TANESCO jipu, Prof. Muhongo ndiye waziri bora wa nishati kuliko mawaziri wote katika sekta hii ya nishati

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,732
7,611
Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kama kweli dhamira yake ni Tanzania ya viwanda hana budi kuisafisha TANESCO kuanzia waziri hadi kwa maofisa wote.

TANESCO imeendelea kuwa shirika la hovyo kabisa umeme hauna uhakika kabisa TANESCO haina hata uwezo wa kutoa huduma kwa masaa 12 bila umeme kukatika, kwa siku umeme hukatika hata Mara 8-12.

Pr. Mhongo alijitahidi sana tulianza kupunguza matatizo sasa yamerudi kwa kasi. Kama tunaitaka Tanzania ya maziwa na asali ni lazima TANESCO ifumuliwe.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Sijui jamaa hutumia kigezo gani kutoa watu.

Lameck wizara imemuelemea mpaka anatia huruma lakini wapi, yupo tu....anaonekana ana perform kweli kweli.
 
Mi nadhani umeme ungefanywa soko hulia kama makampuni ya simu, hapo mwanzo tuliteswa sana na TTCL baada ya biashara ya simu kufanywa hulia tunaona matunda kampuni hii ikizingua unahamia hii mpaka raha, Kama ikitokea kampuni nyingine ya umeme mimi nitakuwa wa kwanza kuachana na TANESCO, they are big fools, wanakula tu pesa yetu hatuoni wanachokifanya, gharama za huduma yao ni kubwa mno.
 
Mkuu kwa usalama wa uchumi wa taifa ni jambo jema kutofanya hiki ulicho shauri.

Unasahau mgomo wa wauza mafuta kipindi cha Mh. Kikwete?
Unasahau mgomo wa kampuni za usafirishaji?

Unafikiri ikiwa TANESCO chini ya mtu binafsi kisha akafanya mgomo wa kuuza au kuwasha umeme na wakati huo huo ukatokea mgomo wa waagizaji au wauzaji mafuta wakubwa nchi itabaki salama?

Uchumi utaanguka moja kwa moja na maisha binafsi ya kila mmoja wetu yatakuwa mabaya sana.
 
Mkuu siyo kuwa lazima Mhongo arudishwe Nishati lakini Raisi aangalie mtu bora wa kumpa hii wizara bila kujali maslahi ya chama ccm inamwangusha Rais J.P.M
Tatizo mauteuzi haya ya ukabila ndiyo yanatugharimu. Waziri wa nishati kama asingekuwa wa kutoka kule tayari angeshatumbuliwa.
 
Sijui jamaa hutumia kigezo gani kutoa watu.

Lameck wizara imemuelemea mpaka anatia huruma lakini wapi, yupo tu....anaonekana ana perform kweli kweli.
Tanesco imeshindwa na kabisa na kama itaendelea hivi miezi 6 ijayo inawezekana umeme ukawashwa ktk taasisi mhim tu.
 
Magufuli kaja kutualibia nchi yaan kavuruga system waliokuwa wameweka watangulizi badala ya kuboresha yeye anabomoa.

Swissme
Shida kubwa niliyoigundua kwa Mkuu wa inchi ni kususiwa na wenzie wana ccm wanafiki ndio wanaomwangusha magufuri ila kwa sababu Rais nae anapenda kusifiwa kama ilivyo watu wa kanda ya Ziwa anadhani wanamshangilia kumpenda hajui ni unafiki
 
Muhongo ni bure kabisa, Nishati haimuhitaji, inahitaji kufumuliwa na kupangwa upya.

Nyimbo za umeme wa gas sijui nini UVCCM waliziimba sana, huo umeme uko wapi na gas iko wapi?

Mliamua kuchagua mvurugaji mkuu, hata mfanyeje, atavuruga tu.miaka 2 ijayo mtaweka foleni kununua kilo moja ya sukari.
 
Back
Top Bottom