TANESCO wasitisha mgawo wa umeme

Mbona hii habari siyo ya kuaminika sana? Iweje juzi tu alipoambiwa kuwa Tanesco wanadaiwa Tshs.185Bln baada ya kushindwa kesi alipamba moto na kwaambia Tanesco wajieleze, iweje leo yeye atangeze mgao basi? Kwanini asingewaacha Tanesco wenyewe watangaze hayo mafanikio? halafu umeme anaouzungumzia ni wa kiwango au ndiyo huo wa kupanda na kushuka unaosababisha vifaa kuungua majumbani na maofisini?? Is this statement truly from a Minister?? I doubt it? Kama ni kweli basi nimpe tu pole Waziri wetu.
 
Ngereja nia mwanasiasa kijana anaye tumia mbinu za kizamani, penye mafanikio anajidai ni juhudi zake, penye kushindwa anajitoa na kusakizia wengine! Huku ni kukwepa uwajibikaji-awe kama Mzee wa Kiraracha anasaka mwenyewe gongo live migombani!
 
wakuu nisaidieni kidogo kasaidia kwakufanya lipi?
kwa nilichosikia/kuona nikuwa kwa kuwa mvua zimenyeshe sehemu zisizokuwa na tatizo la ubovu wa transformer ndio tatizo limeahirishwa kwa wenyematizo wasubirie siku 8 za katibu mkuu zitimie ili mafundi wamalize kutengeneza generator/transformer.
 
KAULI YA NGELEJA, LABDA AWE AMEOKOKA TANGU JANA:

Kwa kauli hii nzito kwamba kukatwa katwa umeme HAUTORUDIA TENA, mimi bado nalitilia wasiwasi mkubwa sana tu.

Labda mtoa kauli hiyo asiwe yule yule William Ngeleja ALIEKUA KARANI WAKE Rostam Aziz ghorofa ya kwanza pale makutano ya barabara ya Samora iliko juu ya Ocean Sandles ya sasa hivi. Tangu lini RA alimuondoa kwenye payroll yake kama si kumbadilishia tu seksheni tu ya kazi kutoka Dar kwenda Bungeni Dodoma???

Hii kauli inaweza tu ikawa ni ya kweli kama bosi wake huyo kamwambia ya kwamba BASI ITAKUA NOMA kwa jinsi Umma wa Tanzania tulivyoghadhabika akawashe tu umeme TANESCO, basi pengine huenda ikawa ni kweli kwamba hali ya KUTUYUMBISHA NA NISHATI hiyo safari hii itakoma.

Lakini sasa wale aliowapa leseni za dharura kuleta MIJENERETA KULE KARIAKOO sasa ndio tuseme imekula kwao au kamtambo mojawapo KATALIPUKA HAPO KATIKATI KATIKATI ili aliowachangisha Iddi Azan Zungu wakarejeshe fedha zao???

Jamaae, kwa wale mnaofahamu vema ule mchezo mchafu enzi za Ndolanga kwenye medani ya soka, hivyo vivyo ndivyo ilivyo hata kwa uwanja wetu wa siasa kwa sasa kule bungeni Dodoma.

Kama ambavyo ilivyowahi kutokea huko nyuma katika kwamba katika TIMU ZETU za SIMBA na YANGA ambapo kila TAJIRI anao wachezaji wake binafsi ambao hata KLABU haina nafasi kuwasumbuasumbua na pia inayomfanya akakohoe apendavyo kwenye klabu na hivyo vivyo ilivyo kwa Baraza la Mawaziri pia unapaswa ukaulize tu kwamba EL anao wangapi, RA kafanikiwa wangapi na kadhalika. Nako anapopewa Wizara kwa kwa mapendekezo ya mfadhili ambaye anajichagulia maeneo nyeti ya kuweza kumnufaisha kibiashara mbele ya safari na wala si kwa maslahi ya Wa-Tanzania.

Mpaka hapo sasa kwanza tujiulize Rostam Azizi atakua nao mawaziri wangapi, Manji kawaweka kazini wangapi na kitu kama hicho halafu sasa ndio turudi kusikiliza maumivu yake taratibu mpaka 2015!!!

Na wabunge ndio usiseme, wabunge wa wananchi ni haba sana hata ndani ya CCM sawa sawa na jinsi unavyoona ndani ya CHADEMA na vyama vyetu vingine vidogo vidogo, wengine waliowengi ni wabunge walionunuliwa nafasi hizo kwa ajili tu ya kutetea MASLAHI BINAFSI. Na huo ndio ukweli unaoelezea sababu ambazo siku zote zinafanya HOJA ZENYE MASLAHI BINAFSI kupita bila vikwazo wakati zile zenye MASLAHI YETU KAMA TAIFA hutweta mno kama si kuangushwa kabisa.

Kama haya bado hayakuingii vizuri masikioni basi ngoja mwezi Februari 2011 kule bungeni ndipo utakapogundua kwamba hata zile bilioni zetu 60/- (kodi zetu) kamwe hazikustahili kutumika
kwa jina la kuandalia kitu UCHAGUZI MKUU.

Hata hivyo, hatuwezi kusema sana labda kilicho kule kule walikobahatika kujipatia UJASIRI WA KUTETEA MASLAHI YA TAIFA akina Ole Sendeka, Mama Kilango, S-Square People's Power, Mwakyembe, Mtoto wa Mkulima,Dr Shein Mtetezi wa Raia kwa kutumia Silaha Hatari ya 'Upole', 'Yohana M-Batizaji wa Mafisadi' kwa kutumia moto (pombe Magufuli) na wengine wachache wao, pengine huenda akina Ngeleja Mawaziri na Ngeleja Wabunge nao wameanza kuzinduka usingizini!! You never know!!

Ngeleja, tunakusubiri njia panda na hiyo kauli nzito juu ya umeme!! Vile vile tunakusubiri kule kule tulikohadaika kuliko chochote dunioani - madini yetu, michanga yetu, na uwaziji juu ya maslahi yetu huko.
 
Unaumwa wewe, weka hizo risiti hapa, nyie ndo mtakuwa mnawekewa umeme wa wizi. Mwizi mkubwa wewe.
Nimelipa 1.4 serive line ya single phase
Shetani one service line single phase without nguzo is NOT 1.4 I dare you!
 
Hivi kweli wanaposema maji yamejaa wanamaanisha nini wakati mvua yenyewe imeanza kunyesha jana?
 



It has become so predictable. This thing we call ‘power rationing.’ We had it in 2006, 2007 and 2008. It is here in 2009. If the yearly trend continues then we shall surely experience it in 2010.

If we have forgotten the past then we only have to glance at the dates of the following front page news stories from The Citizen to get a glimpse of how this power rationing is such a vicious cycle: “‘Tanzania 2006: Power’ Crisis dominated headlines” (29 December 2006); “Another power crisis as Songas turbines collapse” (25 September 2008); “Power Crisis: Tough times ahead – No solution in sight as sabotage suggestions angers Tanesco boss” (13 October 2009).

SOMA ZAIDI HAPA: UDADISI: Rethinking in Action: Waiting for Power: Citizens’ Plight during Energy Crises - As it was in 2008 and 2009 so it is in 2010!
 
Shetani one service line single phase without nguzo is NOT 1.4 I dare you!

Jamani achaneni na hilo shetani zuzu,limeshaingizwa mjini kwa kuuziwa kitu cha laki 4 kwa millioni na nusu,hii ndo bondo dalisalama ukilemaa umeachwa feli
 
Kama kuna mawaziri ambao hawaaminiki basi ni hawa ambao wapo ktk awamu ya jk.wamekuwa wakidanganya mara kwa mara na kuumbuka.
Kama hamuamini subirini muone kama mgao utaisha.
Binafsi sina imani na ngeleja na sielewi jk anampendea kitu gani.
 
Nilichokupendea Ngeleja ni pale ulipoongea kwa msisitizo kua unataka Tanesco wawe wanatoa taarifa endapo kutakua na Mgao wa umeme kwa wananchi na sio kukaa kimya! BRAVO SANA!:whoo:
 
jana kwenye TBC na star tv Ngeleja si ndio yule alikuwa anaongea kama mlevi wa Gongo? Hakusema lolote eti mgao umekwisha kumbe wapi ?waulizeni Tanesco bana acheni kushabikia Mawaziri upepo
 
Jamani jana nikiwa naangalia TBC taarifa ya habari tumesikia kua Tanesco wanasema kuanzia jana WAMESITISHA MGAO WA UMEME! Naomba msaada wenu kuhusu hili neno KUSITISHA! inamaana kukatika umeme mara kwa mara ilikua ni makusudi? kwahiyo wamesitisha kukatika kwa umeme? Naomba wajameni mnipe maana ya kusitisha.:angry:
 
hii ndio tanzania nchi ya watu wadogoooo ukitaka umeme nunua solaaaa...!!! dats it bro tannesco wana mamlaka yao wana amua watakavyo tu na serikali yetu ilivyo ovyo wanakaa kimyaaa.. ipo cku yapo tu
 
Umeme umekuwa kama kipindupindu. Visababishi vya kipindupindu vinajulikana, namna ya kuzuia inajulikana, namna ya kutibu inajulikana, madhara kwa binadamu na uchumi yanajulikana.

Inajulikana majira ya mwaka ambapo kipindupindu lazima kilipuke iwapo tahadhari hazikuchukuliwa. Kikishatokea watendaji na wanasiasa wote bize kutibu na kukilaani na kuahidi hatua zinachukuliwa ili kisitokee tena. Lakini wapi, kila mwaka kinatokea, serikali ile ile chama kile kile.

Historia ya mgao wa Umeme tz imefanana kabisa na ile ya kipindupindu. Je, adha na kero nyingine zinazoumiza uhai wa binadamu na uchumi wetu vimeshughulikiwaje? Serikali ile ile chama kile kile na wakati mwingine wahusika wale wale.

Tafakari, jadili kwa muktadha wa uhuru (uhujumu) wa miaka 49.
 
Hakuna cha kumpongeza bse JK alishai sema mgao kuwa historia sasa tumpongze kwa lipi la maana apo
 
Nitampongeza baada ya mwaka na nusu kuisha.
Siwezi kumpa hongera kwa kutimiza wajibu wake. apewe hongera kwa kwenda beyond na majukumu kwa manufaa ya umma
 
Nitampongeza baada ya mwaka na nusu kuisha.
Siwezi kumpa hongera kwa kutimiza wajibu wake. apewe hongera kwa kwenda beyond na majukumu kwa manufaa ya umma

Apongezwe baada ya miaka 5 mkuu asije litia tembo maji
 
Back
Top Bottom