TANESCO kuweni wakweli kwamba umeme umepanda bei

TUKUYU88

Member
Jul 25, 2022
63
196
Ijumaa nilienda ofisi ya TANESCO kuulizia kama naweza kubadilishiwa matumizi ya umeme na kuwekwa kwenye matumizi madogo baada ya kutumia umeme wao kwa miezi mitatu toka nilipounganishwa na line yao.

Nikaambiwa kwamba kwa mjini hicho kitu hakipo, hiyo huduma ipo upande wa vijijini na kama ni mjini basi ni zile kaya masikini.

Je, kwanini hawatangazi wazi ili tujue? na kwanini Waziri Makamba alipinga Bungeni kwamba umeme haujapanda (au hicho kitendo sio kupanda)

Je, ina maana mtu anayetumia umeme majumbani hivyo atakuwa sawa na yule anayetumia umeme kibiashara(eg mwenye mashine ya kusaga?)

Hapa kumbe ni kuhamia tu kijijini ili mjini wabaki peke yao.
 
Kero kubwa ambay TANESCO wameitengeneza, ni pale umeme unapokuwa na tatizo ukawapigia kwa namba yao ya dharura ambayo ni 0754 550 000.

Hiyo simu ukipiga inaunganishwa moja kwa moja na huduma kwa wateja huku ikiendelea kutoa matangazo na bill ikikatwa bila mfanyakazi wa TANESCO kupokea simu. Unaweza kutumia hata masaa mawili bila kuongea na kutoa taarifa. Yaani usiombe upate hitilafu ya umeme ndo utaona hawa TANESCO hawafai.
 
Ndugu mteja

Tafadhali pokea ufafanuzi sahihi kutoka TANESCO, tunakujulisha kuwa bei ya umeme hainajabadilika toka mwaka 2016 ilivyoidhinishwa na mdhibiti ( EWURA),

Kuna makundi manne ya watumiaji wa umeme kama ifuatavyo

-D1 (UNIT 0-75) BEI NI TSH 100 KWA UNIT IKIZIDI UNIT 75 INAKUWA TSH 350 (YAANI UMEME WA 9150 KWA MWEZI)
Masharti

1.Makazi ya kijijini
2.Matumizi ya nyumbani
3.Wastani wa matumizi usizidi unit 75 kwa mwezi

-T1 UNIT zaidi ya 75 to 7500 Bei ni 292 per unit,Hakuna tozo ya kila mwezi

-T2 Gharama kwa mwezi ni 14,233, gharama ya umeme kwa ni 195 kwa unit

T3- M - gharama ya huduma kwa mwezi ni 16,769 na bei ni tsh 157 kwa unit

T3-gharama ya huduma kwa mwezi ni 16,550 na bei ni 152 kwa unit

Bei zote ni bila VAT 18% REA 3% na EWURA 1%
 
Tafadhali tujulishe ulipiga lini namba yako ya simu kwa kufatilia na kuchukua hatua
 
Ndugu mteja

Tafadhali pokea ufafanuzi sahihi kutoka TANESCO, tunakujulisha kuwa bei ya umeme hainajabadilika toka mwaka 2016 ilivyoidhinishwa na mdhibiti ( EWURA),

Kuna makundi manne ya watumiaji wa umeme kama ifuatavyo

-D1 (UNIT 0-75) BEI NI TSH 100 KWA UNIT IKIZIDI UNIT 75 INAKUWA TSH 350 (YAANI UMEME WA 9150 KWA MWEZI)
Masharti

1.Makazi ya kijijini
2.Matumizi ya nyumbani
3.Wastani wa matumizi usizidi unit 75 kwa mwezi

-T1 UNIT zaidi ya 75 to 7500 Bei ni 292 per unit,Hakuna tozo ya kila mwezi

-T2 Gharama kwa mwezi ni 14,233, gharama ya umeme kwa ni 195 kwa unit

T3- M - gharama ya huduma kwa mwezi ni 16,769 na bei ni tsh 157 kwa unit

T3-gharama ya huduma kwa mwezi ni 16,550 na bei ni 152 kwa unit

Bei zote ni bila VAT 18% REA 3% na EWURA 1%
SASA KWA MTEJA MPYA AMBAYE AMETOKA KUFUNGIWA LINE ANABADILISHIWA MATUMIZI BAADA YA MUDA GAN? YAANI KUMTATHINI NA KUMUWEKA KWENYE GROUP ANALOSITAHILI NI BAADA YA MUDA GANI? MAANA MIMI TOKA NIFUNGIWE LINE YENU IMEPITA MIEZI MITATU NA MATUMIZI HAYAJAWAHI ZIDI UNIT 75 KWA MWEZI.
 
Ni ndani ya mieiz mitatu
 
Njoo in box tukafanye mambo umeme unanunua wa 20,000 tu kwa mwezi
 
Back
Top Bottom