TANESCO yashitukia mkataba wa Songas | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO yashitukia mkataba wa Songas

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 25, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tuesday, 24 May 2011 20:08 newsroom


  NA MOHAMMED ISSA

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema mkataba kati yake na kampuni ya gesi ya Songas una utata na unaweza kulisababishia hasara kubwa. TANESCO imesema mitambo ya Songas haiwezi kuzalisha megawati 160 kwa sasa, kwa kuwa haina uwezo wa kutumia gesi na mafuta kuiendesha. Kwa mujibu wa TANESCO, inahitaji sh. trilioni 1.3 kwa ajili ya marekebisho ya mitambo na imekuwa ikipoteza sh. bilioni 51 kwa mwaka kwenye mikoa ambayo haijaunganishwa na gridi ya taifa. Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi William Mhando, alisema hayo jana katika ofisi ndogo za Bunge, mjini Dar es Salaam, mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Mhando alisema mkataba wa Songas ni lazima uangaliwe upya kabla haujaleta madhara. Alisema kampuni ya Pan Africa ambayo hivi sasa imezima mitambo yake kwa ajili ya kuifanyia marekebisho makubwa imekiuka mkataba. Kwa mujibu wa Mhando, kampuni hiyo inapaswa kuzima mitambo kila baada ya miaka minne lakini imekaa hadi miaka saba haijafanya ukarabati.[​IMG]


  Alisema kuzimwa kwa mitambo hiyo kumeongeza makali ya mgawo wa umeme, ambapo hivi sasa ni saa 16 badala ya saa tano. Mhando alisema hali ya upatikanaji umeme bado itakuwa ngumu, na makali ya mgawo yanaweza kuongezeka hadi Julai, mwaka huu. Hata hivyo, alisema hatua kadhaa zimechukuliwa kwa ajili ya mchakato wa ukodishaji mitambo ya megawati 260. Alisema zabuni imeshatangazwa na kampuni 15 zimejitokeza, ambapo moja imekidhi vigezo vya kuzalisha megawati 70. Mtambo huo wa kukodi utafungwa Tanga, eneo la Majani Mapana. Mhando alisema TANESCO inaendelea kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha tatizo la umeme linapatiwa ufumbuzi, ambapo mazungumzo yanaendelea na kampuni ya Marekani kwa ajili ya kupata megawati 112. Naye Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema uzalishaji na ununuzi wa mitambo ya umeme iachiwe TANESCO bila ya kuingiliwa na serikali au wanasiasa. Alisema serikali inaendelea na juhudi za kulitafutia dawa tatizo la mgawo wa umeme, ambalo limekuwa gumzo nchini. Alisema wanaobeza dhamira hiyo ya serikali hawana nia njema na taifa.

  Ngeleja alisema juhudi za makusudi zinafanyika kukamilisha dhamira ya serikali na wanatarajia kuongeza megawati 1,000 kwenye gridi ya taifa ifikapo mwakani. Akizungumzia upatikanaji umeme kwenye migodi nchini, Ngeleja alisema inatumia megawati 59.2 zinazozalishwa na gridi ya taifa. Waziri Ngeleja alisema wakati umefika kwa TANESCO kuangalia uwezekano wa kununua mitambo yake badala ya kukodi kwa gharama kubwa. Alisema serikali inaendelea kupokea maoni na ushauri wa Kamati ya Nishati na Madini kuhusu mustakabali wa TANESCO. Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti January Makamba, iliishauri TANESCO kuchukua hatua za makusudi kumaliza tatizo la umeme nchini. Wajumbe wa kamati hiyo waliwaomba wanasiasa kuacha kuzungumzia suala la DOWANS, badala yake waangalie uwezekano wa kuupatia ufumbuzi mgawo wa umeme.

  Last Updated ( Tuesday, 24 May 2011 20:20 )
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Huyu mbona midomo yake imepinda? Ana tatizo gani kwani....
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  haya si ndio mambo aliyosema IDRISSA RASHID akaambiwa wanasiasa kuingilia TANESCO muhimu
   
 5. T

  Taso JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Unaweza kusema "umeshtukia" proposal ya mkataba, huwezi kushtukia mkataba ambao umeshaingia mkenge. Waandishi wetu mbona hawajaenda shule?

  TANESCO inawezaje kusema mkataba wake na Songas una utata, sio wao wenyewe waliosaini mkataba?

  Legal department ya TANESCO bado ina matatizo hata baada ya kum demote yule mama aliye preside wakati wa Dowans.
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Taso hapo ni uelewa tuu mkuu wewe may be ni learned brother na unajua maana ya proposal na mkataba halisi
   
Loading...