TANESCO jipu, Prof. Muhongo ndiye waziri bora wa nishati kuliko mawaziri wote katika sekta hii ya nishati

Hivi ni ccm inamwangusha ngosha au ngosha anaiangusha ccm ?
Ccm ndio inayo mwangusha maana wamekuwa wanafiki wanapongeza kila kitu kwa sababu wapate teuzi wajinemeshe na familia zao hawana ukweli wanaomwambia na fahamu mnafiki ni mtu mbaya sana Bora uishi na mwizi , mchawi kuliko mnafiki
Maana hukupaka mafta kwa mgongo wa chupa
 
Amrudishe Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi, ameondolewa akiwa anatekeleza wajibu wake (bila kosa lolote).
Kwasababu tunataka Tanzania ya viwanda haina budi kutafta watu sahihi wenye mtizamo wa mbali ili Tanesco matatizo yaishe kabisa
Ikiwezekana Tanesco itaftiwe mwekezaji kwa namna bora ambayo haitaliingiza taifa ktk mgogoro kiusalama na kiuchumi
 
Chief Impongo nakubaliana Na Wewe Atleast Prof Muhongo Aliiweza Wizara Japo Kwenye Madini Alichemka Lakini Kwenye Nishati Nampa Big Up.

Lakini Pia TANESCO tatizo Lao kwa Sasa Ni Mkurugenzi wao Huyu Dr Tito Mwinuka Kiukweli Hana Uzoefu Wowote Katika Kuendesha Taasisi ya Nishati Kama Tanesco Compared to ENG. FELCHESMI MRAMBA huyu Alikuwa Mtaalamu Katika Masuala Haya Na Pia Mwenye Uzoefu Mwingi.

Kiukweli Huyu Mkurugenzi wa Sasa wa Tanesco Bado Anajifunza Kazi so Tusubirie Labda Baada ya Miaka 6 au 7 akizoea Kazi ndo Mambo yatakwenda Sawa.
Huwezi kutafta uzoefu juu ya maisha ya watu hapa ndio huwa nachukizwa na wanasiasa unawezaje kuweka mtu asiye na uzoefu wala utaalam sehem nyeti kama Tanesco?
Tanesco ni kaburi la uchumi wetu ni lazima itafutwe namna bora kuiendesha Tanesco ikiwezekana ibinafsishwe ila baadhi ya sehemu nyeti ziendelee kuwa chini ya serikali kwa sababu ya kiusalama
 
Ilisikika sauti ifikapo 2018 may umeme kukatika itakuwa ni historia
Imekuwa tofauti Leo ni March mabwawa yamejaa maji hakuna kisingizio tena kwa kweli sijui tumerogwa na nani?
 
Umesema kweli katika Dunia ya teknolojia unahitajika ushindani wa kimtazamo hapo ndio tutafika mbali ila tanesco akijiona yupo peke yake ndio matokeo haya

Mfano
Benki zipo nyingi na mchuano ni mkubwa kutafta wateja.
Mitandao ya simu kuna makampuni mengi na ushindani ni mkubwa lakini je tungeacha TTCL peke yao hivi leo tungekuwa wapi?
Nahisi hadi leo tungekuwa kwenye teknolojia ya cdma ya china badala ya gsm inayotumika ulimwenguni kote! Ttcl mtandao wa hovyo sana utafikiri sio wa serikali
 
Kama vipi aishikilie yeye mwenyewe hiyo wizara kwa muda mpaka mambo ya umeme nchini yatakaponyooka.
Yeye mwenyewe maknikia imemshinda alimweka kairuki kama picha lakini sasa hivi picha lilikoishia Sterling kafa labda movie litengenezwe tena
 
Na imekuwa kweli kuwa sasa hivi mgawo wa umeme ni historia tunayoiishi kila siku.
Siasa za kiafrika ni upuuzi yani mtu anasimama mbele ya watu anawadanganya na watu wanapiga makofi miaka yote kwa kweli afrika inahitaji ukombozi tena.
 
Unaweza kuwa upo sahihi lakini kwa mtazamo wangu naona athari au tuite unyeti wa sekta ya nishati ni wa juu sana kuliko mashirika ya usafirishaji kama ndege au mabasi.

Mgomo wa umeme kwa wiki moja utakuwa na athari kubwa sana kwa uchumi na usalama wa nchi kama vile mgomo wa madaktari kuliko mgomo wa ndege za abiria au mabasi ya abiria.
Mkuu tunaweza kubinafsisha baadhi lakini tukaendelea na Tanesco ya kuhudumia sehem nyeti kwa ajiri ya usalama na hata huku kwingine kwa ajiri ya kulinda kurndeshwa na mwakezaji itabidi tumiliki hisa zinazotufanya kuwa na nguvu kubwa ili tusiyumbishwe na wawekezaji.
 
Umeme now days n kero kubwa,waziri kila siku yupo kwenye TV mikwala mingi lakn umeme bado n big problem.
Tatizo la mawaziri wengi kwa sasa wanafanya kazi kwenye TV na uongo mtupu wanachosema hakina uhalisia kabisa
 
lakini sio prof, muhongo
Prof. Mhongo kwa sasa hatufai kwanza haamini kama mtanzania anaweza kufanya jambo la maana kwa hiyo ni kama ana laana ya fikra.
Tunahitaji wachapa kazi sahihi wenye mtizamo chanya wa kuijenga Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati si hawa wa kujitangaza ktk TV.
 
Mkuu umesahau kuwatag wapo humu.
Kipindi cha profesa ukatikaji wa umeme ulikuwa umepungua sana.wakamfukuza na yule bwashee kwa fitnafitna.
Tanesco kimekuwa kama kijiwe cha siasa si watendaji kama tunavyotaka na Rais kama kweli anaitakia mema Tanzania ya viwanda ni lazima Tanesco ifumuliwe au aangalie namna bora ya kuongeza ufanisi au abinafsishe
 
Umeme ni bidhaa muhimu sana katika uchumi,huwezi kufanya kama kilichofanyika TTCL, Tanesco ingeanguka anguko la TTCl hapo siku za nyuma basi inchi ingekuwa katika hali tete. Ukumbuke uwezi kuweka bidhaa kama umeme rehani kwa kumilikiwa na watu binafsi siku wakiweka kamgomo ujue umekwisha.
Mkuu ni tofautiane na wewe maana unaweza kubinafsisha kwa makubaliano ya wewe kuendelea kumiliki hisa 51% na ukabakia kuwa msemaji wa mwisho na ukapata uzoefu zaidi hata kama mwekezaji anaondoka tayali utaweza kujiendesha kwa manufaa zaid
 
Mramba alikuwa mtaalamu wa umeme aliyebobea. Rais kamwondoa bila sababu ila kwa kuwa tu katoka kanda fulani. Sala yake haitatuacha salama. Katuletea mtu wanadharia ya darasani. Wote madoctor na maprofesa ni bure kabisa kwenye kazi za kweli. Mwimu bora darasani siyo mtendaji bora. Waziri wa Ardhi imu ya kawaida lakini anafanya vema. Prof au doctor gani anayefanya vizuri kwenye mbuga, warudi madarasani!
Tatizo ni siasa za kinafiki
 
Prof. Mhongo kwa sasa hatufai kwanza haamini kama mtanzania anaweza kufanya jambo la maana kwa hiyo ni kama ana laana ya fikra.
Tunahitaji wachapa kazi sahihi wenye mtizamo chanya wa kuijenga Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati si hawa wa kujitangaza ktk TV.
Ni kweli watanzania hatuwezi la maana. Tuambie lipi tumeeeza?
 
Nakuunga mkono mkuu kwa Rais kuisafisha TANESCO from top to bottom,ni kweli ni jipu.Hata hivyo nadhani Muhongo sio suluhisho,yeye pia alikuwa sehemu ya tatizo.
Kwa sasa hatumuhitaji mhongo kwa sababu alisema hakuna mtanzania anaweza kuwekeza kitu cha maana labda kutengeneza maandazi na juice
Ni lazima tusiingize siasa ili tuiokoe Tanesco kama kweli raisi wetu ana nia ya dhat na Tanzania ya viwanda
 
Back
Top Bottom