Tanesco ni kama kinyonga........mnatia kichefu chefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco ni kama kinyonga........mnatia kichefu chefu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by fikirini, Jun 24, 2011.

 1. fikirini

  fikirini Senior Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana Jf asalamaleykum. Hawa TANESCO kila siku mabadiliko tu yasiyo na tija bali ni ya umahiri wa kubooresha makali ya umeme, hakuna kipya....hata kinyonga japo hubadilika rangi ila ni kwa malengo na tija pia ni kwa manufaa ya maisha yake hasa pale hatari inapokuwa mbele yake. Kwa TANESCO Hakuna ubunifu, kweli hiki ni kichefuchefu. Hii inatokana na habari za kusikitisha kuwa shirika hilo limetangaza mgawo mkubwa wa umeme usio na kikomo, utakaokuwa kwa saa 10, siku saba kwa wiki nzima.Maafisa wa shirika hilo na Wizara ya Nishati na Madini wamesema mgawo huo umetokana na upungufu wa maji katika bwawa la Mtera na transfoma zake kuzalisha umeme mdogo kuliko mahitaji.Kwa mujibu wa tangazo la ratiba ya mgao huo lililotolewa na Tanesco jana, mgao huo utakuwa wa kati ya saa sita hadi 10 kwa siku ambapo maeneo yatabadilishana muda wa mgao. Hata hivyo, tangazo hilo la Tanesco limekuja wakati maeneo mengi nchini yakiwa na mgawo wa muda mrefu wakinyemela na ambao unachukua muda wa saa zaidi ya zilizotangazwa jana na shirika hilo hali inayosababisha malalamiko kwa wananchi na kupoteza imani na serikali iliyopo madarakani.

  Sasa hii serikali na shirika lake, wanaona fahari gani kila siku kuwa wataalam tu wa kutoa ratiba za mgao, hivi utoaji wa huduma za umeme hatuwezi tukafanya kama makampuni ya simu.? Turuhusu ushindani katika sekta hii wadau.....alafu ndo tunaambiwa tudumishe amani. Ni amani gani hii ya kuumizana? Kutojaliana? Huu ni unafiki wa viongozi wetu....nini hatima ya kilio hiki wana JF?
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Si bora ingekuwa massa kumi. Mtaani kwetu ni masaa 24 hakuna umeme.
   
 3. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wa Tz mpaka tupigane ndio tutaheshimiana.
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  waongo wanataka kuingia makataba mwingine,hiyo ni danganya toto,subilini mtaona kwani ule mkataba na symbion si waliingia kwa staili ya mgawo?


  karibuni Welcome to the IHAM Solar Suppliers
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,050
  Likes Received: 3,081
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa nimesikia wanataka kuirejesha AGRECO ilete umeme August,yaani hii nchi ni ya raha sana.,huwezi kuamini kule Ruvuma wanasema mafuta yameisha wiki nzima wako gizani,juzi tuliambiwa maji machache,mvua zikanyesha badala yake wakasema sasa ni ubungo mitambo ya gesi inasafishwa,wakasema Symbion ndo suruhisho,sasa wanasema maji yameisha mtera suruhisho ni kurudi AGRECO

  Tusipokuwa makini yale makampuni ya nyuma yatarudi upya kwa majina mapya,Network Group Solution,Richmond n.k,hii ni ajabu sana sahivi tunapigwa mgao mkubwa tofauti na mda wowote huko nyuma,huu wa sahvi ni funga kazi

  Let's awake,demonstrations could make these people change the world,tuingie barabarani vinginevyo tunapewa adithi za abunuwasi
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Nipo jirani sasa hivi na bwana Eng Mhando naona anaweweseka tu,nimemwambia aangalie jf jinsi watz wanavyochukizwa na shikirika hili mfilisi!!
   
 7. duda

  duda Senior Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAICHUKIA SAN HII TANESCO, Just imagine saivi tunalipia huo umeme, je! ingekuwa vp kama ungekuwa wa bure? si tungelala na giza miezi hata sita???????// I hate this TANESCO
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,356
  Trophy Points: 280
  Me too!!huo mgawo ni kwamba umetangazwa tu, lakin kama kuwepo mbona upo tu muda mrefu.kijitonyama toka walivyokata juzi usiku hawajarudisha mpaka leo
   
Loading...