ngudengude
JF-Expert Member
- Jul 2, 2015
- 1,175
- 466
mkulu kampa wizara homeboy wake , tatizo la homeboy kapewa wizara imemzidi uwezo anaharibu. Kwanza wizara imegawanywa mara mbili kwa maana kapunguziwa mzigo lakini bado inamshinda!Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kama kweli dhamira yake ni Tanzania ya viwanda hana budi kuisafisha TANESCO kuanzia waziri hadi kwa maofisa wote.
TANESCO imeendelea kuwa shirika la hovyo kabisa umeme hauna uhakika kabisa TANESCO haina hata uwezo wa kutoa huduma kwa masaa 12 bila umeme kukatika, kwa siku umeme hukatika hata Mara 8-12.
Pr. Mhongo alijitahidi sana tulianza kupunguza matatizo sasa yamerudi kwa kasi. Kama tunaitaka Tanzania ya maziwa na asali ni lazima TANESCO ifumuliwe.
Mungu ibariki Tanzania.