Tanesco msituchezee akili -- maboresho yenu ya LUKU yamekwama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco msituchezee akili -- maboresho yenu ya LUKU yamekwama!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Sep 1, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa Tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya Tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama Tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

  Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.
   
 2. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  hawa jamaa ni vilaza sana...afu eti leo hawafanyi kazi kwa hiyo tukae na giza paka jumatatu wameniuzi sana.....vilaza wakubwa..
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami nimesikia watu wanalalamika hivyo. Ndiyo maana wengina huamua kuiba umeme.
   
 4. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Na kwa ujinga wao leo badala ya kukifanya kitengo cha luku kufanya kazi masaa 24 wao wanafanya nusu siku! Akili ya matope matupu.
   
 5. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Zaidi ya 80% ya Watz hawafanyi kazi ipasavyo siajabu hata wewe mwenyewe haufiki kazini kabla ya 07:30 asubuhi muda uliopangwa na Serikali na siajabu kila siku unasign chini ya mstari, hili halioni ila unaona ya wenzio tu Tanesco, kifupi sisi Watz hakuna anayefanya ipasavyo wote wazembe kwa namna moja au nyingine aidha tunachelewa kufika sana kazini au tunawahi kutoka (kutoroka) au tunakwenda lunch kwa saa nzima, na yote hayo tunayafanya hatuyaoni kwa maana wanodhurika ni wengine ila mzunguko ukienda ukikufikia ndio unaanza kulalamika kama hayo ya Tanesco!

  Hivyo kuwalaumu Tanesco kwamba hawafanyi kazi masaa 24 ni kuwaonea tu Watz karibu wote tuko hivyo, siajabu na wewe ukafit ktk hao niliowaleza hapo juu jibu unalo wewe mwenyewe kwenye nafsi yako!
   
 6. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nataka kununua leo nikasita nakuhisi mipango yao lazima kuwe na itilafu.
   
 7. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ID yako imenipa majibu kibao ya ulichoandika hapo juu.
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Acheni uongo hamuoni aibu sura mbayaa
   
 9. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  uongo upi mkuu.???
   
 10. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Haijalishi lakini ndio hivyo what goes around comes around!
   
 11. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Haya ndio madhara ya kukurupuka! Tangazo limetolewa wiki nzima kuwa: nunua umeme kuanzia tarehe 1 Sept, ktk Ofisi za TANESCO au Wakala walioorozeshwa na TANESCO . Siyo ma agent wote wanauza token!
   
 12. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Nimekwenda kununua umeme kwa "wakala" kama tangazo linavyosema. Nilikuta foleni kubwa kiasi na kupitia hiyo nimejifunza jambo. Baada ya watu kadhaa kununua umeme alitokea bwana mmoja ambaye alipata karatai moja tu badala ya tatu (mbili zikiwa ni key changer). Yule dada aliyekuwa anahudumu akamwambia kuwa nenda kajaribu kuingiza hizo token na kama zikigoma chukua namba ya TANESCO imebandikwa hapo nje uwapigie kwani ndio maelekezo yao yalivyo. Mie sikuridhika na hali hiyo ndipo nikaanza kufanya utafiti kwa nini baadhi wapate karatasi moja tu. Ndipo akajitokeza mzee mmoja na kueleza kuwa maboresha yanalenga kuwakamata wale wote waliounganishia umeme na vishoka. Na kwamba kwa wasiopata vikaratasi vitatu wako matatani! Na ndio maana maelekezo ni wao kuwasiliana na ofisi za TANESCO. Hivyo usitokwe mapovu bure, huenda ni mmoja wao.
   
 13. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mimi nilifikiri hawa jamaa kwavile wanajiendesha kibiashara, wangefanya kazi masaa mengi zaidi ili wakusanye fedha za kujiendesha badala ya kuomba ruzuku ya serikali( kodi yetu) kila siku! Hawa siyo wabunifu/uchungu na shirika lao. Pamoja na monopoly waliyonayo hivi sasa kwenye umeme, bado biashara inawashinda!
   
 14. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mie nilipata ujumbe huu:
  TANESCO will be upgrading LUKU system on 01/09/12. You are required to purchase LUKU from vendors. Thereafter, you will continue purchasing LUKU with M-PESA.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Uwongo huo. basi watu wote wamefungiwa luku na vishoka? kama ni hivyo basi wafanyakazi wote wa Taesco ni vishoka pamoja na magari yao n.k.

  nani aaminike? Watz waende ofisi gani sasa wapate kufungiwa Luku ya halali?
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yule dada Badra inabidi atoe tamko haraka, ama sivyo kuna watu watalala giza hadi J3 na Tanesco kukosa mabilioni!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Unachotakiwa kufanya ni hivi: Ukienda kutaka kufungiwa Luku, kuna fomu pale lazima uipate ya kuwataka mafundi watakaokufungia Luku watie saini zao na kujifunga kabisa kwamba wao siyo vishoka!
   
 18. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tumuamini nani sasa ama ndio za mbayuwayu.
   
 19. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mimi nimepata hivyo vikaratasi vitatu na nimeingiza namba lakini hakuna umeme unaoingia...nimekwenda kwa hawa jamaa wa luku wameniambia inabidi kwenda tanesco kubadiishiwa sijui vidudu gani! hiyo ni mpaka j'tatu na nikiangalia kilichosalia kwenye luku kunifikisha j'tatu ni 0.64! 'mamae zao tanesco!
   
 20. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280

  Sina la kusema zaidi.
   
Loading...