho kwenye mkataba na ni jukumu la Tanesco kuutumia umeme huo wa gesi kulingana na mahitaji yake au kutoutumia. Tanesco huilipa Songas hata pale inapokuwa haitumii umeme wa kampuni hiyo.

  Badra alisema kuwa kiwango hicho cha upungufu wa umeme kinaweza kuongezeka hadi kufikia megawati 120 jambo alilosema likitokea, shirikma hilo litazidisha mgawo.

  "Wakati mwingine kunapokuwa na peak (matumizi yanakuwa makubwa), upungufu unaweza kufikia megawati 120. Ikitokea hivyo, kwa kuwa sasa tunategemea uzalishaji umeme kwa njia ya maji, itabidi nasi tuongeze mgawo," alisema Badra.

  Alieleza kuwa mgawo huo utaanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika baadhi ya maeneo huku maeneo yaliyopata umeme katika muda huo yakiukosa kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku mara tatu kwa wiki.

  Kwa mujibu wa Badra, ratiba ya mgawo huo zitatangazwa katika magazeti na vyombo vingine vya habari.

  Hata hivyo, alisema baadhi ya maeneo hayatakumbwa na mgawo huo akitaja baadhi kuwa ni hospitali, pampu za maji, migodi na viwandani ambako alisema vitakosa umeme usiku ili mchana viendelee kuzalisha.

  Alisema kuwa maeneo yanayopata umeme kutoka transoma ya Kipawa hawatakumbwa na mgawo huo, kutokana na kukamilika kwa matengenezo yake.

  "Transfoma ya Kipawa imeshatengemaa na hivyo kuanzia Desemba 23 (jana) haki ya kupata umeme katika maeneo yaliyoathirika kutokana na kuharibika kwa transfoma hiyo, itarejea kama kawaida na wateja wa maeneo hayo hawatakumbwa na mgawo huu tulioutangaza," alisema Badra.

  Baadhi ya maeneo yanayopata umeme kutoka transfoma hilo ni pamoja na Yombo Dovya, Tandika, Temeke, Chang'ombe, Chamazi, Tazara, Maji Matitu, Charambe, Keko na Uwanja wa Taifa.

  Akizungumzia siku kuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, Badra alisema Tanesco itajitahidi kuhakikisha wananchi wanasherehekea siku hizo bila kukosa umeme huku akiwaomba radhi kwa mgawo huo.

  Mgawo wa umeme, ambao ulizalisha kashfa kubwa ya Richmond ulipoibuka mwaka 2006, umeshaanza kuzoeleka kwa wananchi na ahadi za shirika hilo na wizara kugeuza tatizo hilo kuwa historia, sasa zinaonekana za kawaida.

  Machi 16 mwaka huu Tanesco ilitangaza mgawo wa umeme katika mikoa yote ya Tanzania Bara uliokuwa wa saa tano kila siku. Wakati mgawo huo ukiisha, Tanesco ilitangaza kuwa tatizo la umeme sasa litakuwa historia.

  Watanzania, ambao ni asilimia 12 tu wanaotumia huduma hiyo majumbani, pia walipata machungu ya mgawo wa umeme Oktoba mwaka uliopita ambapo walikosa huduma hiyo kwa saa 12 kwa siku.

  Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo Stephen Mabada, alitangaza mgawo huo akieleza kwamba Tanesco ililazimika kuanza mgawo huo kutokana na upungufu mkubwa wa uzalishaji umeme, uliosababishwa na kuharibika kwa mitambo minne kwenye vituo vya uzalishaji wa nishati hiyo.

  Mitambo iliyoharibika ilikuwa ni ya Kidatu, mkoani Morogoro, Kihansi (Iringa) na Pangani (Tanga) wakati jijini Dar es Salaam mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia wa Songas pia uliripotiwa kuharibika.

  Wakati huo, serikali iliamuru kuwashwa kwa mitambo inayozalisha umeme kwa kutumia mafuta ya IPTL licha ya kampuni hiyo na Tanesco kuwa kwenye mgogoro mkubwa ambao unashughulikiwa mahakamani.

  Matatizo makubwa ya umeme yaliibuka mwaka 2006 wakati nchi ilipokumbwa na janga kubwa la ukame na ikabidi serikali ichukue hatua za dharura kumaliza tatizo hilo.

  Lakini hatua hizo za dharura zikaishia kwenye kashfa kubwa ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme kwa kampuni ya Richmond Development LLC, ambayo ilidhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake kwenye mkataba.

  Baadaye mkataba huo ulirithishwa kwa kampuni ya Dowans Tanzania ambayo, licha ya kuchelewa, ilileta nchini mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 120.

  Lakini mwaka 2008 Tanesco ilikatisha mkataba huo mwaka mmoja kabla ya kumalizika, ikidai kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ilikiukwa wakati wa kuingia mkataba huo, lakini ikaahidi kuwa ina uwezo wa kuzalisha umeme bila ya kutegemea jenereta hizo.

  Uamuzi huo uliifanya Dowans kufungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), ikidai kuwa taratibu hazikufuatwa wakati wa kuvunja mkataba huo.

  Mwaka mmoja baadaye Tanesco ikaibuka na hoja ya kutaka kuinunua mitambo hiyo ya Dowans, ikidai kuwa nchi ilikuwa hatarini kuingia kwenye tatizo kubwa la umeme na kwamba isingekuwa rahisi kununua mitambo mingine kabla ya tatizo hilo kuanza.

  Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na Kamati ya Madini na Nishati ambayo ilieleza kuwa kununua mitambo hiyo mitumba ni kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma, kitu kilichomfanya mkurugenzi wa Tanesco wa wakati huo, Dk Idris Rashid kutoa tamko kuwa iwapo nchi itaingia gizani, asilaumiwe.

  Mapema mwezi huu, ICC) ilitoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Dowans na kuiamuru Tanesco kuilipa kampuni hiyo binafsi fidia ya Sh185 bilioni.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tunashindwa na Somalia nchi ambayo haina serikali miaka nenda rudi. Wana umeme wa hakika. What a shame!
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  wafanye wafanyalo wao ndio waloshika mpini, ila wakae wakijua kuwa watanzania wamechoka
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Hakuna Serikali huko kuna Utawala wa nguvu tu. Wezi Ulaji rushwa na Ufisadi ndio umezidi hiyo Nchi yetu inakokwenda huko ni Kaburini
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hizi ni sababu za mgao kwenye majira manne ya mwaka

  Masika
  Songas wanafanya matengenezo
  Kiangazi Mabwawa yamepungukiwa maji
  VULI- ukarabti wa kawaida wa grid ya taifa
  Kipupwe- Malizia.........

  Arent these justifiable reasons for power rationing through out the year. Naamin nyuma ya pazi ni justication ya Dowans

  siku dowans wakiingia mkataba wa kutukamua tena ndio mgao utaisha

  teh tehteh
  Imebidi nicheke. the way anavyosema utadhani hiyo mikoa hata kabla ya mgao haina matatizo. infact hiyo mikoa ina migao ya kudumu

  mshirika zaidi ya matatu yanazalisha umeme lakini bado mgao. Huu umemewa mafungu huu sijui utatufikisha wapi
   
 18. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Leaves me speechless. Stunned.
   
 19. c

  chamajani JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Ngeleja ameshawahi ugua wendawazimu au!!!!? kwani si a-resign tu, ivi haoni kuwa hiyo Wizara imemshinda? Shame on her:angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry:
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Habari hizi zinachanganya ubongo.....................Majira yasema....................Krismasi gizani............................Tanesco yatangaza magawo wa umme nchi nzima...................................................

  lakini kwenye gazeti la Mtanzania lalonga...............................mgao hautakuwepo kesho siku ya Krismasi...............................sasa sijui yupi asema kweli..........................................
   
Loading...