TANESCO: Kupanda bei ya umeme hakutaathiri wateja wa kawaida

Hao watumiaji wakubwa ndio wazalishaji wakuu wa bidhaa. Kuwaongezea gharama za umeme kutasababisha kupanda kwa gharama za bidhaa zao hali itakayowaathiri wananchi wa kawaida ambao ndio watumiaji wa mwisho. Serikali isimamie hilo kuhakikisha kuwa hakuna kupata kiholela kwa gharama za umeme
Aise umesema kweli
 
vat kwenye miamala simu walisema hivi hivi,vat kwenye mihamala ya mobile money transactions walisema hivi hivi,ila kilichotokea wote twajua!
 
Huo ni usanii mtupu. Wateja wadogo hawataathirika kwa namna ipi? Hao wateja wakubwa ni industrialists/manufacturers wakishazalisha mali zao watakwenda kuuza India ili sisi cos isituathiri? Jamani acheni huo usanii;watanzania wa Leo tumesoma na tunaongea ufahamu mkubwa sana. Hatudanganyiki. Muwe ni wa wazi tu kwamba mnatafuta hela za kulipia std had bank Hong Kong Siyo vinginevyo. Yaani sisi tuwalipie wale waliosema visandarusi na singasinga? Aaah wapi tutamtimua tu Mungu
 
Nadhani kuna haja ya kufuta EWURA,kwa sababu ya conflict of interest,umeme ikipanda na wenyewe hela inaongezeka sasa watamtetea nani?
 
Hivi Tanesko sio jipu?,au limekaa sehemu mbaya?,naona jitia kulalamaa,ila naamini wako kwenye foleni docta at a washughulikia tu
 
Hao watumiaji wakubwa ndio wazalishaji wakuu wa bidhaa. Kuwaongezea gharama za umeme kutasababisha kupanda kwa gharama za bidhaa zao hali itakayowaathiri wananchi wa kawaida ambao ndio watumiaji wa mwisho. Serikali isimamie hilo kuhakikisha kuwa hakuna kupanda kiholela kwa gharama za umeme

Usipost tena ukiwa Lumumba

Kumbe ukipostia huko uliko unakuwaga na akili kidogo

hakikisha hurudii tena matapiko
 
Usipost tena ukiwa Lumumba

Kumbe ukipostia huko uliko unakuwaga na akili kidogo

hakikisha hurudii tena matapiko
Hadi nimedoubt kama ni yeye au account yake imekuwahacked... Kwani hao wateja wakubwa sio watanzania? Gap ya maskini na tajiri haitakaa ipungue kama mambo ndo haya!
 
Lizaboni Leo umeongea bonge la point mshikaji wangu

Hao watumiaji wakubwa ndio wazalishaji wakuu wa bidhaa. Kuwaongezea gharama za umeme kutasababisha kupanda kwa gharama za bidhaa zao hali itakayowaathiri wananchi wa kawaida ambao ndio watumiaji wa mwisho. Serikali isimamie hilo kuhakikisha kuwa hakuna kupanda kiholela kwa gharama za umeme

big up brother
 
Hata gharama za mitandao ya simu mlitudanganya hivyo hivyo ,saivi mnatukata hadi VAT hadi vocha za simu .....mxiuwwwwwwww
 
Yaani ametuona sisi watz hatunazo anaongea uongo ambao sio professional at all.
 
hao ndio wasomi wetu wa TZ, ukimpandishia gharama za umeme bakharesa si atapandisha bei ya sembe, mtu wa chini si atazidi kuumia? Hivi akina muhongo si walituahidi tanesco wakianza kutumia gas umeme utashuka sn bei? kweli wa tz tumelaaniwa
Tulishaambiwa kuwa ikitokea mwanasiasa akaongea ukweli labda atakuwa anataja jina lake tu.

Tanesco wenyewe mwaka huu waliposhusha asilimia 1 na kuondoa service charges waliahidi kuwa sasa bei itashuka zaidi kuanzia mwakani baada ya kuanza kutumia umemeutokanao na gesi. haya ya kupandisha ni mapya kabisa. ila sitashangaa kama wananch hawakumbuki lolote kuhusu suala hili.
 
Hivi kwanini matamko mengi ya viongozi wetu hayahusishi ubongo. Umeme ni nishati. Nishati hii hutumika kwenye uzalishaji. Nayo huongezwa kwenye gharama za uzalishaji. Na ili mzalishaji atengeneze faida ni lazima bei ipangwe juu ya gharama za uzalishaji. Ukipandisha bei ya umeme, unaongeza gharama za uzalishaji na consequently kupandisha bei ya bidhaa husika. Worse enough chanzo cha umeme cha bongo ni HEP, hiyo gesi porojo tu... bora tumgekuwa tunafua umeme kwa mbinu tofauti kama kuwa na geothermal, wind mills, extensive solar mills... hapo tusingewaza gharama za umeme. Kina cha maji kikipungua mabwawani umeme mtaani unakuwa wa mgao. Embu acheni ubongo uplay part kwa mnavyovizungumza
 




Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa watumiaji wakubwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu mapendekezo yaliyo wasilishwa na mamlaka ya udhibiti wa huduma Za nishati na maji EWURA.

“Niwatoe hofu wananchi kwamba yale mapendekezo tuliyoyapeleka wananchi wa kawaida wale wanaotumia umeme mdogo bei zao hazitaathirika sana. Kuna jambo moja ambalo tumelitazama kwa mtazamo tofauti, unajua sasa hivi we mteja wa kawaida unalipa sawasawa na kampuni zinazoweka mabango barabarani ambazo ni kampuni za kibiashara,” alisema Mramba.

“Sasa katika mapendekezo tuliyopeleka EWURA tulikuwa tunamuomba aangalie kwamba yale makampuni yanayofanya biashara za mabango ya matangazo yasilipe sawasawa na mteja wa nyumbani bei yake iende juu zaidi.”
Hata kodi kwenye miamala mlisema hivyo hvyo watu wa chini hawataguswa bali ni makampuni sasa hivi tunateseka. Wabongo tushaonekana mijinga hatujielewi tunalalamika siku moja then tunasahau...
 
Back
Top Bottom