TANESCO Na Wataalamu wa IT, Tusaidieni!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,240
4,263
Kilio na ombi hili hiki navipeleka kwa shirika la TANESCO.

Mimi natumia umeme wa LUKU na ninasafiri sana.

Wakati mwingine safari hizi hunichukua hata mwezi mzima kabla ya kurudi nyumbani.

Katika kipindi hicho umeme kwenye luku unaisha mpaka nirudi nyumbani kununua.

Je TANESCO haiwezi kutanua teknolojia yake ili nikiwa safarini niweze kununua umeme kwa ajili ya nyumbani?

Mathlani nyumbani kwangu ni Moshi na nipo Mwanza kikazi na ninataka ninunue umeme kwa ajili ya nyumbani Moshi.

Nina hakika hii huduma haipo ila ningependa sana TANESCO waianzishe kurahisisha maisha.
 
Last edited by a moderator:
SHIEKA unaweza kununua luku popote tanzania, kwa kutumia maxmalipo, luku vendor,mashirika ya simu, na ukipata token ukituma kwa sms namba unapata umeme. Siyo hivyo tuu waweza lipia bili ile ya mita za convention popote Tanzania.
 
Mkuu hii mbona rahisi labda niwe sijakuelewa.

Unachotakiwa kufanya ni kuwa na no za luku yako.unanunua umeme kwa mpesa, tigopesa, airtelmoney, simbanking, nmbmobile.kisha ukitumiwa token unatuma nyumbani hizo no kama sms ya kawaida kwa yeyote aliyepo nyumbani anaziingiza.
 
Mbona inawezekana!! Kambi popote, ni wewe na namba ya mita yako, bhaaas!
Au unamaanisha ununue popote kisha iingie automatically?
 
kama sikosei, ni alikuwa anataka kusema kuwa awe na uwezo wa kununua umeme popote nchini na uwezo wa kuingiza kwenye mita yake moja kwa moja kwenye simu yake bila kupitia kutuma zile token kwa mtu ili akaingize. sasa naona hii ni wazo zuri kwa TANESCO kupewa
 
Anamaanisha kununua umeme na kuuingiza kwenye luku bila kuwa nyumbani.
kama sikosei, ni alikuwa anataka kusema kuwa awe na uwezo wa kununua umeme popote nchini na uwezo wa kuingiza kwenye mita yake moja kwa moja kwenye simu yake bila kupitia kutuma zile token kwa mtu ili akaingize. sasa naona hii ni wazo zuri kwa TANESCO kupewa
Exactly
SHIEKA unaweza kununua luku popote tanzania, kwa kutumia maxmalipo, luku vendor,mashirika ya simu, na ukipata token ukituma kwa sms namba unapata umeme. Siyo hivyo tuu waweza lipia bili ile ya mita za convention popote Tanzania.
Yeye anaongelea kuhusu kuingiza hizo tokken kwenye luku bila kuigusa
 
Yaani kwa ufupi, kuingiza umeme kwenye LUKU iwe kama unavyonunua salio la muda wa maongezi linarushwa moja kwa moja kwenye simu yako.

Au kwa mfano rahisi zaidi kama unavyoweka pesa kwenye M-pesa au tigopesa unapoenda kwa wakala. Vivyo hivyo iwe ukienda kwenye kituo cha kununua umeme unalipa pesa na kuwapa meter namba yako kisha units zinajiongeza zenyewe huko nyumbani.

Naomba nirekebishwe kama nimeelewa tofauti na alichomaanisha SHIEKA
 
Nimemuelewa, ni wazo zuri!

Hata mimi nimelipenda lakini kuna vitu vingi sana vya kuzingatia kabla ya kutekeleza hilo wazo, kwanza TANESCO watafaidika vipi na huo uwekezaji wa miundo mbinu? Faida mojawapo ni ile ya wateja kupata urahisi wa kununua umeme na kuingia moja kwa moja kwenye LUKU, je hiyo pekee linatosha?

Kuna haja ya wataalam wa TANESCO kulifanyia kazi hili wazo kuona watapata faida gani (mara nyingine kumrahisishia mtumiaji mambo ni sababu tosha ya kuboresha mfumo au kuwekeza kwenye miundo mbinu). Ikumbukwe TANESCO hawapo kwenye ushindani mkubwa wa kibiashara kiasi cha kugombea wateja.
 
Mkuu hii mbona rahisi labda niwe sijakuelewa.

Unachotakiwa kufanya ni kuwa na no za luku yako.unanunua umeme kwa mpesa, tigopesa, airtelmoney, simbanking, nmbmobile.kisha ukitumiwa token unatuma nyumbani hizo no kama sms ya kawaida kwa yeyote aliyepo nyumbani anaziingiza.

Atazituma vipi nyumbani wakati hayupo? Soma na uelewe.
 
Tanesco wezi sana. Unaweza kununua unit mia wao wakaweka unit hamsini ni afadhali unumue upate token uweke na uhakikishe.
 
Tanesco wezi sana. Unaweza kununua unit mia wao wakaweka unit hamsini ni afadhali unumue upate token uweke na uhakikishe.
can you provide proof? Yaani ununue unit mia wakupe hamsini? Sidhani kama watafanya blunder kama hii. Check na service provider wako aliyekuwezesha. Possibly tatizo lipo hapo
 
Kilio na ombi hili hiki navipeleka kwa shirika la TANESCO.

Mimi natumia umeme wa LUKU na ninasafiri sana.

Wakati mwingine safari hizi hunichukua hata mwezi mzima kabla ya kurudi nyumbani.

Katika kipindi hicho umeme kwenye luku unaisha mpaka nirudi nyumbani kununua.

Je TANESCO haiwezi kutanua teknolojia yake ili nikiwa safarini niweze kununua umeme kwa ajili ya nyumbani?

Mathlani nyumbani kwangu ni Moshi na nipo Mwanza kikazi na ninataka ninunue umeme kwa ajili ya nyumbani Moshi.

Nina hakika hii huduma haipo ila ningependa sana TANESCO waianzishe kurahisisha maisha.
Inawekana kabisa hata kwa simu kupitia huduma za Kama tigopesa
 
Wakuu,
Mtanisamehe kama nitakua nje ya mada ila nimepata taarifa kua Tanesco wametoa mita mpya za Luku huko ukanda wa Pwani ambazo zimekua ni msaada mkubwa kwa wenye nyumba waliokua na wapangaji ambao ni wasumbufu katika kununua Umeme pindi unapoisha.

Kunakua na mita kubwa kama kawaida halafu kila Chumba kinakua na mita ndogo(zinazotumika kujazia umeme kwa wale ambao mita zao za Luku zimefungwa kwenye Nguzo) ambayo kila mtu anaweka Umeme wa kiasi chochote cha Pesa kulingana na matumizi yake na Unit zake zikiisha Umeme unakata kwenye Chumba husika je kwa mlioko Dar mshaziona hizo Mita?

Swali langu kwa wahusika wa Tanesco hizo Mita zitafika lini huku Mikoani?
 
mtoa mada hilo suala nimekua nikilitafakari kitambo sana..na nimeona inawezekana...ila itawezekana tu kama kama hizi mita za luku za kisasa zitabadilishwa na kufungwa zingine kwakua hizi si smartmeters kutosha kufanya hilo..

kiteknolojia inawezekana mtu unapoenda kununua luku kwa vendor,mara umalizapo malipo akaunti yako inajaziwa salio papo hapo..kwa kutumia ama media ya cable zao umeme au zile meter zifungwe simcards ziwasiliane na server yao iliyopo makao makuu..

ni kama vile zile mita za AMR za tanesco...wanaweza kusoma/kukukatia au kukufungulia umeme wakiwa ofisini kwao bila kufika site..
 
Back
Top Bottom