TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

wanajua nn kinaendelea wanajidai gesi gesi hamna cha gesi wala nini
 
[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]


Inaonekana ni jibu zuri la kitaalam toka kwa ingineer sasa kwanin kuna mgao??ndo swali la msing
 
Arusha imekuwa ni kawaida sasa, wanasubiri oct 25.
 
kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.

Mnafanya siasa badala ya professionalism hayo masuala yanajulikana tokea mradi unaanza mnapaswa kutoa taarifa zote kwa mapema na kwa wakati muafaka ili watu nao wajipange mara tunaboresha vituo vya kupozea umeme,mara tunaingiza gesi kinyerezi,mara tunajaribu mitambo mara tunawasha mitambo vyote hivi huwa vinajulikana tokea mwanzoni kwa nini msitoe projection yote nzima acheni ubabaishaji!.
 
Unapotokea mgao, TANESCO imekuwa na uharaka wa kuelezea. Mara husemwa kuna matengenezo kwenye njia za umeme. Mara husemwa kuna hitilafu kwenye mitambo ya sehemu fulani. Mara husemwa kuwa kuna maboresho na kadhalika.

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchemi Mramba aliuambia umma wa watanzania kuwa mitambo ya umeme wa gesi kutoka Mtwara imewashwa na hivyo umeme kuwa wa kutosha Dar es Salaam na kwingineko. Bado mgao wa umeme unaendelea kwenye jiji la Arusha na hata hapa jijini Dar es Salaam pamoja na kuwashwa kwa mitambo hiyo ya umeme wa gesi.

Nawauliza TANESCO, mgao huu wa umeme unaoendelea nchini Tanzania unatokana na nini tena?

Nchi ya mazoea chini ya utawala Wa CCM usitegemee majibu sahihi
 
Watanzania tunahitaji elimu.
CCM wananufaika na ujinga wetu.
 
Kiukweli hii hali inauzi na kuumiza sana. Kibaya zaidi ni kwamba TANESCO WAMEKUWA WAKITOA AHADI NA DEADLINE YAKUMALIZA TATIZO LAKINI INAPOFIKA TAREHE YA MWISHO WANAKUJA NA SABABU INGINE.

Ni vema kama kuna tatizo kubwa wananchi waelezwe tu ukweli wakajua. Otherwise wanatufanya kama watoto.

Nashauri kama Magufuli anauchungu kweli na wananchi basi alikemee hili KIPINDI HIKI KABLA HAJACHAGULIWA
 
Naamini hakuna cha gesi wala nini, hyo ni danganya toto tu. Tatizo nchi yetu ni yakisanii. wakati inawashwa mitambo walituhakikishia kuwa umeme utakuwa wa uhakika. one day after tatizo linaendelea. kwa style hii mtz kuendelea ni shida. wengine huku umeme umeshakuwa anasa. unarudi usiku na alfajiri unakatwa.
 
[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye Mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]

kauli za namna hii hazijaanza leo,tumeshazizoea na hazileti any change isipokuwa tu zile kauli za "umeme utapanda bei" huwa na effect hapo hapo,ikitangazwa leo,basi kesho asubuhi bei juu,ni hilo tu ndio mnaloliweza,stupid!
 
kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye Mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.

ina maana kazi hii itakamilika baada ya uchaguzi
 
Hakuna cha mtambo wa gesi wala nini. Kipindi hiki ndio kuna mgao mkubwa kuliko kipindi kingine cho chote Tz. Nafikiri gesi ya Ntwara imegoma kuja. Ndio maana wakasema sijui inatkiwa ifike 52psi wakati iko 20psi. CCM na serikali yake hawana uwezo wa kurekebisha matatizo waliyoyaunda wenyewe. October mwisho
 
Suala la kwamba mitambo inaunganishwa na gesi ya Mtwara ni propaganda ili CCM ipate kura, nina hakika kama kweli gesi hiyo ingekuwa imeunganishwa kusingekuwepo mgao huu unaoendelea. Ukweli ni kuwa TANESCO imefilisika, na Mtera kina maji kimepungua kwa kiasi kikubwa. Suala la gesi kuunganishwa kwenye mitanbo ni hadithi za alinacha.
 
Halafu mie nashangaa wakati mitambo ya diesel mwanza inazinduliwa walisema mgao wa umeme kanda ya ziwa itakuwa historia
huku geita unakatika daily asubuhi unarudi jioni ila jana umerudi saa moja jioni ukakatika tena saa tisa usiku sasa sijui mafundi walikuwa kazini usiku huo?
Mbaya zaidi hawatuambii na kwa wale wanatumia mita za.zamani ukichelewa kulipa siku mbili tu wanachomoa fyuzi
au gas imeisha yale matrilio ya ujazo yameshauzwa china?
 
[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye Mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]

Acha kudanganya watu mkuu.Hakuba kitu kama hicho zaidi ya kulaghai wananchi wasiojielewa.Tanesco wamesema tatizo litaisha mwezi ujao mwishoni wakitegemea mvua zitakuwa zimenyesha kuweza kujaza mabwawa ya Mtera na Kidatu kwa ajili ya kufua umeme.Hayo mambo ya gesi ni zuga tu ili kusogeza siku.
Naamini kama sio issue ya Uchaguzi basi nchi ingekuwa gizani kbsa.
 
ccm ikishaondoka ndio tatizo la Umeme litaisha, Kama wangekua wana uwezo wa kulimaliza wangefanya muda huu ili wasikose kura. Uwezo wao umefika mwisho, hawana suluhisho, tuchague wenye majibu ya tatizo la Umeme.
 
Kwa zaidi ya mwezi sasa TANESCO wamekuwa wakikata umeme karibia nchi nzima kwa muda wa kuanzia masaa 8 hadi 12. Pale awali tulielezwa kuwa katizo hilo la umeme litakuwa kwa muda kama wa wiki moja hivi kwani walikuwa wanaingiza umeme wa gesi kwenye gridi ya taifa, ivyo basi wananchi sasa tungepata umeme wa uhakika.
Lakini wapi, umeme unakatika tena katika kiwango kikubwa zaidi, kwa mfano leo Kimara umeme umekatika saa 10.55 alfajiri na kurudi ni mpaka saa 1 usiku.
Sasa TANESCO jitokezeni mtuambie wananchi shida ni nini...!!?? Maana tunasikia sijui hamjawalipa SYMBION ivyo wameuondoa umeme wao kwenye gridi ndio maana kuna huo upungufu, wengine wanasema ni mgao kama wa miaka mingine nk nk.
Tunataka umeme wa uhakika na sio fix-fix.. mara sijui umeme utashuka bei, utashuka bei vp wakati upatikanaji wake ni wa namna hii ya kimagumashi magumashi...!!
Tumelichoka kabisa hili shirika wana jamvi.
 
Back
Top Bottom