TANESCO wasitisha mgawo wa umeme

Nilichokupendea Ngeleja ni pale ulipoongea kwa msisitizo kua unataka Tanesco wawe wanatoa taarifa endapo kutakua na Mgao wa umeme kwa wananchi na sio kukaa kimya! BRAVO SANA!:whoo:

Taarifa ya mgao wakati kesha sema mgao sasa basi??
 
Source: TBC1

mgao wa Umeme umekwisha na hautarudia tena. Amelishuhulikia tatizo kisha akatutaarifu. Mawaziri wengine walioingia kwa mbwembwe vipi?

Tanesco wasitisha mgawo wa umeme

Wakuu,

nimerudia hii thread leo kwa sababu nilivyoipost kuna watu waliosema ngeleja alikuwa anafanya usanii, mimi sikuwaamini kwa sababu mbwembwe alizoonesha kwenye TV nilidhani kama angekuwa anasema uongo basi alikuwa anaandika first draft ya barua yake ya kujiuzulu.

leo tunatangaziwa kwamba mgao umerudi, ingawa ulikuwepo hata baada ya ngeleja kutangaza kwamba umekwisha. Pia tunaambiwa kwmba bei ya umeme itapanda kuanzia January wakati yeye siku hiyo hiyo alikuwa ametangaza kwamba umeme Tz utakuwa ni historia kutokana na miradi mikubwa ambayo serikali ya JK imeshaanza kutekeleza.

kwa maneno ya ngeleja mwenywewe aliseam. "watanzania watakuja kumkumbuka Kikwete kwa kumaliza tatizo la umeme TZ kwa vizazi vijavyo"

Samahani nimeandika hii post kidogo nimekasirika sana. Kumbe serikali inatudharau kiwango hiki? Kwamba wanaweza wakaamua tu kutudanganya wakijua fika kwamba wanatudanganya. Na sasa wananchi hawakumbuki tena maneno haya ya Ngeleja ambayo hata hayajamaliza wiki mbili.

Na bado yuko madarakani na wananchi wanaendelea kukubali mgao kwa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na taarifa za kupanda gharama za umeme!!!1
 
Just spoken to my friends in Mwanza wapo gizani kama kawa..... au Dar ndio Tanzania......

Kijitonyama dar es salaam... wiki ya pili sasa tunakatiwa asubui unarudishwa jioni..ukipiga Tanesco wanasema mgao....sasa huo mgao umeisha vp....tuna viongozi ama viinimacho
 
Hivi wanavyoleta wawekezaji wanawaambia power is available ama waje na majenereta yao? Ha ha ha yaani hii nchi niyakuisikitikia....tushakufa tunasubiri kudondoka...
 
Just spoken to my friends in Mwanza wapo gizani kama kawa..... au Dar ndio Tanzania......

Kijitonyama dar es salaam... wiki ya pili sasa tunakatiwa asubui unarudishwa jioni..ukipiga Tanesco wanasema mgao....sasa huo mgao umeisha vp....tuna viongozi ama viinimacho
 
Back
Top Bottom