TANESCO Mwanza inahitaji kufumuliwa kuendana na Sera ya Viwanda

LENDEYSON

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
2,980
2,000
Maeneo mengi ya Jiji la Mwanza Mgao wa Umeme ni mkali haswa! Tumebaki tunajiuliza, hawa wapo tayari kumsaidia Mh. Rais kukamilisha ndoto yake ya Tanzania ya Viwanda? Viwanda hivi vinahitaji Nishati muda Wote, lakini huwezi kuamini imeshakuwa ni kila Leo Umeme kukatika kwa masaa mengi tu, huo uzalishaji mnataka utumie biogas?
Maeneo ya Mkolani,( ambapo Kuna substation), Buhongwa, na Nyegezi kwa uchache, hayana Umeme hadi muda huu, Mh. Kalemani tumbua huyu Manager km ulivyofanya kwa Yule wa Kidatu!
 
chibalangunamchezo

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,543
2,000
Acha uchochezi kumbuka miundombinu sio rafiki hasa kipindi hiki cha mvua
Nyie ndo mnawapa kiburi hawa, bageti iliyotolewa kwa wizara husika nadhani inatosha sana ku sovu hayo yote, unasema mazingira siyo rafiki Kwani nchi nyingine ambazo hazina matatizo ya umeme mvua hazinyeshi?
 
LENDEYSON

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
2,980
2,000
Acha uchochezi kumbuka miundombinu sio rafiki hasa kipindi hiki cha mvua
Kwa hiyo mvua zikinyesha itabidi Viwanda visitishe Uzalishaji? MH. Magufuli ana kazi kubwa sana kwa akili za hivi! Huo Uchumi wa Kati tusubiri Yesu Kristo arudi!
 
SaaMbovu

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
5,987
2,000
Maeneo mengi ya Jiji la Mwanza Mgao wa Umeme ni mkali haswa! Tumebaki tunajiuliza, hawa wapo tayari kumsaidia Mh. Rais kukamilisha ndoto yake ya Tanzania ya Viwanda? Viwanda hivi vinahitaji Nishati muda Wote, lakini huwezi kuamini imeshakuwa ni kila Leo Umeme kukatika kwa masaa mengi tu, huo uzalishaji mnataka utumie biogas?
Maeneo ya Mkolani,( ambapo Kuna substation), Buhongwa, na Nyegezi kwa uchache, hayana Umeme hadi muda huu, Mh. Kalemani tumbua huyu Manager km ulivyofanya kwa Yule wa Kidatu!
Mkuu kumbuka kuwa pia kuna natural disaster au causes. Wiki 2 zilizo pita nilikuwa Ngudu na kulikuwa na upepo mkali sana. Kama umewahi kufika Ngudu, kabla hujafika Ngudu mjini kwenye kona ukitokea Jojiro upepo huo ulisababisha nguzo 22 kukatika na kusabisha watu kulala giza siku 2. Waliokuwa wanafika pale wanatamani waisaidie TANESCO but hawana wataalamu nami nilitamani kuwasaidia. Sasa fikiria nguzo hakuna hata 1 iliyooza na bado zilikatika.
Pia kumbuka Mwanza inaathiriwa sana na ndege wale wakubwa. Akipigwa shot na akinasa mpaka uje ugundue huchukua muda kutafuta tatizo lilipo.
Kama unaelewa mambo ya technical huwezi kuja kupiga kelele huku.
Usijilinganishe na wazungu maana wao wanasiasa safi. Viongozi watafukuza sana but umeme utaendelea kukatika kama kuna natural reasons.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom