TANESCO itafutiwe mshindani wa kibiashara?

Mkuu umeelezea kitu kizuri sana, naaminj umetufungua wengi.
Hivi mfano haiwezekani kua na kampuni nyingine ambayo itazalisha umeme kwa kutumia windmills?

Au kutumia malighafi zingine ambazo teknolojia ya TANESCO bado haijawa na uwezo nayo?

Tatizo ni shirika la kusambaza umeme kama linaemdeahwa kihuni na kungizwa kwenye mikataba mibovu hatakama unalazishwa bure lazima watumiaji mtaumizwa tuu.
 

..jamaa wa ewura ni kama refarii.

..anatetea watumiaji na wazalishaji.

..pia anaamua baada ya shauri kupelekwa mbele ya baraza la wadau.

..sasa Tanesco walipeleka ombi umeme upande kwa 18% lakini ewura wamewapa 8%. Kwa hiyo utaona kwamba mdhibiti ameangalia pande zote--watumiaji na wazalishaji huduma.

..sasa kwa uelewa wangu sheria ya udhibiti wa hizi huduma inamzuia waziri kuingilia maamuzi yanayotolewa na mamlaka za udhibiti.

..huko tunakoelekea, bahati mbaya ua nzuri watawala huwa hawatuambii ukweli, sekta ya Nishati na Umeme itashirikisha makampuni binafsi.

..Msije mkashangaa sekta ya nishati na umeme ikawa kama sekta ya mawasiliano ambapo kuna makampuni mengi binafsi ya simu.
Ndiko tunakoelekea huko.

..sasa kukiwa na ushindani Waziri hawezi kuingilia na kupangia bei watoa huduma.

..Kwa maoni yangu huu uamuzi ni wa muda tu kulingana na upepo wa kisiasa. Kinachosababisha Tanesco wapandishe bei ya umeme siyo Wakurugenzi wabovu bali ni mikataba ya kifisadi baina yake na independent power producers kama IPTL na wengine.

..hili suala la Tanesco na kujikanganya baina ya Magufuli na Muhongo kuhusu Tanesco lilishaletwa hapa JF na mwanachama anaitwa HNIC lakini wachangiaji wakawa wanambeza.
 
Phillipo Bukililo ,

..kwanza tukate mirija yote inayoinyonya damu Tanesco.

..mirija hiyo ni mikataba ya kifisadi baina ya Tanesco na makampuni kama iptl.

..baada ya hapo tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuijadili hii hoja yako.

..nimesema haya kwa kuheshimu hoja yako. Ila mimi binafsi napendelea Tanesco iwe na monopoly ktk sekta ya umeme.

.. Natamani Tanesco iwe multinational iweze kutoka Tz na kuwekeza ktk nchi jirani.
 
Nimeingia kwenye hii link ni kweli hawa jamaa wapo committed katika kutatua tatizo la umeme.
Obviusly chain reaction itakayosababishwa na hizi projects itakuza tu uchumi wao.

December 21 wenzetu wanaanzisha project sisi vikao vya kupandisha bei ya umeme vilikua vimepamba moto.
 
Tatizo ni shirika la kusambaza umeme kama linaemdeahwa kihuni na kungizwa kwenye mikataba mibovu hatakama unalazishwa bure lazima watumiaji mtaumizwa tuu.
Hapo nimekuelewa, hivyo kwa maoni yako mkuu suluhisho siyo kuruhusu ushindani ila nia na usimamizi madhubuti ndiyo tatizo?
 
Umeona eh. Tanzania inataka machief executive wa hivi. Sio CEO kazi yake kusaini burua na mikataba tu ofisini. Isitoshe huwa hawasomi uvivu mwingi ndo maana tunaangukia pua kila mala kwa kujifunga kwenye mikataba isiyo na tija kwa taifa
 
Hapo nimekuelewa, hivyo kwa maoni yako mkuu suluhisho siyo kuruhusu ushindani ila nia na usimamizi madhubuti ndiyo tatizo?

Miundombinu mingi hasa umeme uwezi kupata ufanisi kwa kutegemea ushindani wa makampuni binafsi. Hata kwenye nchi kama marekani ambako kuna vigorous private enterprise national grid na nuclear plant zinamilikiwa na serekali au serekali inamkono mrefu. Ndio maana Mchina anamshinda mmarekani kwenye swala miundombinu kwasababu miundombinu yao kama treni niserekeli ina-invest treni za marekani ni zakampuni binafsi zimechoka. CCM wanapenda kujilinganisha na communist part ya china kwakusema demokraaia sio muimu na tunaitaji strong man badala ya institutions. Tofauti ni China communist part wapo serious na maendeleo ya nchi wakati CCM ipo serious na maendeleo ya Mafisadi.
 
Ewura kwa mamlaka waliyo nayo waisaidie tanesco bei ya gas ishuke ili waweza kuzalisha umeme kwa bei ya chini.
 
Kwa hii observation yako mkuu, tatizo letu linaanzia mbali, linaanzia serikali za mitaa zinazoongozwa na mwenyekiti asiyejua kusoma, mbunge aliyeishia la saba mpaka raisi anayetenda kwa interest zake na za chama chake na siyo wananchi.
 
Mkuu umeongea mengi lakaini ni kwa sababu umekariri. Naongelea namna ambavyo nchi inaweza kuondokana na ukiritumba wa TANESCO, namba ambavyo wadau wenye rlimu ya umeme wanavyoweza kujiona wapo nyumbani katika kutumia elimu zao kwa faida ya nchi yetu inayozidi kukua kiuchumi.
 
Kwa hii observation yako mkuu, tatizo letu linaanzia mbali, linaanzia serikali za mitaa zinazoongozwa na mwenyekiti asiyejua kusoma, mbunge aliyeishia la saba mpaka raisi anayetenda kwa interest zake na za chama chake na siyo wananchi.
Kwani chama sio cha wananchi?
 
Kwani chama sio cha wananchi?
Wananchi wote wa Tanzania ni wanachama wa chama kimoja tu?

Jengo la chama lililozinduliwa wiki iliyopita mapato yake watafaidika wananchi au chama?
 
Wananchi wote wa Tanzania ni wanachama wa chama kimoja tu?

Jengo la chama lililozinduliwa wiki iliyopita mapato yake watafaidika wananchi au chama?
Chama kinahudumia wananchi wote kinapokuwa madarakani na hata kile cha upinzani kikiibua madudu ya serikali ni kwa faida ya wananchi wote.
 
Sasa mimi najiuliza tanesco ndoo wanao miliki nguzo zote huyu mshindan wake atatumia nini ili kuwapata wateja ?
 
Chama kinahudumia wananchi wote kinapokuwa madarakani na hata kile cha upinzani kikiibua madudu ya serikali ni kwa faida ya wananchi wote.
Ungeandika hivi 'Chama kinatakiwa kuhudumia....'

Huko kutakiwa nchi kama Tanzania hakukutimizi, kwa kua nchi yetu haijtenganisha chama na serikali viongozi wote wa kiserikali hutokea chamani.
Lakini kama maamuzi yao yanamuumiza mwananchi wa kawaida, huku wenyewe wenye chama wakiishi kama hatupo nchi moja, utaanzaje kusema hiki chama kinahudumia wananchi?
 
Kinahudumia wananchi.
 
Tuna zungumzia hapa kwetu umeme
Apatikane mpinzan atatumia nini kuwafia wateja wake hapa
Nilikuonesha hivyo ili ujue kua nguzo uliyoitaja mara ya kwanza siyo kikwazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…