TANESCO yanunua mitambo ya megawati 160 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO yanunua mitambo ya megawati 160

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Peter Mwenda

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 100 utakaotumia gesi katika Kituo cha Ubungo na
  mwingine utakalozalisha megawati 60 na kutumia mafuta mazito katika mtaa wa Nyakato mkoani Mwanza.

  Mhandisi Mkuu wa Miradi ya Uzalishaji Umeme TANESCO, Bw. Simon Jilima aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa mitambo hiyo itaanza kuzalisha umeme kuanzia Mei mwakani baada ya kukamilika kufungwa.

  Alisema ujenzi wa mitambo hiyo mitatu itapunguza upungufu wa mahitaji ya umeme katika gridi ya Taifa ambayo kwa sasa ni megawati 260 kwa nchi nzima.

  "Mitambo hiyo nimekwenda kuihakikisha mwenyewe kuwa inafanya kazi baada ya kufungwa nchini Sweden na kuwashwa ambako ilifanya kazi kwa ufasaha," alisema Bw. Jilima.

  Alisema ujenzi wa mitambo hiyo unatokana na fedha za mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Norway ambayo ni imetoa asilimia 85 ya fedha hizo na asilimia 15 ni fedha zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

  "Hii ni mitambo mikubwa ambayo inafika kontena zaidi ya 100 hivyo kutokana na ufinyu wa eneo letu hapa Ubungo ni mizigo mingi ambayo imegharimu fedha nyingi, thamani ya mitambo yote ni dola za Marekani 124,895,988 pamoja na kodi," alisema Bw. Jilima.

  Naye Meneja Mawasiliano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud alisema kutokana na ongezeko la mahitaji ya umeme katika gridi ya Taifa, lililosababisha upungufu wa umeme, TANESCO limekuwa likifanya jitihada mbalimbali za kupambana na tatizo hilo.
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  gesi yenyewe wanayo? Ngoja ije ioze hapa
   
 3. B

  Bwana bonny Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hadi pale tutakapoona mgao haupo ndo tutaamini, siasa kila mahala siku hizi utekelezaji No!
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wezi tupu...
   
 5. mtaratibuuuuuu

  mtaratibuuuuuu Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Next Richmond..............
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  TANESCO kwa longo longo hakuna wa kuwashinda.tunataka mgao umalizike kabisa.
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi hii ubungo bado inaweza kufungwa mutambo mingine, Mbunge wa ubungo hebu angalia suala hili isije ikaharibu mazingira ya ubungo. halafu inaonekana katika upanuzi wa barbara hii mitambo isije ikakumbwa.:pound:Kwanini isiende Mkuranga kwenye gesi?:mod:
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Tanesco as Tanesco hawana uwezo wa kumaliza mgao.

  Bila steigler kuanza kuzalisha, mgao hautaisha.
   
 9. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Stiegler's gorge isn't sole solution, Ruhudji is the nearest from the EA done and way cheaper, funders for Stiegler's have pulled out due to culmination of issues

  Its the government that is supposed to invite grants and syndicate loans for that purpose , Uganda under Museveni is completing Bujagali project whilst a second 750MW is now starting

  Zambia govt is now expanding Kafue Gorge which has 900MW to add 750 ,

  Kenya has imported 3 gas plants under KenGen here the Kikwete govt still sits on its big slumber waiting for mother nature to do magic and by september vuli isipoanza Mtera will have to be closed then loadshedding will know, no mercy!
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Carry on kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya chama tawala
   
 11. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe saimoni na wenzako sijui niwaite machizi. Hivi hapo ubungo hamuuoni huo msongamano wa nyumba na vitu vingine? kwani msiupeleke hata huko chanika au picha ya ndege au bagamoyo au kimbiji? Njie mnataka hayo mamitambo yaje yatulipukie ndo mfurahi> Tumeyaona ya mbagala na ngongolamboto. yahapo ubungo yatakujakuwa funga kazi nyie endeleeni tu. Mbona tanzania inaaridhi kubwa tu ya kutosha ambayo haitumiki?
   
Loading...